Narudia tena, Mafundi gereji msipojiongeza mtaishia kutengeneza gari za mwaka 90

Narudia tena, Mafundi gereji msipojiongeza mtaishia kutengeneza gari za mwaka 90

Tatizo la mafundi kukubali ukweli ni mgumu sana. alafu wanapata pesa kwa kukadilia ndio maana wamelizika.

Mifumo ya magari sasa imebadilika ndio maana Nissan zinawashinda na kundandia kusema kimeo kumbe nyie ni vimeo.

Swala la vifaa ndio kabisa yani na mkuta fundi anatumia nyundo kuondoa kitu kwenye matairi mpaka unachoka.

Magari yanayo toka yanatumia electronic na umeme mwingi sana kuliko mlivozoea gari zenu 90.

Kila siku mnaunguza magari ya watu.
Gari za kisasa, peleka kwa wakala wanaoshughulikia Aina ya gari yako. Ni kweli muda na ugunduzi mpya na wa kisasa unawapita mafundi magari wetu, na wenye uwezo wakizidi kununua magari ya kisasa, si ajabu mafundi wetu wakakosa kazi.
 
Siyo mafundi tu; binafsi hapa Tanzania naona Kada zote hufanya kazi zao kwa kubahatisha..

Hata hawa Madaktari wetu, wengi wanabahatisha kwenye kutibu wagonjwa..

Wanasiasa ndiyo usiseme, na Uchawi wanatumia ili kufanikisha siasa zao Uchwara..

Tanzania ni maeneo machache sana wanazingatia Professionalism kwa asilimia 100%..

Nadiriki kusema Ikulu yetu pamoja na Wizara na Ofisi zote za Umma ndiyo Vinara wa kufanya mambo Kikanjanja kanjanja..
Ni ukweli na uhalisia mtupu! Nchi nzima ina mifumo iliyopitwa na wakati na bahati mbaya, tunazidi kurudi nyuma!
 
Kuna Nissan Dualis ya teacher mmoja hivi alikopa ndo akanunua, ilienda kufia gereji ... Gari ilikuwa na shida ya usukani kumbe ilihitajika matengenenezo madogo tu pamoja na kuweka fluid, fundi kafumua usukani wote, mfumo wote wa umeme ukapiga shoti...
Teacher hakuongea kitu alinyooka moja kwa moja polisi... Sikujua kiliendelea nn
Police kwanza watavuta mkwanja ili mambo yaende, pili huyo fundi hata laki mbili hana [emoji23] [emoji23]
 
Mafundi aina zote ni makanjanja na wengi wajinga wasiotaka kujiongeza maisha yao yote
Unakuta mechanics ana garage miaka 30 ila spanner ni zile zile ufundi ule ule na wizi kwenda mbele kwa baadhi

Yaani hawataki kujiongeza hata kuwa na vifaa vya maana
Garage inatakiwa iwe na kila kitu na kuenda na wakati

Wengine ni wajenzi nao hivyo hivyo mjenzi hana hata gari la kubebea vifaa vyake na hata akihitaji kitu
Hawa nao ni masikini tu wasiotaka kujiendeleza

Tatizo wana ujuzi ila hawataki kujipeleka mbele
Utasikia ooh hela hakuna, miaka 30 unasema hela hakuna

Yaani wote hali moja ni njaa tu na wizi na uongo ndio linawafanya wengi wasiendelee na ukiwaambia wanakushangaa
 
Utawalaumu tu mafundi ila kiukweli Tanzania hatujawahi kua serious kwa kitu chochote,,angalia juzi Waziri mkuu anamuuliza jamaa kwanini amechoma nyaraka za Serikali just imagine, wote mashahidi Waziri wa fedha anaulizwa kuhusu fedha za tozo anajibu trab na truck utasema tupo serious hapo....
Nadhani anapenda publicity kuna issues yeye angetakiwa tuu kutoa directives kimya kimya na mtu anapandishwa kizimbani...
 
Siyo mafundi tu; binafsi hapa Tanzania naona Kada zote hufanya kazi zao kwa kubahatisha..

Hata hawa Madaktari wetu, wengi wanabahatisha kwenye kutibu wagonjwa..

Wanasiasa ndiyo usiseme, na Uchawi wanatumia ili kufanikisha siasa zao Uchwara..

Tanzania ni maeneo machache sana wanazingatia Professionalism kwa asilimia 100%..

Nadiriki kusema Ikulu yetu pamoja na Wizara na Ofisi zote za Umma ndiyo Vinara wa kufanya mambo Kikanjanja kanjanja..
Upo sahihi kabisa mkuu
Unakuta mtu ni fundi cherehani anapata tender mpaka za shule kushona sare na wafanyakazi wake wengi ni wa msimu ila sasa jichanganye umpelekee vitambaa akutengenezee utajuta

Hela amekula na utazungushwa mwezi

Ukienda kwa carpenters nao ndio kabisa unauziwa kochi kalijaza maboksi ukilikalia siku Tatu tu umemezwa na kochi

Ukanjanja kila mahali ndio maana hakuna wanaoendelea huku wakisema ooh foreigners wanatajirika kwa ndagu na kuiba na kujuana na wakubwa

Mtu anafeli maisha hajui anafeli wapi halafu kutwa kwa mganga
Inatakiwa shule wafundishwe sana maisha badala ya kukaririshwa tu

Ndio maana hata viongozi unakutwa vichwa boga
 
Utawalaumu tu mafundi ila kiukweli Tanzania hatujawahi kua serious kwa kitu chochote,,angalia juzi Waziri mkuu anamuuliza jamaa kwanini amechoma nyaraka za Serikali just imagine, wote mashahidi Waziri wa fedha anaulizwa kuhusu fedha za tozo anajibu trab na truck utasema tupo serious hapo....
Tupo serious na comedy, udaku na kucheka watu wanaokosea....
 
Kuna Nissan Dualis ya teacher mmoja hivi alikopa ndo akanunua, ilienda kufia gereji ... Gari ilikuwa na shida ya usukani kumbe ilihitajika matengenenezo madogo tu pamoja na kuweka fluid, fundi kafumua usukani wote, mfumo wote wa umeme ukapiga shoti...
Teacher hakuongea kitu alinyooka moja kwa moja polisi... Sikujua kiliendelea nn
Mfumo wa umeme ukipiga short means sensors zote nazo zimepiga short
 
Back
Top Bottom