Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Hivi mkuu kumiliki gari la 4 millions ndy Tajiri?

Bado tuna safari ndefu sana ya kujitambuwa.
 
Ukweli mchungu,daladala ni usafiri wa kifukara sana,na watu wanakuwa na hasira,msongo balaaa,ukimgusa mtu na begi,anaweza akakuporomoshea matusi hatari!
 
Nyumba nne za aina gani, ziko wapi, alijengaje?
Maana job kuna jamaa ana nyumba mbili hapa mjini ila kazini anakuja na baiskeli na manguo ya mtumba.
Kuna mtu anamiliki nyumba nne mjini lakini anatumia usafiri wa daladala, huyo tumweke kundi gani?
 
Teh kwa ninavyowajua wabongo watakuwa radhi wapande ya mia nne hayo ya buku yatakuwa yanazunguka matupu tu
Uko sahihi.
Siku moja wakati tuko M/complex tunasubiri daladala za Chanika akapita mjamaa na private car ile gari ina sehemu ya mizigo na sehemu ya watu (pick up).
Sasa akasema Gongolamboto 500 nyuma sehemu ya mizigo na kwenye siti 1000. Watu walijazana kwenye body nyuma huku siti zikikosa watu . Nilishangaa sana.
 
Point ya msingi sio kuogopa macho ya watu, ishu ni zile adha zinazopatikana kwenye usafiri wa daladala...zile habar za kushikilia bomba gari imeshona had mlangoni halafu mnakaa kwenye folen nusu saa nzima, kupambana mlangoni uwahi siti, au ukikaa ile siti ya katikati mtu anakuja na begi au mfuko wake anaushikilia hapo hapo karibia na kichwa chako...kuna baadhi ya maeneo ukiishi unawaza hata kuvaa baadhi ya nguo kwa sababu itarud haitamaniki,plus kupangwa kama nyanya na makonda na walivyo na mdomo mchafu ukizingua kidogo mnaharibiana siku ,..ni obvious ukiwa na uwezo mzur utawaza alternative ways za usafiri mjini ..iwe ni kutumia gari yako ,au ubber ili kuepuka habar za kupangana kwenye folen ndeefu pale gerezan kwenye mwendo kasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…