Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Basi kijijini kwenyewe iwe Mikoa ya Pwani,Lindi ama Mtwara.. watu hawalimi kazi kushinda kwenye bao tu.. unga wa sembe mpaka utoke Dar.. kila kitu kitoke mjini, kazi wanayoithaamini ni kurogana tu.. maisha ya vijijini mazuri yapo Usukumani unaamka asubuhi unakumbana na viazi unashushia na maziwa .. kufumba na kufumbua unaibukia kwenye (Ng'homele) nyama zilizokaushwa, hujagusa (Mashishanga) jibini huko ni full kujiachia utakumbuje Dar ya chai na slace mbili !?
Wengi tukishafika mjini, tunakuwa kama tumepumbazwa akili, tunakuwa hatufikirii mazingira mengine ya kuishi yenye utulivu.
 
Nimeamua nikazeekee kijijini kwa sababu zifuatazo:-​
  • Kule kijijini nitapata hewa safi isiyokuwa na mchafuko​
  • Kule kijijini nitapata majirani wema wasiokuwa na choyo​
  • Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana bila chuki​
  • Kule kijijini tutakuwa tunakunywa togwa pamoja​
  • Kule kijijini tutapunguza msongo wa mawazo​
  • Kule kijijini tutaingia shamba lolote kuchuma matunda na kula​
  • Kule kijijini tutakuwa tunasikia milio ya ndege na viumbe mbali mbali​
  • Kule kijijini tutafurahia uoto wa asili​
  • Kule kijijini tutakuwa tunaenda kuwinda kama sehemu ya michezo​
  • Kule kijijini tutapata marafiki wengi ambao sio wanafiki​
  • Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana panapotokea mmoja wetu anaumwa.​
  • Kukaa kwenye nyumba ya nyasi yenye hewa safi na ya kuvutia​
  • Kula vyakula vilivyopikiwa kwenye vyungu na kuwa na ladha nzuri​
  • Kendwa kuogelea mitoni na kuvua samaki kama sehemu ya michezo na uwindaji​
Kwa ujumla maisha ya kijijini yatakuwa ni mazuri sana

View attachment 3121969

Kwa nyie mnaobaki mjini, nawaachia mpambane na:-​
  • Majungu na fitina zenu​
  • Mchafuko wa hali ya hewa​
  • Jua kali​
  • Msongamano wa watu​
  • Makelele ya baa na kumbi za starehe zinazoharibu utulivu wa ubongo​
  • Misongo ya mawazo kutokana na changamoto za kimazingira​
  • Kudharauliwa na vijana​
  • Kununua kila kitu; nyanya, yai ,mchicha n.k​
  • Kutokuwa na marafiki wa kweli​
  • Kila mmoja kumuona mwenzie fursa​
  • Kuzeeka kabla ya umri wako​
  • Kupata magonjwa ya moyo na presha n.k​
  • Kula vyakula vyenye kemikali katika kukuzia au usindikaji​
View attachment 3121971

Fanya maamuzi mapema; njoo kijijini tukawinde kanga pori, sungura, n.k pamoja na kuongeza miaka mingi ya kuishi.
Usitufokee sasa jomba , we nenda tu .
Wasalimie huko Ileje
 
Tobaaaaa!!! kuna watu wanaenda kuumia huko🤕🤕
Haumii mtu, haya ndio yatakuwa makazi yangu 😀
wr.jpg
 
Back
Top Bottom