Uhakika upo mana nishakwambia kwamba chombo kikfika huko pia kinapiga picha na kuzituma duniani,wewe umetuma chombo Mars kimefika na kikapiga picha huko Mars halafu kikakutumia utakua bado hujaamini tu?
Pia chombo kikisharushwa huko kwenye space tunaweza kuwasiliana nacho huku duniani na tukajua kipo wapi kinatembea spidi gani kina temperature kiasi gani na tukiomba picha za huko kinatutumia na mambo mengine mengi tu.Hata wewe sahvi unaweza ukadownload apps kwenye simu yako ambazo zinakupa mawasiliano na baadhi ya satellites ambazo zipo kwenye space mfano ISS pia kama una telescope unaweza ukaviangalia mwenyewe kupitia telescope yani kuna njia nyingi sana za kujua, sio wewe ukae tu useme umerusha chombo angani haya tukikwambia tunataka kukiona hicho chombo kwa telescope au tuwasiliane nacho kwa computer au tukiombe hicho chombo kiturushie picha za huko kilipo utafanayaje?
Nikutolee mfano satellite ya kwanza ilirushwa na warusi kipindi hicho ilikiwa ni soviet union, walivyoirusha walijua kabisa wapo watu watabisha kama hawajarusha sattelite kwa hiyo walichokifanya wakafunga radio transmitter kwenye hiyo sattellite ili ikishafika huko nje ya dunia iweze kutuma radio signals duniani, so wewe kama ulikuwa unataka ujue kama warusi kweli wamerusha satellite ulikuwa unachukua kifaa maalum kinachopokea mawimbi ya radio halafu kikishapokea hayo mawimbi kinaanza kutoa sauti,uwe marekani uwe Canada uwe ulaya uwe China hayo mawimbi ya radio yatakufikia tu ukitumia kifaa maalum cha kuyapokea. kwahiyo dunia nzima waliiamini satellite ya urusi mana hakukuwa na namna unaweza kubisha wakati satellite ipo na inasikika.
Na pia hao NASA wana washindani wao wakarne na karne ambao ni ROSCOSMOS ya urusi na space agency ya China,yani hata wakidanganya hao washindani wao hawawezi kukaa kimya hata siku moja mana wanashindana kwelikweli kila mmoja anatak aonekane yeye ndio yupo juu kwenye tafiti za anga kuliko mwenzake so sio rahisi kudanganya hata kidogo lazima uumbuliwe na hii tafiti ya kwenda kwenye jua Marekani amewapiga gepu kubwa sana warusi na wachina kwahiyo isingekuwa ya kweli wachina na warusi wasingenyamaza.