Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Naunga Mkono Hoja! NAKAZIA kupanda Daladala ni Umasikini na hakuna anaye enjoy kupanda Daladala, tunapanda ili tufike tu! Haiwezekani eti Diamond apaki Rolls Royce aone usumbufu halafu apande Daladala [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]wote mnaompinga mtoa mada ni Masikini.

Nauchukia Umasikini

Nauchukia Umasikini

Nauchukia Umasikini

Hata kutumia Tecno au Infinix Pia ni Umasikini.. Goodnight EVERI BADI

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
Dah we jamaa umeniua sana, so mkuu yaan Infinix na techno ni sawa??
 
Baadh ya watu licha ya kumilik magar mazur tu ya kutembelea wanaamua kupanda daladala walau kupata fikra tofaut,baadh ya watu wanafany kazi za aina moja kila siku watu anaokutana nao ni walewale nyaraka zilezile na akitoka kazin anapanda gar la peke yake mpaka nyumban inamaana ili apate fikra mpya analazimika kujichanganya maeneo km hayo walau achangie mijadala ambayo itamfanya apate fikra mpya
 
Habari wanajukwaa!

Natumaini hamjambo,

Hii sio kashfa bali ni ukweli mtupu.

Usafiri wa daladala hapa Dar ni kwaajili ya maskini.

Vijana tutafute pesa huku tukimwomba Mungu atuepushe na Usafiri huu uliojaa karaha na kadhia.

Haiwekani mtu una pesa zako usimame Kariakoo mpaka Mbagala, au usimame Kariakoo mpaka Tegeta.

Jioni ukitoka mjini kwenda pembezoni mwa jiji unavizia basi la kugeuka nalo ili upate siti, nako ukishangaa hupati.

Makonda jioni wanaringa kama wasichana mabikira.

Watu wananuka sigara mnapumuliana.

Mwendokasi nako niliwahi kupanda jioni nako hali ni ngumu. Kuna mfanyakazi mwenzangu alikatwa kidole na mlango wa mwendokasi asubuhi wakati anakuja kazini.
Hii picha chini haina uhusiano na mada bali iko hapo kuchangamsha mada.
Ni mimi mwanadaladala mwenzenu.
View attachment 1860695

giphy.gif

Hakuna jipya zaidi ya kutofautiana masaa ya ya kufika nyumbani.
 
Siyo kwa maskini, ni kwa ajili ya watu wanaohitaji kutumia usafiri wa daladala kwa wakati husika. Mfano wengine wana magari yao lakini wakati mwingine hutumia daladala kuepuka usumbufu wa kuendesha, maana kuendesha gari siyo rahisi kama mtoa mada unavyofikiria au kama wanapiga bajeti ya mafuta.

Mimi nina gari na sikuelewi unaongea nini ndugu,I can’t relate mbona unatusemea wenye magari na sio kweli,ebu tulio na magari mniunge mkono
 
Mimi nina gari na sikuelewi unaongea nini ndugu,I can’t relate mbona unatusemea wenye magari na sio kweli,ebu tulio na magari mniunge mkono
Kwani namna ya matumizi ya gari ipo sawa kwa kila mtu, au unafikiri nilivyoandika hapa sina gari......mimi gari langu kama halina mafuta nitapanda daladala, hilo nalo ni la kuficha? na naweza kuamua tu kwenda kupanda daladala hata kama gari lipo full tank......tatizo mkiwa na vipasso mnafikiri maisha mmeyapatia sana mnaanza kudharau watu kisa wanapanda daladala..
 
Ungetafsiri maana ya umasikini ili niweze kuchangia mada kwa umakini.
 
Mimi SAnNLG yangu naiwekeaga mafuta ya 20,000 natumia mwezi mzima na nikiweka miezi minne mfululizo huwa tanki linajaa.

naishi mji mdogo ambao kutumia Pkpk ni salama na umbali toka home to job ni km2 tu.

sijawahi kujuta kumiliki chopa kama ninavyoiita Mimi.
 
Ili mradi uwe usafiri, unamtoa point A hadi B. Ukiwa na dharau kwa vitu vidogo, hata vikubwa unapata shida sana kuvipata. Jifunze!!
Mkuu una passo nini? ukikutana na tambo za kidukulilo mbona utazima, anakwambia Toyota na Nissan kwake siyo gari......ni vitu vinavyosogea kwenda mbele...
 
Hapo si ajabu mtoa mada katoka kula ugali wa kulumangia na dagaa mchele, sasa hivi yuko zake kitandani mkonononi na smatfon yake iliyopasuka kioo huku mkono mwingine ukifanya kazi ya kufukuza mbu
Daaah! 🤣🤣🤣
 
Kwenye eicher za tegeta nyuki to kivukoni asubuhi mnapangwa kama ndizi. Unashika bomba la kulia unakuta mama mwenye umri wa mama yako anakugeuzia tako naye kashika bomba la kushoto. Konda anapenya hapo hapo kuchukua nauli... Hakika huu usafiri ni wa kudhalilisha basi tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapo Bado hujakutana na madunga dunga wazee wa chaji
 
Kuna mtu anamiliki nyumba nne mjini lakini anatumia usafiri wa daladala, huyo tumweke kundi gani?

Kwa sasa hapa dar gari sio luxury need ni basic need,inategemea na aina ya mizunguko mtu ulio nayo pia
Huyu mwenye nyumba nne amefanya jambo zuri
Ajichange sasa achukue passo yake kwa ajili ya kumrahisishia mambo[emoji1376]
 
Sijawahi kufuatilia kujua rank ya umaskini kwa Tanzania unaanzia mtu awe/apate bei gani kwa siku au amiliki nini ili kumtofautisha na wale hohehae!

Mf;wapo watu a'cally kutokana na mazingira waliyoishi/kulia yaliwafanya kuwa tu social,uwezo wa kuhudumia gari wanao even kumiliki hizi baby walker zaidi ya moja wanao ila haiingii akilini eti mtu ujibane ili ununue gari kwa kuogopa kupanda daladala,maisha ni yako ninyi mnaoona aibu kupanda daladala mnaogopa macho ya watu hamjui kwamba mumiliki gari au musimiliki gari hamuwapunguzii wala kuwaongezea chochote wale mnaohisi wanawatazama.

Mimi nina Bajaj tatu mpya zinazunguka barabarani ila ukinikuta kwenye Mwendokasi kama siyo mimi vile yote ni kwa sababu naishi maisha yangu Tanzania hii ukiogopa ogopa vitu vidogo vidogo kama kupanda public buses kuna baadhi ya vitu vitaku-cost.

Kuishi maisha yako ni raha sana
Hukimbizani na mtu
Sitaki kusema kutumia public transport ni umaskini ila usafiri ni muhimu sana hapa jijini
Binafsi siwezi kupanda mwendo kasi ile kero ya kupambania ndio kitu kinanishinda
Daladala napanda vizuri route ambazo hazina vurugu
Mfano route ya ninapokaa mpaka ofisini ni route isiyo na karaha kabisa na ni dakika 10 tu
Hivyo huwa napanda sana dalala
Lakini usafiri binafsi ni kitu muhimu dar Kuna sehemu ni kero kupanda daladala
 
Back
Top Bottom