Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Nimeamua nikazeekee kijijini kwa sababu zifuatazo:-​
  • Kule kijijini nitapata hewa safi isiyokuwa na mchafuko​
  • Kule kijijini nitapata majirani wema wasiokuwa na choyo​
  • Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana bila chuki​
  • Kule kijijini tutakuwa tunakunywa togwa pamoja​
  • Kule kijijini tutapunguza msongo wa mawazo​
  • Kule kijijini tutaingia shamba lolote kuchuma matunda na kula​
  • Kule kijijini tutakuwa tunasikia milio ya ndege na viumbe mbali mbali​
  • Kule kijijini tutafurahia uoto wa asili​
  • Kule kijijini tutakuwa tunaenda kuwinda kama sehemu ya michezo​
  • Kule kijijini tutapata marafiki wengi ambao sio wanafiki​
  • Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana panapotokea mmoja wetu anaumwa.​
  • Kukaa kwenye nyumba ya nyasi yenye hewa safi na ya kuvutia​
  • Kula vyakula vilivyopikiwa kwenye vyungu na kuwa na ladha nzuri​
  • Kendwa kuogelea mitoni na kuvua samaki kama sehemu ya michezo na uwindaji​
Kwa ujumla maisha ya kijijini yatakuwa ni mazuri sana

View attachment 3121969

Kwa nyie mnaobaki mjini, nawaachia mpambane na:-​
  • Majungu na fitina zenu​
  • Mchafuko wa hali ya hewa​
  • Jua kali​
  • Msongamano wa watu​
  • Makelele ya baa na kumbi za starehe zinazoharibu utulivu wa ubongo​
  • Misongo ya mawazo kutokana na changamoto za kimazingira​
  • Kudharauliwa na vijana​
  • Kununua kila kitu; nyanya, yai ,mchicha n.k​
  • Kutokuwa na marafiki wa kweli​
  • Kila mmoja kumuona mwenzie fursa​
  • Kuzeeka kabla ya umri wako​
  • Kupata magonjwa ya moyo na presha n.k​
  • Kula vyakula vyenye kemikali katika kukuzia au usindikaji​
View attachment 3121971

Fanya maamuzi mapema; njoo kijijini tukawinde kanga pori, sungura, n.k pamoja na kuongeza miaka mingi ya kuishi.
Umesahau kusema kule kijijini ukikoma unapata demu safi na fresh kabisa na ukibaki nae huko huko uwezekano wakula wewe mwenyewe ni mkubwa mno
 
Bado unaangaika!? Si mchukuzane na mkeo!? Ni wazo zuri kwa sababu ndiyo maono yangu pia...nitamalizia maisha yangu kijijini...nikafuge na kulima vibustani
Si unajua msaidizi ni muhimu
 
Kijijini kutamu sana Mimi Kila mapumziko lazima niende kijijini na familia kama hakuna jam asee. Na Nina shamba mahala nitajenga tu uzee wangu nirudi hukoo
 
Back
Top Bottom