Nasema tusiwapishe viti wazee kwenye daladala, walichezea ujana

Kama uko ulaya sawa ila bongo ukiacha mwendokasi the rest ni kero sana majasho,konda kukutukana ,kukanyagana,kuegemeana,kubahashiana,kukaa kwa foleni muda mrefu.hapo ndio umetoka mishen town zako zimebuma
Ndugu Mwendokasi Ina afadhali gani?Ni tatizo tu Kama mengine
 
Mafanikio hayapimwi kwa kuwa na gari tu? Hata heshima kwenye jamii ni zao la matumizi mazuri ya ujana ila najua kwakua umejengwa kwenye vitu huwezi kunielewa. Wengine wana magari lakini wakati mwingine wanachagua kupanda daladala either for fun or for refreshment
 
Kwnn hamuwapishi wenye watoto.
Bro,huu Mji unatufunza Sana tabia zote mbaya!na mimi pia nina watoto,sijawahi kupishwa na mwanamke mwenzangu hata siku moja niliwahi bahatika kupishwa kama mara mbili Ila Ni wanaume,Hii Imenifanya kuwa makini Sana siku ninayojua natumia public transport nikiwa na watoto,naweka budget vizuri,nageuka na gari,nalipia Siti ya mtoto wangu na mtu akijifanya naomba nikae nitampakata Ni big NO.......Na wenye vibendi vilevile sipishi hata maana hata mimi nilishakuwa nacho sikuona hiyo favor,........na uso wangu huwa mkavu tu Wala sipepesi macho
 
Jamani, this made me cry.
 
Uko sahihi maisha ni kitu kipana ila tujadili kero za daladala kwa wazee,
 
Me wazee HUWA siwapishi kabisaaaa naaminigi kua maishani mwao wamepitia mengi na magumu kwahiyo HILI la kusimama kwenye gari ni chamtoto tu[emoji4][emoji4][emoji4]
[emoji23][emoji23][emoji23],Dah!!!,haya bhana.
 
Huu Ni ukweli,ndio maana watu wenye roho nzuri wengi wao wanaishia kuwa na uchumi wa Kati au wa chini.
 
Tuwasawehe tu wazee wetu,zamani kulikuwa hakuna mikopo ya magari Kama Sasa...ukute wengi humu tunawabeza Hawa wazee wetu Ila ukichunguza magari tuliyonayo Ni matokeo ya kuwezeshwa na mabenki...
 
Mkuu! Kumbuka unaweza ukatafuta halafu ukipata, usitukane mamba kabla hujavuka mto.
 
Halafu unakuta magari kibao hakuna shida ya usafiri wanapanda tu, pia wajawazito. Nitakae mpisha ni mgonjwa tu.
Huwa sielewagi,hakuna shida ya usafir halafu mtu anapanda kwenda kusimama n thn mtu anampisha kukaa wakat aliacha gar nyngne hata haijajaa.Kiukweli mm sikupish uwe mjamzito,sijui una mtoto mchanga,mzee au kikongwe.Itakua imekula kwako.
 
Ama kweli "Uungwana ni vitendo"

Yani kasafari ka kilomita 2 au 3 nako kakukoseshe utu[emoji849][emoji849][emoji849]

watu wanasimama kilometa 100 halafu fresh tu, Kweli kuishi kwingi kuona mengi aisee [emoji119]
 
BOGUS
 
Ama kweli "Uungwana ni vitendo"

Yani kasafari ka kilomita 2 au 3 nako kakukoseshe utu[emoji849][emoji849][emoji849]

watu wanasimama kilometa 100 halafu fresh tu, Kweli kuishi kwingi kuona mengi aisee [emoji119]
Binafsi huwa nawapisha siti, ila mostly inategemeana maana Ni tendo la kiutu na siyo lazima.

Kuna siku nilikuwa natoka Bukoba kuja Mwanza, nikawa nimepanda stand Bukoba kwahiyo nikapata siti.

Bus lilipofika Muleba akapanda Mzee mmoja, ila alikuta siti zimeisha baada ya KUSIMAMA kwa muda mrefu, akaniomba, kijana naomba nikupe 1,000 (elfu moja) nikae.

Nilivyomuona nikaona kweli anahitaji kukaa Wala buku lake sihitaji. Nikamwambia kaa tu mzee Wala usijali.

Tulivyofika Busisi Ferry akanitafuta, anilipie Ferry nikwamwambia Haina haha mzee.

Sometimes, hivi Ni viti ambavyo hata havikuumizi ukivifanya. Kwahiyo sioni shida.

Tatizo kubwa na baadhi ya wazee kwa Dar kukosa ustaarabu. Yaani unapanda daladala, unapata siti, anakuja mzee unampisha unasimama.

Sasa kumbe mzee mwenyewe anashuka karibu tu, badala akwambie urudi kwenye siti yake yeye anshuka tu anasepa bila hata shukrani utafikiri nlikuwa Ni haki yake.

Na akishuka, kwenye siti anakaa mchizi boti tu , halafu wewe unaendeleaje kushika bomba mpaka mwisho wa Safari.

Huo ndio upuuzi mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…