Naseeb Abdul maarufu kama 'Diamond' ashikiliwa na Polisi kwa muda

Naseeb Abdul maarufu kama 'Diamond' ashikiliwa na Polisi kwa muda

Ile ilikuwa kick tu mtaona kwenye video yake mpya hadi vifaru vipo na hajaomba kibari
 
MSANII Naseeb Abdul (Diamond) leo anashikiliwa na polisi, siku moja tu baada Meneja wake Babu Tale kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta mwishoni wiki.

Habari zaidi zitafuata.

diamond3.jpg

mkuu badilisha hyo avatar
 
yote kheri awe na kibali asiwenacho ................
yangu macho na masikiooooooo
 
Huyu raia anayetamani combat halafu anaidhalilisha kwa kukata nayo mauno jukwaani dawa ni JKT mwaka mzima. Akitoka ataiheshimu combat.
 
Kwa hili navilaumu vyombo vya habari kwa kulikuza maana sijui kama ni kosa kuubwa kiasi hicho!
 
Ikiwezekana apigwe kabisa mana tumeshachoka.
 
Huyu raia anayetamani combat halafu anaidhalilisha kwa kukata nayo mauno jukwaani dawa ni JKT mwaka mzima. Akitoka ataiheshimu combat.

Adhabu kwa mujibu wa sheria ni tsh 500/- au kifungo cha mwezi mmoja jela
 
Wanapenda nguo zao

mafunzo wanayaogopa
==apewe adhabu kali sana huyo -----
 
Kwa hili navilaumu vyombo vya habari kwa kulikuza maana sijui kama ni kosa kuubwa kiasi hicho!

kwa mtazamo wako unadhani hivyo lakini kuna uzito wake. Najua huyu diamond alijua kuwa ni kosa ila alifanya makusudi. Acha sheria ichukue mkondo wake
 
kama mtampiga faini atalipa hakuna shida ila tukubali Jeshi letu limedhalilshwa vya kutosha na kijana huyu.
 
acheni uongo nyie... alipewa kibali... kumchafua tuu ndo mjuavyo

Sasa kama alipewa kibali meneja wake alishikiliwa kwa nini? Na yeye Platinamzi anashikiliwa kwa nini kama walipata kibali?
 
Ila jamani ustaa nao ni kazi, hivi katika mavazi yoote duniani hizo nguo zenye mabaka-mabaka ya namna hiyo ndio inaonekana zinapendeza saaaana kuvaa kwenye show?
 
Huyu jamaa anajua sana kufanya PROMO.

Sintashangaa watakuja kudai siyo nguo za Tanzania na mchezo uishe.

Ila mwisho wa siku, tumemtangaza kwa kishindo. Jamaa namkubali kwa kujitangaza,

Ukicheka na mbwa atakufuata msikitini! hawa kina Diamondo and the so called No school billioneas; mamlaka zikicheka cheka nao sana haya ndio matokeo; kanafikiri nchi iko mfukoni mwake. kama CDM kuandamana ni kuvunja sheria basi kuvaa sare za jeshi ni kuvunja sheria pia tumeambiwa hivyo, sasa hebu tuone kama PoliCCM watamgwaya "prezida" wa bongo flava!
 
Back
Top Bottom