Hiyo ni hadithi ya kusadikika, binafsi nimeoa huko ulikotaja na wakati ninaoa sikuwa na kiwanja achilia nyumba ndo usiseme.
Kuna mtu ni muajiriwa either serikalini au kampuni flani, unataka kila anakoenda awe na nyumba yake asipange?. Hilo haliwezekani.
Mfano hapa Arusha vijana wenye sifa ya kuoa na wameoa wake zao wenye asili ya hukuhuku wengi wao tuseme zaidi ya 75% hawana nyumba zao wenyewe walizo jenga, ni either amepanga au anaishi kwenye nyumba inayomilikiwa na familia, taasisi, shirika, serikali n.k, wengi wanajenga wakiwa kwenye ndoa, hivyo ni ngumu kwa vijana wadogo hususani walioko mjini kumiliki nyumba kabla hajao ingawa wapo wachache waliojenga kabla ya kuoa.
Ungesema vijijini ni mhimu kuwa na nyumba kwa kijana kabla ya kuoa hakika hakuna ambaye angeshangaa hilo ila mijini nimezunguka karibu karibu Tanzania yote lakini vijana wengi wa mijini wanaanzia maisha kwenye nyumba za kupanga.
Ukiwa kijijini, ni ngumu kwa kijana ambaye hajaoa amiliki gari kabla ya kujenga nyumba lakini kwa mjini kuwa na gari kabla ya kuitwa baba mwenye nyumba ni suala kawaida sana.