Nasema ukweli kuhusu uganga

Kwa hiyo tufuate darasa ama?
 
Mimi naonaga kila mganga ni mchawi maana anatumia mamlaka za giza, au nakosea?
 
Uganga = Uchawi.

Wote wapo chini ya kitengo cha kuongozwa na nguvu za giza kutoka kuzimuni.
Uchawi ni taaluma iliyo mbele ya wakati, ni wakati sahihi sasa wa kuiboresha ili iweze kulinufaisha taifa.

Uchawi unaweza kutumika kusafirisha vitu au watu haraka kuliko chombo chochote ulimwenguni.

Uchawi unaweza kuleta mafanikio ya haraka kwa jambo lolote mfano elimu, biashara, kazi n.k

Uchawi unaweza kumtanguliza mtu kaburini

Kwaharaka haraka utabaini uchawi ni taaluma nzuri inayoweza kuleta mapinduzi makubwa ila wenye shida ni watumiaji wa taaluma husika
 
Anayemfahamu mganga kwelikweli anisaidie nataka kumfunza mtoto wa mtu ambae hakufunzwa na mama yake adabu na heshima 🤣🤣
Ninyi ndio mnasababisha taaluma hii ionekane ni ya hovyo, %kubwa ya watanzania tunadhani uganga au uchawi ni kufanya mambo mabaya tu.

Uganga ni taaluma inayoweza kukusaidia kujua yaliyopita ambayo hukubahatika kuyaona au kuyahisi, yaliyopo ambayo huyajui, na yajayo.
 
Ni kweli napia ndio.maana watu hupewa kuwasaidia watu kutatua shida zao
 
Umepanic brother!!
 
Halafu wanapinga eti hakunaga wapo waganga wengi wazuri nawanasaidia
Usikubali kushauriwa na mtu mwenye DIPLOMA halafu anajiita MSOMI. Ni URONGO hana usomi wowote ni makaratasi matupu ya KUGANGA NJAA.

USOMI WA KWELI ni kutambua mambo bayana na yasiyo bayana kisha kuyapima katika uhalisia wa MAISHA YA KAWAIDA (PRACTICAL EXPERIENCE) na KUYASHABIHIANISHA na MUUNGANIKO WA MATUKIO au MUUNGANIKO WA TAARIFA (PATTERNS).

Mtu hawezi kuja na vikaratasi vyake vya DIPLOMA aanze kutamba yeye ni msomi wakati sote tunajua hana alijualo.

Mimi mwenyewe ni msomi kweli kweli, lakini ninajua mengi yaliyo nje ya vyeti vya darasani, kwahiyo mtu akija na KADIPLOMA KAKE lazima nimnyuke kweli kweli bakora za kisogo.
 
min -me njoo usome! Sweety ake kaniona kwa macho ya rohoni😂
 
Uongo mtupu...

Familia zote za kiafrika zina waganga...

Haya umeyaandikia kuwasema WAGANGA wa kule Kyiv Ukraine ?!!! [emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…