Nasema tusiwapishe viti wazee kwenye daladala, walichezea ujana

Nasema tusiwapishe viti wazee kwenye daladala, walichezea ujana

Kama uko ulaya sawa ila bongo ukiacha mwendokasi the rest ni kero sana majasho,konda kukutukana ,kukanyagana,kuegemeana,kubahashiana,kukaa kwa foleni muda mrefu.hapo ndio umetoka mishen town zako zimebuma
Ndugu Mwendokasi Ina afadhali gani?Ni tatizo tu Kama mengine
 
Walemavu tuwapishe hawakuomba kuwa walemavu. Wajawazito na wenye watoto inahitaji mjadala Ila wazee hapana.

Mitaani kuna magari hadi milioni tatu, bodaboda used mpaka laki sita, hivi kweli mpaka unafika miaka sitini na zaidi hata pikipiki imekushinda.

Tukiacha kuwapisha tutawapa uchungu wa kupambana na maisha hata katika uzee wao.

Kuwapisha siti ni kuwadekeza na kuwafanya wabweteke. Vijana pambaneni msitegemee hisani ya kupishwa siti uzeeni

Mimi hata ukija na miaka 89 sikupishi nakuangalia macho makavu sikupishi. We kula bata ujanani ila jua uzeeni tutakutana kwenye daladala.

Uzee si ugonjwa ni baraka tusiogope uzee, nimejisikia kuwatania babu na bibi zetu.
Mafanikio hayapimwi kwa kuwa na gari tu? Hata heshima kwenye jamii ni zao la matumizi mazuri ya ujana ila najua kwakua umejengwa kwenye vitu huwezi kunielewa. Wengine wana magari lakini wakati mwingine wanachagua kupanda daladala either for fun or for refreshment
 
Kwnn hamuwapishi wenye watoto.
Bro,huu Mji unatufunza Sana tabia zote mbaya!na mimi pia nina watoto,sijawahi kupishwa na mwanamke mwenzangu hata siku moja niliwahi bahatika kupishwa kama mara mbili Ila Ni wanaume,Hii Imenifanya kuwa makini Sana siku ninayojua natumia public transport nikiwa na watoto,naweka budget vizuri,nageuka na gari,nalipia Siti ya mtoto wangu na mtu akijifanya naomba nikae nitampakata Ni big NO.......Na wenye vibendi vilevile sipishi hata maana hata mimi nilishakuwa nacho sikuona hiyo favor,........na uso wangu huwa mkavu tu Wala sipepesi macho
 
Unenikumbusha Miaka kadhaa nyuma; kuna Jamaa alikuwa mwanafunzi chuo flani amepanga kwa Msataafu mmoja anaishi na Familia yake..

Huyu Mwanachuo alikuwa mtu Wa Dini sana ilhali Vijana Wa Mzee Mstaafu walikataa shule wakawa watu Wa mitungi na Bhange tu. Mstaafu akatokea kumwelewa sana Bwana mdogo mpaka akamkabidhi Kadi yake ya Benki. Siku akitaka pesa anamwambia Dogo amtolee mpunga Kwenye ATM maeneo ya chuoni kwao akirejea maskani awe anampatia.

Maisha yakaenda hivyo, huku Familia haijui kuwa Mzee amekabidhi kadi kwa Dogo maana Mzee alimwambia wakijua watakusumbua.. Sasa siku moja Ghafla Mzee Presha ikapanda, ile kumwahisha Hospitali akafia njiani. Jioni Jamaa anarejea akakutana na msiba, Mama Analia na kuomboleza wataishije bila Mzee.

Dogo akala buyu tu mpaka walipomaliza kuzika ndipo akamwita Mama pembeni akamkabidhi kadi akamwambia hii alinipa Mzee niwe namtolea Pesa na kwenye akaunti kimebakia kiasi kadhaa. Mama hakuamini macho yake. Kuanzia siku ile Dogo akawa halipi kodi na akawekwa kwenye orodha ya msosi kama mmoja Wa watoto Wa Mama. Na jukumu la kutoa pesa Mama akamwachia aendelee nalo pindi akihitaji pesa.

Yule Jamaa alipomaliza chuo hakumaliza mwezi Mtaani akala Shavu kwenye Mashirika ya UN, Mshahara mnono na marupurupu ya maana. Mpaka Leo anamhudumia yule Mama pamoja na kuipa sapoti zote Familia ya Marehemu Mstaafu, na hata shughuli za kuozesha mabinti Wa Mstaafu Mama alimkabidhi Jamaa asimamie kama Kaka Mkubwa Wa Familia..
Jamani, this made me cry.
 
Mafanikio hayapimwi kwa kuwa na gari tu? Hata heshima kwenye jamii ni zao la matumizi mazuri ya ujana ila najua kwakua umejengwa kwenye vitu huwezi kunielewa. Wengine wana magari lakini wakati mwingine wanachagua kupanda daladala either for fun or for refreshment
Uko sahihi maisha ni kitu kipana ila tujadili kero za daladala kwa wazee,
 
Me wazee HUWA siwapishi kabisaaaa naaminigi kua maishani mwao wamepitia mengi na magumu kwahiyo HILI la kusimama kwenye gari ni chamtoto tu[emoji4][emoji4][emoji4]
[emoji23][emoji23][emoji23],Dah!!!,haya bhana.
 
Sio wazee wote unaowaona walikuwa wanakula bata ujana wao ila wengine walikuwa mishahara yao inalipa Ada za ndugu halafu ndugu walipopata kazi za maana wakawatupa

Kuna mzee alikuwa waziri na Mbunge alisomeshwa na ndugu yake wa damu ila baada ya kufaulu vizuri na kuwa na kazi nzuri hakumsaidia ndugu yake kabisa kisa eti mlevi

Wote wametangulia mbele ya haki ila hakumtendea haki ndugu yake

Na hao ndio wakipanda bus unamhukumu na kusema ujana aliumaliza kwa raha kumbe ni kuhangaika mwanzo mwisho mpaka kaburini
Huu Ni ukweli,ndio maana watu wenye roho nzuri wengi wao wanaishia kuwa na uchumi wa Kati au wa chini.
 
Tuwasawehe tu wazee wetu,zamani kulikuwa hakuna mikopo ya magari Kama Sasa...ukute wengi humu tunawabeza Hawa wazee wetu Ila ukichunguza magari tuliyonayo Ni matokeo ya kuwezeshwa na mabenki...
 
Halafu unakuta magari kibao hakuna shida ya usafiri wanapanda tu, pia wajawazito. Nitakae mpisha ni mgonjwa tu.
Huwa sielewagi,hakuna shida ya usafir halafu mtu anapanda kwenda kusimama n thn mtu anampisha kukaa wakat aliacha gar nyngne hata haijajaa.Kiukweli mm sikupish uwe mjamzito,sijui una mtoto mchanga,mzee au kikongwe.Itakua imekula kwako.
 
Ama kweli "Uungwana ni vitendo"

Yani kasafari ka kilomita 2 au 3 nako kakukoseshe utu[emoji849][emoji849][emoji849]

watu wanasimama kilometa 100 halafu fresh tu, Kweli kuishi kwingi kuona mengi aisee [emoji119]
 
Nadhani vijana wengi humu wanaongelea nadharia kuna kundi kubwa sana la vijana ambao sasa hivi wana Miaka kibao ajira hamna wengine wana Miaka 40 sasa hivi hawajapata kazi na wamesoma muda sio mrefu wataingia kundi la wazee Kusema walichezea maisha ni kukufuru na kutowapisha viti ni kuwaadhibu Mara mbili

Anyway kifupi mleta mada ana roho ya kishetani na wote wanaom mu support wana roho za kishetani mtakwama mbeleni kimaisha kwa sasa mwajiona salama kwa visenti vichache na vigari mitumba vilivyookotwa majalalani Japan mnavyotembelea .Lakini safari bado ndefu. MUNGU AWALAANI KWA KUTOHESHIMU WAZEE

Amri ya Mungu inasema waheshimu Baba yako na mamako update kuwa na siku nyingi zenye heri duniani .Kutoheshimu wazee kunafupisha maisha au siku zenye heri ndio maana vijana wengi sana sasa hivi wanakufa kuliko wazee na wanaharibikiwa sana vitu vingi kama ukosefu wa kazi,maisha magumu maofisini na majumbani kwenye familia zao,nk lakini sababu kuu ni kuwa heshima kwa wazee hamna .
Na mlaaniwe na Mungu wote mlioonyesha kutokuwa adabu kwa wazee humu riziki zenu zipotee na muwe na maisha magumu ambayo hakuna atayeweza kuyabadilisha hadi mfe
BOGUS
 
Ama kweli "Uungwana ni vitendo"

Yani kasafari ka kilomita 2 au 3 nako kakukoseshe utu[emoji849][emoji849][emoji849]

watu wanasimama kilometa 100 halafu fresh tu, Kweli kuishi kwingi kuona mengi aisee [emoji119]
Binafsi huwa nawapisha siti, ila mostly inategemeana maana Ni tendo la kiutu na siyo lazima.

Kuna siku nilikuwa natoka Bukoba kuja Mwanza, nikawa nimepanda stand Bukoba kwahiyo nikapata siti.

Bus lilipofika Muleba akapanda Mzee mmoja, ila alikuta siti zimeisha baada ya KUSIMAMA kwa muda mrefu, akaniomba, kijana naomba nikupe 1,000 (elfu moja) nikae.

Nilivyomuona nikaona kweli anahitaji kukaa Wala buku lake sihitaji. Nikamwambia kaa tu mzee Wala usijali.

Tulivyofika Busisi Ferry akanitafuta, anilipie Ferry nikwamwambia Haina haha mzee.

Sometimes, hivi Ni viti ambavyo hata havikuumizi ukivifanya. Kwahiyo sioni shida.

Tatizo kubwa na baadhi ya wazee kwa Dar kukosa ustaarabu. Yaani unapanda daladala, unapata siti, anakuja mzee unampisha unasimama.

Sasa kumbe mzee mwenyewe anashuka karibu tu, badala akwambie urudi kwenye siti yake yeye anshuka tu anasepa bila hata shukrani utafikiri nlikuwa Ni haki yake.

Na akishuka, kwenye siti anakaa mchizi boti tu , halafu wewe unaendeleaje kushika bomba mpaka mwisho wa Safari.

Huo ndio upuuzi mtupu.
 
Back
Top Bottom