Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
NARUDIA; VIJANA MAISHA NI POLEPOLE, HUO NDIO MWENDO. USIYASUBIRI. YAFUATE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Haba na haba hujaza kibaba. Bandua bandua humanize gogo.
Hizo ni hekima za wahenga, manabii wa kale. Polepole ndio mwendo.
Kijana nisikie, ndoto kubwa uliyonayo ni kama gogo la mbuyu. Huwezi itimiza ndoto hiyo kwa usiku mmoja. Huwezi angusha mbuyu kwa shaka moja. Bandu bandu humaliza gogo.
Imege hiyo ndoto yako kidogo kidogo ndani ya muda ushangaa mbuyu umeanguka.
Kamwe usiyasubirie maisha.
Unakuta kijana anakuambia mimi sitaki kuwa na familia kwa sababu bado mambo hayajakaa vizuri.
Mimi sitaki kujenga kwanza kipato change kidogo.
Hapana! Mambo hayaendi hivyo.
Maisha hayasubiriwi. Maisha ni mjongeo. Movements. Usikubali kukaa sehemu moja. Usikubali kusubiri.
Hata mwingine anakuambia mimi nitafurahia siku fulani. Au mpaka nifikishe milioni kadhaa au nijenge nyumba. Au nifike degree. Au mpaka ninunue gari.
Wengine hata kufurahia na Wake/waume na wake zao wanakuambia bado mpaka siku fulani. Nope! Mambo hayaendi hivyo.
Sisi Watibeli kila siku inayoenda kwa Mungu tunafurahia tuu. Yaani maisha ni kufurahia tuu hiyo ndio mission yetu kuu. Iwe tupo kwenye wakati mzuri au mgumu katika maisha.
Maisha ni Polepole. Maisha ni hatua. Ili uweze kuyafurahia lazima ujue hili.
Usisubiri hela ijaye. Rahisisha maisha yako kwa kuondoa kwanza vitu vidogovidogo.
Anza na mahitaji yako madogomadogo ya msingi. Furahia.
Usisubiri upate au upewe kazi. Jipe kazi. Anza na ulichonacho Bro au sister.
Siongei kama mtu tajiri. Ila naongea kama kijana niliyefanikiwa. Watu wengi hasa wenye uelewa finyu kuhusu maisha hufikiri utajiri pekee ndio mafanikio jambo ambalo sio sahihi.
Nimefanikiwa kwa sababu ninajua maisha yanataka nini. Yanataka kiumbe a-move, ajishughulishe, afanye Movements.
Niliwahi kusema niliuza dagaa wa mwanza na mpaka sasa nauza. Kwa kutembea. Kwa mtaji wa elfu hamsini. Niliwahi kusema nilikuwa nashona wakati nipo chuo. Kupitia boom. Na mpaka sasa nashona. Hayo usiyahesabu kama matambo. Najaribu kueleza kwamba lazima uanze kwa kidogo ulicho nacho.
Usiwe na kiburi. Usijione kwamba wewe ni mzuri sana, au unaakili sana. Au umesoma sana. Au vyovyote vile. Usiwe na kiburi.
Ajikwezaye atashushwa.
Alafu kufanya kazi hata kama ya mtaji mdogo sio jambo la aibu. Kuanza ukiwa chini sio aibu. Ni mtazamo wako potofu aiseeh!.
Unajichelewesha Aiseeh! Wote unaowaonea aibu hawana habari na wewe. Hutaishi nao miaka yote. Watahama au utahama hapo. Then what? Watakufa au utakufa. Then what?
Yaani Mtibeli nishindwe kuuza dagaa kisa nina degree sijui ya nini na ya chuo gani?
Yaani niche kufanya jambo fulani kisa ati ni maarufu mshenzi huko mitandaoni?😄😀 thubutu. Watibeli hatuko hivyo.
Vijana ninyi ni Watibeli. Msione haya kwenye jambo la haki. Usione haya kwenye jambo la kweli. Ni kweli wewe bado uko chini. Kubali na Furahia ukweli huo.
Sio tatizo. Sio dhambi. Sio vibaya. Na zaidi ni heshima.
Na nakuhakikishia heshima inakawaida ya kukuinua. Hautabaki vile ulivyo.
Najua concern kubwa ya vijana ni watu watawaonaje, marafiki au mademu au vijana wakuwaoa watawaonaje.
Aiseeh! Ukitaka upate mademu wakali, wanaojitambua, mtaofanya maisha basi usiwe nq aibu katika kufanya kazi kuanzia pale ulipo.
Siongei kukupa moyo. Naongea kwa uzoefu. Kwani nami nimepitia huko.
Leo unakula mlo mmoja. Kesho utakula miwili na utakula kusaza kama hutokuwa na aibu za ajabu ajabu. Kama utajua maisha ni hatua. Kama utajua mbuyu ulianza kama McMichael.
Kama utajua bandu bandu humaliza gogo. Kama utajua mali bila daftari huisha bila habari. Kama utajua mchumia Juani hulia kivulini. Kama utajua penye nia pananjia.
Kama utajua subira ya vita kheri.
Kama utajua mvumilivu hula mbivu. Kama utajua haba na haba hujaza kibaba na polepole ndio mwendo.
Sisi watunzi tunapotunga kazi zetu tunasuka visa kwa kuvifungua polepole. Huku tukiweka mafumbo na kuyafumbua polepole. Zipo sehemu tunaweka plot twist kwa lengo la kuleta mtikisiko na kuihamisha akili ya msomaji. Ndivyo hivyohivyo katika maisha ya mtu.
Polepole!
Fanya kazi!
Kuwa na malengo!
Jifunze sana.
Kuwa mwaminifu na heshimu watu.
Linda mipaka yako.
Heshimu pesa unayoipata.
Jali Afya yako.
Usimsahau Mungu.
Jitoe kwa taifa lako. Hakikisha kuna jambo unalifanya bure kwaajili ya jamii na taifa lako.
Usikubali kuishi kwa kusubiri. Kama jambo linahitaji kusubiri angalia katika jambo hilo ni eneo gani unaweza kuwa una move.
Mfano, unandoto ya kununua gari au nyumba. Lakini kwa sasa hauna hela. Hivyo itakupasa usubiri.
Hutakiwi usubiri kabisa kabisa. Unaendelea kufuatilia kwenye mitandao ya kijamii, blogs, websites unaenda kwenye yard za magari kufuatilia na kujifunza magari hata kama hauna.
Unajifunza kuhusu magari hasa lile unalotaka kulinunua. Unajifunza sheria za barabarani na udereva.
Ilimradi usisubiri.
Vivyohivyo kwenye mambo ya ujenzi wa nyumba. Vivyo hivyo kwenye biashara.
Kadiri unaposogea ndivyo ndoto yako inavyozidi kuwa karibu.
Akili na mawazo huvuta uhalisia. Matendo na maneno yako hufanya uhalisia kuwa kweli.
Mimi nimemaliza.
Mungu aliyekuumba akuongoze.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam