Narudia; Vijana maisha ni Polepole, huo ndio Mwendo. Usiyasubiri. Yafuate

Kwa hiyo mtoto asome shule za hovyo tu , au ule vyakula vya hovyo tu , kisa uanzishe familia bila kuwa na uchumi wa kueleweka?
 
Kwa hiyo mtoto asome shule za hovyo tu , au ule vyakula vya hovyo tu , kisa uanzishe familia bila kuwa na uchumi wa kueleweka?

Shule za hovyo ziko huko mijini mlikojazana kama nzi kwenye Mavi.
Mimi nimesoma Makanya huko Same, miaka ya 1999 na sijawahi kukaa chini. Secondary sijakaa chini.
Shule sio nzuri sana lakini sio mbaya pia.

Hiyo ya kusema shule za hovyo ni propaganda tuu za wamiliki wa shule binafsi.
Niliwahi kufundisha shule mbili za Private. Moja ipo Dsm, nyingine ipo Morogoro mjini.
Hakuna la maana mule na watoto Ada ilikuwa milioni 2.
Kwanza hawali vizuri, hakuna vitabu, hakuna uongozi wa kueleweka.
Yaani chakula na sehemu wanayolala watoto utabaki mdomo wazi.
Kuna siku nilianzisha uzi humu kuhusu jambo hilo nilipolikumbuka.

Hivi wazazi wakipeleka watoto shule hizi za private wanakaguaga mabweni? Wanauliza watoto wao kuhusu msosi?
Alafu uwakute waalimu na uongozi wa shule unavyojibu utacheka use. Ati mtoto hajaja shule kula au kulalq. Kaja kusoma.
Wakati mtu katoa milioni 2. Hiyo hela ni miaka 10 iliyopita Bwashee!

Kuhusu Kula.
Kwa nini ule vibaya?
Niliwahi kuandika hapa pia kuhusu bajeti ya watu watano kwa 300k kwenye ishu ya chakula mtu anakula vizuri sana. Akinunuq vyakula vya jumlajumla.
 
Kipato changu ni 500K natoboaje mkuu

Hiyo hela ni ninyi sana. Kama uko smart.

Kama utaanzisha mahusiano. Mwenza wako kipato chake kisipungue 300k

Weka kila mwezi 100k Kama akiba kisha zikifika 1M anzisha mradi. Kama ni saluni ya kiume ya 1M inatosha kuanzia. Tafuta kijana muwekw kila siku akupe 7. Kama upo DSM.

Au fungua ofisi ya kushona, nunua machine Tatu. Lipia kodi. Tafuta mafundi. Weka Kamera. Chukua hela
 
Ahsante sana kaka japo kutunza 1M kwa miezi 10 ni kazi
 
Vijana wajipange asee, maisha sio lelemama hauna hela ya maana bora ujipange kwanza kuliko kuja kuleta familia na kuitesa tu
 
Ahsante sana kaka japo kutunza 1M kwa miezi 10 ni kazi

Sio kazi.
Alafu sifa ya mtu anayeweza kutoboa kiuchumi ipo maeneo matatu tuu. Na maeneo hayo matatu yanaonyesha tabia yake sio akili yake.

1. Kutafuta
2. Kuzitunza.
3. Kuzizalisha.

Kila hatua inategemea hatua iliyomtangulia.
Na circle inaendelea hivyohivyo

Kama unaweza kutafuta 500k
Unashindwaje kutunza 100k kwa mwezi?
 
Vijana wajipange asee, maisha sio lelemama hauna hela ya maana bora ujipange kwanza kuliko kuja kuleta familia na kuitesa tu

Kutesa familia ni mtazamo pia

Mfano, mtu anafikiri mtoto kusomea serikalini ni kuitesa familia. Jambo ambalo sio kweli.
Ni bad education

Mtu anahitaji Chakula, malazi, mavazi. Hizi ni basics.
Mtu yeyote akiweza hizi mambo Tatu kwa kiwango cha kuridhisha anatakiwa aanzishe familia

Sio mpaka awe na magari, majumba, sijui Ada za shule za gharama, hizo ni ziada
 
Hiko kiwango cha kuridhisha ndio hoja yangu ya kujipanga kwanza , watoto wapate elimu sehemu nzuri shule za serikali hamna kitu🚮
 
Hiko kiwango cha kuridhisha ndio hoja yangu ya kujipanga kwanza , watoto wapate elimu sehemu nzuri shule za serikali hamna kitu🚮

Inategemea na shule ya serikali mkuu.

Hizo shule za private zenyewe ujipange haswa. Zilizo nzuri ni gharama sana angalau 3M kuendelea.

Hizi za 3m kurudi chini nyingi magumashi.
Shule yoyote ambazo waalimu wanalipwa chini ya 1M hiyo haiwezi kutoa elimu ya maana. Tena nyingine hazilipi kwa wakati wakati wazazi wanatoa Ada.

Tena usinikasirishe nisije nikaanzisha hiyo mada
 
Ndio maana nikasema watu wajipange hizo za 3m ndio kujipanga kwenyewe, shule za serikali tulisoma sisi ndio na mtoto wako arithi ubovu huo huo hii hapana
 
Ndio maana nikasema watu wajipange hizo za 3m ndio kujipanga kwenyewe, shule za serikali tulisoma sisi ndio na mtoto wako arithi ubovu huo huo hii hapana

Mkuu shule ni zilezile. Mtaala ni uleule. Hakuna maajabu.
Labda private kwa sababu wanaweka vingereza ambavyo mtoto anaweza kujifunzia nyumbani kama wazazi ni wasomi.

Nje ya hapo hakuna ziada.

Kuhusu confidence sijui kujieleza mtoto anaweza kufundishwa nyumbani kama ninyi wazazi mlishasoma.

Wazungu wengi hata degree hawajaenda ila wana ile self awareness waliyofundishwa nyumbani.

Sisi waafrika jukumu la elimu limeachwa kwa waalimu pekee. Na huko shuleni hakuna la maana.

Shule karibu zote Tz zinalenga ufaulu wa Div 1 hakuna masuala ya ujuzi, vipaji sijui ubunifu.

Aiseeh! Mimi mtu hajanishawishi Aiseeh ningekuwa sijasomea mambo ya hiyo sekta ningekukubalia lakini ninachozungumza hapa ninakielewa vizuri sana. Tena sana.

Wewe peleka mtoto akasomea shule ya hata milioni 10 yenye waalimu kama wote. Lakini mtaala huuhuu. Lengo lilelile la kupata division one. Mwingine ampeleke kayumba.
Wakutane pale Udsm.

Then mtaani utaona nani anaenda kufanya vizuri.
Labda wapelekwe sokoni kuuzwa ambapo siku hizi soko la ajira ni gumu
 
Well said Taikon
 

Ni kweli ambiere kinachoboa kwenye shule za serikali ni idadi kubwa ya wanafunzi kwenye chumba kimoja hasa kwa shule za mjini ila kwa sisi tuliosoma mkoani hasi shule za Kilimanjaro mnakaa wanafunzi wawili kwenye dawati au mmoja kabisa hivyo ratio ya mwalimu na mwanafunzi inakuwa sawa.

Lakini bado kama mtu hamudu shule ya private asiache kuanzisha family kisa sababu hiyo.
 
Umesema kweli kabisa. Maisha hayahitaji ukamilike kwanza ndipo uanze; yanahitaji uanze na ulicho nacho, usonge hatua kwa hatua. Polepole si kushindwa, ni mwendo. Haba na haba hujaza kibaba. 🔥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…