Narudia tena akili ya mbantu haiwezi kufanya biashara. Graphic designer kadengua kazi ya zaidi ya laki 5 then baadae anaitaka tena

Narudia tena akili ya mbantu haiwezi kufanya biashara. Graphic designer kadengua kazi ya zaidi ya laki 5 then baadae anaitaka tena

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Sista angu alikuwa na project yake anatakiwa kuisubmit mahali. Hiyo project ilikuwa na picha kama mia na ushee hivi ambazo yeye aliona zinafaa kufanyiwa graphics zote.

Bajeti ya sista kwa picha ni sh. Elfu 5 kwa kila picha.

Mimi huyo nikaenda mpaka kwa ofisi ya brother mmoja anafanyaga graphics.

Kwanza jamaa akasema anataka elfu 20 kwa kila picha, nikamchekecha akakubali elfu tano kwa kila picha ambayo ningempa yote kwa pamoja. Ningempa laki 2 na nusu and then baada ya kumaliza kazi ningempa laki 2 na nusu inayo baki.

Jamaa akasema powa. Nikampa picha moja atengeneze kama sample ya kumpelekea sista na nikampa sh elfu kumi kazi hiyo. Akafanya kazi nzuri sana. Nikampelekea sista akaipenda sana. Nikamrudishia jamaa majibu kwamba sista ameikubali sana kazi so kesho yake ningempelekea hizo picha nyingine na hela. Akasema powa.

Duh asubuhi nakutana na meseji " kaka duh naona tufanye hiyo kazi kwa elfu kumi kwa kila picha, elfu 5 itakuwa haina maslahi kwangu"

Hapo hapo nikamjibu " Poa hakuna noma kaka wacha niangalie utaratibu mwingine "

Nikamuita sista nikamwambia huyu jamaa mzinguaji. Nikamuuliza kazi yako inahusu nini? Aliponionyesha kazi yenyewe na kunifafanulia inahusu nini nikaona kumbe ilikuwa haina hata haja ya kuzifanyia graphics picha zote. Picha moja tu ilitosha sana . Hizi nyingine zote wala hata hazikuwa na umuhimu wa kufanyia graphics zaidi ya urembo tu.

Sista tayari kasubmitt kazi yake na imepokelewa vizuri sana.

Mchana wa siku hiyo jamaa ananitext " kama vipi kaka leta tu hiyo kazi tuifanye hivyo hivyo" nikamjibu tayari sista ameisha I submit na ameondoka.

Siku hizi graphic designers wapo kibao wengine wanafanya graphics kwa buku buku kila picha. Kuna apps kibao za kufanya graphics. Nimekupa kazi angalau ofisi yako iingize hela usije fukuzwa kodi halafu unaleta mambo ya ukhanithi.

Unafanya biashara kama machinga wa miaka ya 90 ana uza nguo sh elfu kumi wewe anamwambia elfu 5 anashusha mwisho elfu 8 anakwambia kama huna elfu 8 hupati nguo unamwambia sawa halafu ile ukianza kuondoka tu anakuita anakwambia basi leta hela yako.
 
Hii inaonyesha watu wengi hawaijui thamani yao.Na sio hata suala la mapatano ya bei.

Hata mimi wakati naanza kufanya side gigs ilikua inanipa tabu sana, nakwenda kwa muhindi namsafishia data, namchambulia data za mauzo na visualize na kutengeneza summary na kuandaa report, nabackup data then ikija malipo nashindwa kumwambia exactly amount ambayo naworth(nachomdai), nilikua naona atadhani nyingi.

Inachukua muda kumasta hiyo kitu.
 
Tz Graphics designers wakali wanahesabika sana... wengi ni wanagusagusa tu..

Nikitulia nitapandisha baadhi ya project
 
Hii inaonyesha watu wengi hawaijui thamani yao.Na sio hata suala la mapatano ya bei.
Hata mimi wakati naanza kufanya side gigs ilikua inanipa tabu sana, nakwenda kwa muhindi namsafishia data, namchambulia data za mauzo na visualize na kutengeneza summary na kuandaa report, nabackup data then ikija malipo nashindwa kumwambia exactly amount ambayo naworth(nachomdai), nilikua naona atadhani nyingi.

Inachukua muda kumasta hiyo kitu.
Dah kwel kabisa mkuu, hii inanikutaga nikiwa nafanya kazi za watu za upigaji picha nashindwa kumwambia nahitaji kiasi fulani.
 
Back
Top Bottom