NASA yaingia kwenye anga hewa la jua

Wao walionaje kama kinakaa kwa mkao huo?

Na kama wameweza kutengeneza picha isiyo halisi kwenye computer tunawezaje kuwa na hakika kama wamefikisha hiko chombo?

Eti mkuu!
Wamarekani sio wa kuamini. Uongo mwingi ili kuwatisha wengine.
Ni kitu gani kinaweza kuvumilia temperature zaidi ya 10000°

Halafu atuambie kwanini vyombo vinashindwa kutua mercury na wanakimbilia kwenye jua!?
 
Mbona kipo mkuu ,kuna chombo kinaitwa mariner 10 spacecraft kishawahi kwenda huko mercury ila hakikuland kwenye mercury kilifanya orbiting tu nakukusanya data. Mpaka sasa kitu ambacho hawajaweza ni kuiland spacecraft katika sayari ya mercury kwa sababu inakuwa ni ngumu sana kuslow its speed ili kiweze kuland safely kwakuwa mercury ipo karibu sana na jua.
 
Wao walionaje kama kinakaa kwa mkao huo?

Na kama wameweza kutengeneza picha isiyo halisi kwenye computer tunawezaje kuwa na hakika kama wamefikisha hiko chombo?

Eti mkuu!
Mbona mkuu kila siku zinarushwa rockets na vyombo mbalimbali huko angani na wala hamna anayeviangalia kwa macho jinsi vinavyosafiri na vyombo vinafika salama kabisa na kufanya kazi ambazo vimetumwa, watu wakishafanya mahesabu yao wanafunga sensors kwenye hicho chombo then wanaprogram computer ili kuweza kuwasaidia kumonitor safari ya vyombo vyao, hizo mission zote za warusi,wachina,wamarekani,wajapan na ulaya wote hao wakishatuma vyombo vyao wanatulia ndani ya jengo maalum wanaangalia safari ya hicho chombo kwenye computer tu so hapo ndio wanaona picha nzima ya hicho chombo kiliivyo bila hata ya kukipiga picha kwa sababu hizo computers zinatoa enoumous amount of data ya hizo spacecraft yani kila kitu inakwambia mfano speed ya chombo,umbali ilipofikia,angle yake ilioweka,temperature,heat friction na vitu vyengine kibao mpka chombo kinafika
 
Hafu Afrika tunasema tunaweza kushindana na beberuz, hao jamaa wako mbali miaka 500 ijayo,
 
Kwani umeme unasafiri Kwa Km ngapi kwa Sekunde? Au Mwanga?
 
Asa mkuu huyo muumba unayemsemea kaumba ulimwengu halafu hajui kama dunia ni duara,kaumba ulimwengu halafu hajui kama dunia ndio inazunguka jua. Anyway wanasayansi huwa wakitaka kufanya yao hawafikirii kabisa hzo habari za muumba na laiti ingekuwa hivyo basi hapa duniani tusingefika hapa tulipo sa hivi, kitu kingine huwa hawaamini kwamba kuna jambo haliwezekani wewe kwa akili yako ya kawaida utaona mambo mengi hayawezekani kufanyika ila wenzako wanayafanya bila ya shida yoyote. Hiyo speed ya hicho chombo inafikiwa kirahisi tu kwa kupata boost ya speed kutoka kwenye gravitational pull ya sayari zilizoko huko pia kutokuwepo kwa air friction
 
Usichukulie mazingira ya duniani ukafananisha na ya anga za mbali huko,kwa uelewa wangu mdogo wa physics huko anga za mbali hakuna friction force hivyo inafanya vyombo vinavyosafiri huko kukimbia speed kubwa sana.
 
Nashukuru mkuu, lakini bado haujanipa jibu au pengine sijakuelewa.

Chukulia mfano wewe umemuagiza mtoto kwenda dukani(assume huyo mtoto hawezi kujipiga picha), lakini wakati huo wewe umebaki ndani.

Wewe utatumia mechanisim gan kupata picha ya mtoto na duka kwa pamoja.

NB: sio picha za satelite kwamba zinaweza kuonyesha direction ya chombo, distance n.k. bali picha halisi ndio ninazo zungumzia
 
Wamarekani sio wa kuamini. Uongo mwingi ili kuwatisha wengine.
Ni kitu gani kinaweza kuvumilia temperature zaidi ya 10000°

Halafu atuambie kwanini vyombo vinashindwa kutua mercury na wanakimbilia kwenye jua!?
Ngoja tuendelee kuhoji
 
Wanasayansi waongo sana aisee!! Sijui wananichukuliaje!!?
 
Wao walionaje kama kinakaa kwa mkao huo?

Na kama wameweza kutengeneza picha isiyo halisi kwenye computer tunawezaje kuwa na hakika kama wamefikisha hiko chombo?

Eti mkuu!
Asante mkuu
Mimi nashangaa vile hawa weupe wanavyotuchukulia, yaani wanatuambia wametuma vyombo viwili kwa mkupuo serious!!?
Yaani wamerusha chombo cha kutafiti na wamerusha chombo cha kupiga picha chombo cha utafiti!!
Wananionaje mimi hawa??
 
Ni kweli na hakika ndugu, tangu uzaliwe hujawahi kuiona dunia ikizunguka wala ikiwa duara, hujawahi kuiona zaidi ya kusimuliwa na hao jamaa, pia;
Nina uhakika wote kuwa tangu uzaliwe hujawahi kuliona jua lililo stationary, never hujawahi kuliona zaidi ya kusimuliwa tu na hao jamaa!
 
Asante mkuu
Mimi nashangaa vile hawa weupe wanavyotuchukulia, yaani wanatuambia wametuma vyombo viwili kwa mkupuo serious!!?
Yaani wamerusha chombo cha kutafiti na wamerusha chombo cha kupiga picha chombo cha utafiti!!
Wananionaje mimi hawa??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]pengine wana majibu ngoja waje mkuu
 
Asante mkuu
Mimi nashangaa vile hawa weupe wanavyotuchukulia, yaani wanatuambia wametuma vyombo viwili kwa mkupuo serious!!?
Yaani wamerusha chombo cha kutafiti na wamerusha chombo cha kupiga picha chombo cha utafiti!!
Wananionaje mimi hawa??
Hapa jitahidi kwenda nao taratibu utapewa hukumu mbaya kwamba aidha wewe ni mfia dini au flat eather.
 
Halafu kuna mtu kutoka Buguruni akishiba ugali na dagaa anaiona Marekani iko chini eti China ipo juu, Sayansi ya hicho chombo ,ni kubwa ya hali ya juu,Urusi ijipange sana
China usiwachukulie poa, wako mbali sana
 
Halafu kuna mtu kutoka Buguruni akishiba ugali na dagaa anaiona Marekani iko chini eti China ipo juu, Sayansi ya hicho chombo ,ni kubwa ya hali ya juu,Urusi ijipange sana
hujui tu mainjinia na madesign walounda hicho chombo wengi ni hao unaowaponda

Marekani fala tu ikisemwa kila RAIA harudi kwao NASA itabaki nyeupe ndio mana siku zote NASA haifungamani na SIASA za MAJITAKA inajari zaidi UBORA wa mtu na mawazo IQ yake
na kukuongezea huo ugomvi unaouna wa kuekeana vikwazo linapokuja swala la FUTURE TECHNOLOGY hasa kwenda NJE ya ANGA hao jamaa wanaushirikiano mkubwa
 
Poa mkuu najitahidi kukuelezea ila usikaze ubongo,ipo hivi
Spacecraft zote huwa zinafungwa kamera ili kupiga picha mahali ambapo imetumwa,mfano kama imetumwa iende sayari ya mars basi itafungwa kamera ikapige picha hiyo sayari ya mars kama vile ilivyofanya curiosity rover,kama imetumwa iende saturn basi itawekewa camera ikapige picha sayari ya saturn. Lakini hamna spacecraft inayofungwa kamera ili ijipige yenyewe wakati ipo safarini .Hizo picha za spacecraft unazoziona kama hiyo parker solar probe ni picha zilizotengenezwa tu na computer kwa ajili ya simulation ya mission na pia kurahisisha watu waweze kuelewa kinachoendelea kiurahisi, just imagine NASA au ROSCOSMOS ya urusi wangekuwa hawatoi picha yani watupe tu data ya vyombo vyao wanavyotuma huko si tungekuwa tunatafutana sahivi, kwa hiyo ili kurahisha mambo wakaona sehemu ambazo huwa haziwezi kupigwa picha huwa wanatengenezea wenyewe kwenye computer. Kwahiyo kiufupi kuna picha ambazo ni halisi na nyengine sio halisi ,picha halisi ni zile zinazopigwa na spacecraft zikiwa huko zilipotumwa kisha zinatumwa duniani mfano picha za dunia kutoka kwenye ISS,picha ya sayari ya mars,picha za jua kutoka kwa parker solar probe,picha za saturn,picha kutoka kwenye satellites etc. Na picha ambazo si halisi ni zile ambazo kuna sehemu hamna namna ambayo utaweza kupiga picha kwa hiyo huwa wanazitengeneza tu kwa computer mfano ndio kma hicho chombo kikiwa safarini kuelekea kwenye jua huwezi kukipiga picha hicho chombo kwakua hamna kitu kilichopo huko kwenye jua ambacho kitaweza kukipiga picha. So hapa unaweza kusema parker solar probe haiwezi kujipiga picha yenyewe wala kupigwa picha ila kinaweza kulipiga picha jua kwasababu imefungwa kamera ili iweze kuchukua picha za jua na kuzituma duniani na tayari imeshafanya hivyo mara nyingi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…