NASA yaingia kwenye anga hewa la jua

NASA yaingia kwenye anga hewa la jua

Wao walionaje kama kinakaa kwa mkao huo?

Na kama wameweza kutengeneza picha isiyo halisi kwenye computer tunawezaje kuwa na hakika kama wamefikisha hiko chombo?

Eti mkuu!
Wamarekani sio wa kuamini. Uongo mwingi ili kuwatisha wengine.
Ni kitu gani kinaweza kuvumilia temperature zaidi ya 10000°

Halafu atuambie kwanini vyombo vinashindwa kutua mercury na wanakimbilia kwenye jua!?
 
Mbona kipo mkuu ,kuna chombo kinaitwa mariner 10 spacecraft kishawahi kwenda huko mercury ila hakikuland kwenye mercury kilifanya orbiting tu nakukusanya data. Mpaka sasa kitu ambacho hawajaweza ni kuiland spacecraft katika sayari ya mercury kwa sababu inakuwa ni ngumu sana kuslow its speed ili kiweze kuland safely kwakuwa mercury ipo karibu sana na jua.
 
Wao walionaje kama kinakaa kwa mkao huo?

Na kama wameweza kutengeneza picha isiyo halisi kwenye computer tunawezaje kuwa na hakika kama wamefikisha hiko chombo?

Eti mkuu!
Mbona mkuu kila siku zinarushwa rockets na vyombo mbalimbali huko angani na wala hamna anayeviangalia kwa macho jinsi vinavyosafiri na vyombo vinafika salama kabisa na kufanya kazi ambazo vimetumwa, watu wakishafanya mahesabu yao wanafunga sensors kwenye hicho chombo then wanaprogram computer ili kuweza kuwasaidia kumonitor safari ya vyombo vyao, hizo mission zote za warusi,wachina,wamarekani,wajapan na ulaya wote hao wakishatuma vyombo vyao wanatulia ndani ya jengo maalum wanaangalia safari ya hicho chombo kwenye computer tu so hapo ndio wanaona picha nzima ya hicho chombo kiliivyo bila hata ya kukipiga picha kwa sababu hizo computers zinatoa enoumous amount of data ya hizo spacecraft yani kila kitu inakwambia mfano speed ya chombo,umbali ilipofikia,angle yake ilioweka,temperature,heat friction na vitu vyengine kibao mpka chombo kinafika
 
NASA's PARKER SOLAR PROBE .☀️☀️

✍️Kama utakuwa na kumbukumbu basi bila shaka utakua unakumbuka vyema kipindi tunakijadili chombo cha NASA kiitwacho #Parker_solar_probe ambacho kilirushwa anga za mbali mnamo tar.12 August 2018 kwa ajili ya kwenda kulichunguza #Jua ☀️

✍️Wengi wao humu walidai kuwa hakitoweza kufika kwenye jua na kitaishia kuyeyuka kutokana na joto kali lililopo kwenye jua. Bila kujua kuwa chombo hiko kiliundwa madhubuti kwaajili ya kukabiliana joto la kutisha🌡️🔥

✍️Taarifa kamili ni kwamba chombo cha #Parker_solar_probe hatimae kimefanikiwa kuingia kwenye eneo la jua. Chombo hiko kimeweza kuingia kwenye atmosphere ya jua eneo liitwalo #Corona ambalo ndilo lina joto kali zaidi kuliko hata joto lililopo kwenye uso wa jua. Eneo la corona hufikia hadi nyuzi joto milioni 1, wakati uso wa jua hufikia nyuzi joto 5,500 tu.🌡️

✍️Hivyo chombo cha parker solar probe kimeendelea kuweka record za kibabe ya kuwa chombo chenye kasi kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa na mwanadamu ambapo huweza kwenda kasi ya Kilometer 194 kwa sekunde (194 Km/s) ama Kilometer 700,000 kwa saa ( 700,000 Km/h) 🛰️💨🔥

✍️Na sasa kimeweza kuweka record mpya ya chombo pekee na cha kwanza kilichoweza kukutana na jua uso kwa uso.☀️

✍️ Kumbuka sayari ya #Mercury ndio ilikua kitu pekee kilichopo karibu zaidi na jua kuliko kitu chochote ambapo ilikuwa umbali wa Km milioni 57 kutoka kwenye jua. Lakini #Parker_solar_probe imekuja kuvunja record hyo kwa kulisogelea jua kwa umbali wa Km milioni 8 tu kutoka kwenye jua.💥

✍️ Usikose kutazama kipande cha video iliyorekodiwa na chombo hiko kikiwa kwenye kasi kubwa kulisogelea jua. Video hyo utaipata kwenye link hapo juu 📹📺

By Bob Lee Kizigha
Hafu Afrika tunasema tunaweza kushindana na beberuz, hao jamaa wako mbali miaka 500 ijayo,
 
Inanishangaza San mm hiki kitu wanachofanya Hawa wazungu Ni sawa na kwenda kumchokoza muumba wa vitu hvyo

Alfu unasema. Speed ya chombo Ni km/h 194 kwa second hiyo kitu HAKIWEZEKANI YAANI HATA KWA MACHO AKIONEKANI hpn kwa kweli duh kufumba na kufumbua km 194. Hap na Moro kwa sec
Kwani umeme unasafiri Kwa Km ngapi kwa Sekunde? Au Mwanga?
 
Inanishangaza San mm hiki kitu wanachofanya Hawa wazungu Ni sawa na kwenda kumchokoza muumba wa vitu hvyo

Alfu unasema. Speed ya chombo Ni km/h 194 kwa second hiyo kitu HAKIWEZEKANI YAANI HATA KWA MACHO AKIONEKANI hpn kwa kweli duh kufumba na kufumbua km 194. Hap na Moro kwa sec
Asa mkuu huyo muumba unayemsemea kaumba ulimwengu halafu hajui kama dunia ni duara,kaumba ulimwengu halafu hajui kama dunia ndio inazunguka jua. Anyway wanasayansi huwa wakitaka kufanya yao hawafikirii kabisa hzo habari za muumba na laiti ingekuwa hivyo basi hapa duniani tusingefika hapa tulipo sa hivi, kitu kingine huwa hawaamini kwamba kuna jambo haliwezekani wewe kwa akili yako ya kawaida utaona mambo mengi hayawezekani kufanyika ila wenzako wanayafanya bila ya shida yoyote. Hiyo speed ya hicho chombo inafikiwa kirahisi tu kwa kupata boost ya speed kutoka kwenye gravitational pull ya sayari zilizoko huko pia kutokuwepo kwa air friction
 
Inanishangaza San mm hiki kitu wanachofanya Hawa wazungu Ni sawa na kwenda kumchokoza muumba wa vitu hvyo

Alfu unasema. Speed ya chombo Ni km/h 194 kwa second hiyo kitu HAKIWEZEKANI YAANI HATA KWA MACHO AKIONEKANI hpn kwa kweli duh kufumba na kufumbua km 194. Hap na Moro kwa sec
Usichukulie mazingira ya duniani ukafananisha na ya anga za mbali huko,kwa uelewa wangu mdogo wa physics huko anga za mbali hakuna friction force hivyo inafanya vyombo vinavyosafiri huko kukimbia speed kubwa sana.
 
Mbona mkuu kila siku zinarushwa rockets na vyombo mbalimbali huko angani na wala hamna anayeviangalia kwa macho jinsi vinavyosafiri na vyombo vinafika salama kabisa na kufanya kazi ambazo vimetumwa, watu wakishafanya mahesabu yao wanafunga sensors kwenye hicho chombo then wanaprogram computer ili kuweza kuwasaidia kumonitor safari ya vyombo vyao, hizo mission zote za warusi,wachina,wamarekani,wajapan na ulaya wote hao wakishatuma vyombo vyao wanatulia ndani ya jengo maalum wanaangalia safari ya hicho chombo kwenye computer tu so hapo ndio wanaona picha nzima ya hicho chombo kiliivyo bila hata ya kukipiga picha kwa sababu hizo computers zinatoa enoumous amount of data ya hizo spacecraft yani kila kitu inakwambia mfano speed ya chombo,umbali ilipofikia,angle yake ilioweka,temperature,heat friction na vitu vyengine kibao mpka chombo kinafika
Nashukuru mkuu, lakini bado haujanipa jibu au pengine sijakuelewa.

Chukulia mfano wewe umemuagiza mtoto kwenda dukani(assume huyo mtoto hawezi kujipiga picha), lakini wakati huo wewe umebaki ndani.

Wewe utatumia mechanisim gan kupata picha ya mtoto na duka kwa pamoja.

NB: sio picha za satelite kwamba zinaweza kuonyesha direction ya chombo, distance n.k. bali picha halisi ndio ninazo zungumzia
 
Wamarekani sio wa kuamini. Uongo mwingi ili kuwatisha wengine.
Ni kitu gani kinaweza kuvumilia temperature zaidi ya 10000°

Halafu atuambie kwanini vyombo vinashindwa kutua mercury na wanakimbilia kwenye jua!?
Ngoja tuendelee kuhoji
 
Mchina siyo mchezo, tambo alizopiga kwa muda mfupi zinawaogopesha sana. Sasa hivi anahangaika kumwekea vikwazo kwenye kila kampuni anayoona ni tishio kwake nimeshangaa hadi kampuni ya drones ya DJI kaiwekea vikwazo, kuna kampuni inajishughulisha na mambo ya quantum computers nayo kaipiga vikwazo akidai ikifanikiwa itatumika kuhack system za wamarekani.
Week mbili nyuma mchina katest chombo cha anga ambacho kiliwashangaza wamarekani kwasababu kilirudi kikiwa speed kali sana na bado kikawa maneuvered tofauti na chombo chochote ambacho wamewahi kuwa nacho.
Kuja kushangaa kumbe ni version ya chombo ambacho mchina flani aliwahi fanya kazi NASA miaka ya 90 alikidesign kwaajili ya NASA, design yake wakaikataa. Kwenye miaka ya 2000s akarudi kwao akawapa design wakaimodify ndicho sasa hicho chombo kimefanyiwa testing kwa mara ya kwanza.
Usisahau kuwa mchina ni one man show, yeye ndiye nchi pekee mwenye space station ya pekee yake, ukiachilia mbali marekani, amefanikiwa kushusha chombo Mars kama one man show, wakati Ulaya wanashirikiana nchi kibao.
Wanasayansi waongo sana aisee!! Sijui wananichukuliaje!!?
 
Wao walionaje kama kinakaa kwa mkao huo?

Na kama wameweza kutengeneza picha isiyo halisi kwenye computer tunawezaje kuwa na hakika kama wamefikisha hiko chombo?

Eti mkuu!
Asante mkuu
Mimi nashangaa vile hawa weupe wanavyotuchukulia, yaani wanatuambia wametuma vyombo viwili kwa mkupuo serious!!?
Yaani wamerusha chombo cha kutafiti na wamerusha chombo cha kupiga picha chombo cha utafiti!!
Wananionaje mimi hawa??
 
Ni kweli na hakika ndugu, tangu uzaliwe hujawahi kuiona dunia ikizunguka wala ikiwa duara, hujawahi kuiona zaidi ya kusimuliwa na hao jamaa, pia;
Nina uhakika wote kuwa tangu uzaliwe hujawahi kuliona jua lililo stationary, never hujawahi kuliona zaidi ya kusimuliwa tu na hao jamaa!
 
Asante mkuu
Mimi nashangaa vile hawa weupe wanavyotuchukulia, yaani wanatuambia wametuma vyombo viwili kwa mkupuo serious!!?
Yaani wamerusha chombo cha kutafiti na wamerusha chombo cha kupiga picha chombo cha utafiti!!
Wananionaje mimi hawa??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]pengine wana majibu ngoja waje mkuu
 
Asante mkuu
Mimi nashangaa vile hawa weupe wanavyotuchukulia, yaani wanatuambia wametuma vyombo viwili kwa mkupuo serious!!?
Yaani wamerusha chombo cha kutafiti na wamerusha chombo cha kupiga picha chombo cha utafiti!!
Wananionaje mimi hawa??
Hapa jitahidi kwenda nao taratibu utapewa hukumu mbaya kwamba aidha wewe ni mfia dini au flat eather.
 
Halafu kuna mtu kutoka Buguruni akishiba ugali na dagaa anaiona Marekani iko chini eti China ipo juu, Sayansi ya hicho chombo ,ni kubwa ya hali ya juu,Urusi ijipange sana
hujui tu mainjinia na madesign walounda hicho chombo wengi ni hao unaowaponda

Marekani fala tu ikisemwa kila RAIA harudi kwao NASA itabaki nyeupe ndio mana siku zote NASA haifungamani na SIASA za MAJITAKA inajari zaidi UBORA wa mtu na mawazo IQ yake
na kukuongezea huo ugomvi unaouna wa kuekeana vikwazo linapokuja swala la FUTURE TECHNOLOGY hasa kwenda NJE ya ANGA hao jamaa wanaushirikiano mkubwa
 
Nashukuru mkuu, lakini bado haujanipa jibu au pengine sijakuelewa.

Chukulia mfano wewe umemuagiza mtoto kwenda dukani(assume huyo mtoto hawezi kujipiga picha), lakini wakati huo wewe umebaki ndani.

Wewe utatumia mechanisim gan kupata picha ya mtoto na duka kwa pamoja.

NB: sio picha za satelite kwamba zinaweza kuonyesha direction ya chombo, distance n.k. bali picha halisi ndio ninazo zungumzia
Poa mkuu najitahidi kukuelezea ila usikaze ubongo,ipo hivi
Spacecraft zote huwa zinafungwa kamera ili kupiga picha mahali ambapo imetumwa,mfano kama imetumwa iende sayari ya mars basi itafungwa kamera ikapige picha hiyo sayari ya mars kama vile ilivyofanya curiosity rover,kama imetumwa iende saturn basi itawekewa camera ikapige picha sayari ya saturn. Lakini hamna spacecraft inayofungwa kamera ili ijipige yenyewe wakati ipo safarini .Hizo picha za spacecraft unazoziona kama hiyo parker solar probe ni picha zilizotengenezwa tu na computer kwa ajili ya simulation ya mission na pia kurahisisha watu waweze kuelewa kinachoendelea kiurahisi, just imagine NASA au ROSCOSMOS ya urusi wangekuwa hawatoi picha yani watupe tu data ya vyombo vyao wanavyotuma huko si tungekuwa tunatafutana sahivi, kwa hiyo ili kurahisha mambo wakaona sehemu ambazo huwa haziwezi kupigwa picha huwa wanatengenezea wenyewe kwenye computer. Kwahiyo kiufupi kuna picha ambazo ni halisi na nyengine sio halisi ,picha halisi ni zile zinazopigwa na spacecraft zikiwa huko zilipotumwa kisha zinatumwa duniani mfano picha za dunia kutoka kwenye ISS,picha ya sayari ya mars,picha za jua kutoka kwa parker solar probe,picha za saturn,picha kutoka kwenye satellites etc. Na picha ambazo si halisi ni zile ambazo kuna sehemu hamna namna ambayo utaweza kupiga picha kwa hiyo huwa wanazitengeneza tu kwa computer mfano ndio kma hicho chombo kikiwa safarini kuelekea kwenye jua huwezi kukipiga picha hicho chombo kwakua hamna kitu kilichopo huko kwenye jua ambacho kitaweza kukipiga picha. So hapa unaweza kusema parker solar probe haiwezi kujipiga picha yenyewe wala kupigwa picha ila kinaweza kulipiga picha jua kwasababu imefungwa kamera ili iweze kuchukua picha za jua na kuzituma duniani na tayari imeshafanya hivyo mara nyingi tu.
 
Back
Top Bottom