Nasema tusiwapishe viti wazee kwenye daladala, walichezea ujana

Ndo unakomaa kwenye siti wee mara mzee anaomba akae unagoma kumbe ulikuwa unaenda kwenye mkutano wa kijini kutambulisha mradi halafu uliyemgomea ndo mwenyekiti wa kijiji....
Akikuomba mwenyewe kwa kinywa chake huna ujanja utampusha tu
 
kijana unasahau kwamba hata kma una gari, kuna siku utasafiri kwenda mkoa au mji mwingine, je hautapnda daladala ?
Kwani huo mkoa mwingine hauna taxi,bajaj?
 
Hapa mjini vijana wana zeeka haraka sana mtu ana miaka 40 lakini ukimtazama kama 60 au 70 wengine wana miaka 60 bado wana panga maisha ya mjini Dar hayana kanuni

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
Maisha ya kupanga matamu sana ukiwa kapera hasa upate nyumba yenye changanyikeni ya kistaarabu mixa watoto wakali
 
Nimependa hapo mwishoni mwa title ya uzi kusema “ wamechezea maisha” [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sasa wengi wamekuwa wakitumia hela vibaya na malaya kwa kuwahonga badala ya kutumia hela kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo ya familia halafu badae kuishia kuombaomba wapwa na lawama chungu nzima!


Ujana wako ulikula na nani uzeeni utake kuganda wapwazo [emoji108][emoji108]
 
Eti mtu anajifanya yeye ni chimwaga a.k.a tupatupa [emoji108][emoji108]

Mtazikumbuka hizo! [emoji4][emoji4]

Utapiga simu kwa mpwa hapokei ametingwa!
 
Baba usijione utakuwa kijana maisha na uwezo wa kununua gari, unakuja huku kwetu uzeeni tutakuona unasurvive vipi na hiyo pension.

Unadhani watu wote wana pension ya milioni tano kwa mwezi?
 
Na kadiri unavyohonga mchepuko nyingi ndio huwa anazidi kukuletea mahitaji chungu nzima!

Atakuletea ya kwake , ya watoto wa kufikia, ya wazazi wake na nduguze !

Ambao hao wote hakuna atakaeluja kukulipia hela ya matibabu utakapokuja kuumwa ukiwa umeluzu.

Mchuma janga hula na wakwao!
 
Mzazi mwema huacha urithi hadi kwa wana wa wa wanawe yaani wajukuu.

Hivi kama una mali za hadi kutumiwa na wajukuu utagombana na wanao kuwa hawakutunzi?!

Mali zako zitakutunza
Hadi Yesu arudi bila kuhusudu msaada wa watoto wako wala wajukuu.

Utaendelea kuwa mshauri tu wa nyendo zao ili kuepuka mabaya na familia zao.
 
Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu ukiona mtu amefika umri wa uzee halafu hana mali kiasi cha kurithisha wana hadi wajukuu basi mtu huyo ajihoji na kujipigapiga kifuani mwake !
 
Ishu sio kumpisha mtu yeyote. Kile ni chombo cha biashara, haupandi bure, uwe mzee au kijana. So kama hutaweza kusimama ni vizuri usubiri lije lingine utakalo kaa, usiwakwaze wengine ambao kama ww unavyotaka kukaa wao pia wanahitaji kukaa.

Huwez jua mtu alikua wapi kukaa muhimu, as long as unalipa nauli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mna laana nyote mnaoshabikia uzi huu! Hujui unaweza pambana na ukapata pesa, afu yule aliyeko juu akakuamulia vingine, ukakuta tu siyo huna gari, bali hata hela ya daladala!
 
Mna laana nyote mnaoshabikia uzi huu! Hujui unaweza pambana na ukapata pesa, afu yule aliyeko juu akakuamulia vingine, ukakuta tu siyo huna gari, bali hata hela ya daladala!
Pambana tu mkuu hata ukikosa dunia itajua ulipambana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…