Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Acha na hilo la kupanda daladala..mimi hawa watu wanaopanda daladala halafu wamevaa suti tena wamepanda daladala za mbagala k.koo huwa siwaelewi kabisa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Time kunangwa, na Matajiri washamba, waliokulia umaskini.!
 
Ushamba ndio uko hivyo.
Kutumia kitu ni preferences za mtu tu.
Kama wewe hapo unatumia simu ya 2014. Eti kisa tu sio Infinix. Wakati kuna infinix zenye bei kuzidi simu ako. .bora hata ungekuwa na s au note series ya Samsung ndio uwezo kunanga. Ishi kwa budget yako. Tangu uanze kuuchukia umasikini, umekuachia kweli..!
 
Mafuta ya elfu 50 yanatosha wiki mzima, sasa ukimwona mtu mpaka anapaki gari nyumbani kwasababu ya mafuta kukata huyo bado maskini
Hii ndio Jamii forum mkuu,kwa hiyo kwa kipasso chako cha million 2 unusu tena used ndio kimekupa kiburi kuja kutukana watu hapa jukwaani.

Kwa mantiki hiyo ya mafuta ya 50 elfu per week maana yake wewe ni mwalimu ni kwenda kazini na kurudi nyumbani kulala huna mitikasi yoyote wala ratiba za bata weekend.

Acha zarau za kishamba bwana mdogo maisha ni zaidi ya kupanda dala dala mji mzito huu.
 
Kwa taarifa yako huo ndio usafiri wa mjini kwa majiji yote duniani(Public transport)
Mabasi ya umma na Treni ndio hasa nyenzo ya kukuwahisha kwenye mishe zako hilo ni dunia nzima iko hivyo na usikae ukafikiria kutumia gari binafsi ndio utajiri,wote wapandao dala dala si eti kua hawana magari
Tatizo la wabongo wengi ni Hakuna Exposure wengi hawajatoka nchihii hata ke ya tu hapo mtuhajatia mguu wala passport huna!tembea ujionee!
 
Wapo maskini wengi wenye magari binafsi na matajiri wanaopanda daladala
 
Eti kuna watu wanasema kuwa matajiri nao hupanda daladala ili wapate fikra tofauti. Kwani kwenye daladala kuna kupiga story?
Tajiri hapotezi muda kuongea na maskini . Ikitokea anaongea na maskini ujue yuko kwenye site zake au kwenye biashara zake. Lakini hawezi kupangwa kama mishikaki kirahisi.
 
Nadhani hujanielewa na umekurupuka kujibu.
Kwenye tittle nimeweka neno Daladala Dar es salaam.
Achana na miji ya wenye akili na uchumi wa kati na wa juu ulio halisi.
Wewe unaona ni sawa tu yale manyanyaso ya Makonda wa daladala hapa mjini?
Kupangwa kwenye mistari kamabahesabiwa rokoo jeshini sawa tu?
Usimame huku umebanwa Mbagara - Posta sawa tu?
 
Kwenye daladala kuna root nzuri aiaeee unakaa kwenye daladala unatamani usishuke haraka.Ila ukisimama ukabananishwa dah safari inakuwa ngumu.Ila kwenye mwendokasi hata ukisimama poa tu
 
Dar es Salaam Bora watu waendelee kuwa na kipato cha chini.Dar watu wengi wakiwa na kipato cha Kati au juu,mji utazidiwa kwa magari
 
Dawa kuwe na mabasi ya aina mbili. Kajambanani ambayo nauli ni 400 na Classic ambayo nauli ni buku ila mnakaa level seat.
Yapo asubuhi na jioni Kuna Coaster za Mbezi-Kariakoo, Airport-Posta kwa 1000 na Nyingine ni level seat.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…