Nasema tusiwapishe viti wazee kwenye daladala, walichezea ujana

Ndiyo maana huwa nawaambia jamaa zangu kuwa, hata kama umejenga Dar, jitahidi sana kujenga nyumba ya kawaida tu nyumbani kwenu, utaishi kwa starehe sana. Hata Mzaramo ana kwao(Maneromango).
Miaka 60+ kukaa Dar ni uchuro!
 
Mfano nimetokea katavi unataka nije na gari langu?? au naenda kwenye matibabu unataka niende na gari langu, akiri yako ina matatizo na ulaaniwe.
 
Walemavu tuwapishe hawakuomba kuwa walemavu. Wajawazito na wenye watoto inahitaji mjadala Ila wazee hapana.

Mitaani kuna magari hadi milioni tatu, bodaboda used mpaka laki sita, hivi kweli mpaka unafika miaka sitini na zaidi hata pikipiki imekushinda.

Tukiacha kuwapisha tutawapa uchungu wa kupambana na maisha hata katika uzee wao.

Kuwapisha siti ni kuwadekeza na kuwafanya wabweteke. Vijana pambaneni msitegemee hisani ya kupishwa siti uzeeni

Mimi hata ukija na miaka 89 sikupishi nakuangalia macho makavu sikupishi
We kula bata ujanani ila jua uzeeni tutakutana kwenye daladala.

Uzee si ugonjwa ni baraka tusiogope uzee, nimejisikia kuwatania babu na bibi zetu.
Waheshimu baba na Mama, upate miaka mingi na heri duniani.
 
Mfano nimetokea katavi unataka nije na gari langu?? au naenda kwenye matibabu unataka niende na gari langu, akiri yako ina matatizo na ulaaniwe.
We mzee punguza munkari tafuta hela ukiumwa upande walau bajaj au ubber
 
Umeongea point ....ila wazee walioendekeza starehe ujanani wanakuja kukutukana huku wakijificha kwenye kivuli cha "utalaaniwa "..[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Stress za mzee aliyefeli maisha sio za kawaida
 
We mzee punguza munkari tafuta hela ukiumwa upande walau bajaj au ubber
Vyote vipo ila inafika mahali hauwez kuvigusa hata hizo hela hauwez kusoma tarakimu labda upate msaada, hujawahi enda ATM ukakuta mzee akakwambia naomba msaada wako unitolee hela, je mtu kama huyo anaweza kuendesha gari???
 
Yule mtu aliyeishi akiuza dagan, mbogabaoga, genge sokoni mpaka uzee wake. Mnataka awe na gari.
Yule baba yake Diamond wa kweli, aliyekuwa Tandale sokoni maisha yake yote yo mnataka awe na gari au boda hata ya wizi.
Yule mtu aliyeishi akiamka mapema asubuhi kwenda shambani kukulima kutwa nzima ili kujitafutia chakula chake mpaka akazeeka, mnataka awe na gari.
Hata hivyo, kuna wazee wala hawana haja ya magari unayoyazungumzia. Wana hela za kula, magari wamewaachia watoto wao wajinga wajinga kama wewe, wanalala sebuleni ingawa wana nyumba nzuri kuliko unayolala. Wanaona raha tu kupanda daladala kama mimi.
Nakutakia heri na baraka uliyeanzisha uzi huu, kwa kuwa umetambua hayo mapenda. Uzeeni utakuwa na CHOPA na Jet imepaki pale airport. Gari dogo sana kwako.
 
Pesa mwana haramu ndugu ..ukiwa na hela chawa watakuzunguka tu,utapata dereva wa gari yako na utaoa binti mbichi wa kukupa joto.nyumba itajaa wajukuu nk,ukiwa huna kitu huoni mtu
 
ni kweli wazee wengi walishika hela enzi zao lakini mifumo na sera za kijamaa iliyokuwepo ilikuwa ngumu kumiliki usafiri na vingine vya ziada hivyo tuwasamehe, ila hawa wazee wajao kuanzia 2000 kuja juu msiwasamehe tu maana wameutumia ujana wao huku nchi imeshafunguliwa kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya + kazi iendelee
 
Yule mtu aliyeishi akiuza dagan, mbogabaoga, genge sokoni mpaka uzee wake. Mnataka awe na gari.
Yule baba yake Diamond wa kweli, aliyekuwa Tandale sokoni maisha yake yote yo mnataka awe na gari au boda hata ya wizi.
Yule mtu aliyeishi akiamka mapema asubuhi kwenda shambani kukulima kutwa nzima ili kujitafutia chakula chake mpaka akazeeka, mnataka awe na gari.
Hata hivyo, kuna wazee wala hawana haja ya magari unayoyazungumzia. Wana hela za kula, magari wamewaachia watoto wao wajinga wajinga kama wewe, wanalala sebuleni ingawa wana nyumba nzuri kuliko unayolala. Wanaona raha tu kupanda daladala kama mimi.
Nakutakia heri na baraka uliyeanzisha uzi huu, kwa kuwa umetambua hayo mapenda. Uzeeni utakuwa na CHOPA na Jet imepaki pale airport. Gari dogo sana kwako.
Jipe moyo mkuu .hakuna mzee mwenye gari dar akafurahia kupanda daladala kwa Dar,labda mikoani,usafiri wa umma dar ni wa kudhalilishana sana,tafuta hela hujachelewa , usipofanikiwa muachie Mungu atleast ulipambana,get rich or die trying usikate tamaa
 
Back
Top Bottom