mashinetata
JF-Expert Member
- Oct 31, 2021
- 391
- 896
Asante sana nimekuelewa vizuri, sasa kama hizo picha si halisi yani watu wamecheza na adobe je, kutakuwa na uhakika gani kama hata hiko kifaa kimefika wakati hamna picha halisi zote ,zimetengenezwa?Poa mkuu najitahidi kukuelezea ila usikaze ubongo,ipo hivi
Spacecraft zote huwa zinafungwa kamera ili kupiga picha mahali ambapo imetumwa,mfano kama imetumwa iende sayari ya mars basi itafungwa kamera ikapige picha hiyo sayari ya mars kama vile ilivyofanya curiosity rover,kama imetumwa iende saturn basi itawekewa camera ikapige picha sayari ya saturn. Lakini hamna spacecraft inayofungwa kamera ili ijipige yenyewe wakati ipo safarini .Hizo picha za spacecraft unazoziona kama hiyo parker solar probe ni picha zilizotengenezwa tu na computer kwa ajili ya simulation ya mission na pia kurahisisha watu waweze kuelewa kinachoendelea kiurahisi, just imagime NASA au ROSCOSMOS ya urusi wangekuwa hawatoi picha yani watupe tu data ya vyombo vyao wanavyotuma huko si tungekuwa tunatafutana sahivi, kwa hiyo ili kurahisha mambo wakaona sehemu ambazo huwa haziwezi kupigwa picha huwa wanatengenezea wenyewe kwenye computer. Kwahiyo kiufupi kuna picha ambazo ni halisi na nyengine sio halisi ,picha halisi ni zile zinazopigwa na spacecraft zikiwa huko zilipotumwa kisha zinatumwa duniani mfano picha za dunia kutoka kwenye ISS,picha ya sayari ya mars,picha za saturn,picha kutoka kwenye satellites etc. Na picha ambazo si halisi ni zile ambazo kuna sehemu hamna namna ambayo utaweza kupiga picha kwa hiyo huwa wanazitengeneza tu kwa computer mfano ndio kma hicho chombo kikiwa safarini kuelekea kwenye jua huwezi kukipiga picha kwakua kinasafiri spidi kali mno na pia hamna kitu kilichopo huko kwenye jua ambacho kitaweza kukipiga picha
Mfano mimi nikianzisha taasisi inayo husiana na sayansi ya mambo ya anga then nika utangazia umma kuwa nimepeleka chombo hilo eneo halafu nikatengeza picha za namna hiyo, lakini niwe sijapeleka chombo wala nini. Nasa watakuwa wamenizidi kitu gani hasa katika fact?