Narudia tena, Mafundi gereji msipojiongeza mtaishia kutengeneza gari za mwaka 90

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Tatizo la mafundi kukubali ukweli ni mgumu sana. Halafu wanapata pesa kwa kukadilra ndio maana wamelizika.

Mifumo ya magari sasa imebadilika ndio maana Nissan zinawashinda na kuishia kusema kimeo kumbe nyie ni vimeo.

Suala la vifaa ndio kabisa yani namkuta fundi anatumia nyundo kuondoa kitu kwenye matairi mpaka unachoka.

Magari yanayotoka yanatumia electronic na umeme mwingi sana kuliko mlivozoea gari zenu 90.

Kila siku mnaunguza magari ya watu.
 
Mafundi gereji wa chocho wataendelea kupiga hela na kuharibu hizo nissan na pikipiki za boxer 150. Ni watanzania wachache wenye uwezo wa kupeleka magari yao kwenye gereji za professional maana bill zinazotoka huko siyo za kitoto.
 
Kuna Nissan Dualis ya teacher mmoja hivi alikopa ndo akanunua, ilienda kufia gereji ... Gari ilikuwa na shida ya usukani kumbe ilihitajika matengenenezo madogo tu pamoja na kuweka fluid, fundi kafumua usukani wote, mfumo wote wa umeme ukapiga shoti...
Teacher hakuongea kitu alinyooka moja kwa moja polisi... Sikujua kiliendelea nn
 
Kuna gari niliona inapigwa nyundo hadi tread zikafa zote

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna fundi pancha aliniharibia rim ya gari ikabd niweke tube tu baadae ninunue ring nyngne. Yan alilipga nyundo sema nlikoma kuanzia siku hiyo nikawa nikitaka badili taili au ina pancha naenda sehemu yenye machine ya kuvua rim tairi
 
Umesema kweli hawa watu wa afya wanacheza sana na afya zetu sijui huwa wanashindwa soma vpmo. Ndio maaja watu wanaambiwa magonjwa wasiokuwa nao
 
Mafundi wengi badala ya kutibu tatizo wao wanaongeza tatizo
 
Umemaliza kila kitu, watanzania kwa ujumla wetu ni hakuna kitu, ufanisi ni mdogo sana. Walimu, madaktari, mainjinia nk.
 
Sasa police wamsaidie nini,kwani hio gari hapo garage ilijileta
 
Utawalaumu tu mafundi ila kiukweli Tanzania hatujawahi kua serious kwa kitu chochote,,angalia juzi Waziri mkuu anamuuliza jamaa kwanini amechoma nyaraka za Serikali just imagine, wote mashahidi Waziri wa fedha anaulizwa kuhusu fedha za tozo anajibu trab na truck utasema tupo serious hapo....
 
Garage za maana zipo, na mafundi wapo, tatizo ni watanzania wenyewe.
 
Nimependa analysis yako, umesema vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…