Nashauri coach Gamondi atupishe

Gamondi ni kocha mbovu

Na litimu lenyewe ni libovu

Wachezaji nao wanatembea na mademu wabovu

Ni ubovu,ubovu,ubovu,ubovu kila mahali.
 
Naunga mkono hoja! Na hata jana baada tu ya kile kichapo, nilitoa ushauri wa aina hii.

Sema tu kwa kuweka kumbukumbu sawa; Farid Mussa alifanyiwa upasuaji. Hivyo bado atakuwa hajapona.

Na kuhusu Kibwana Shomari, nadhani kukaa benchi muda mrefu kumempotezea uwezi wake wa kujiamini. Mechi yake ya mwisho kucheza, nilishuhudia mapungufu mengi ya kiulinzi kutoka kwake.
 
Nlianza kutia shaka uwezo wa huyu kocha baada ya kulazimisha Sure boy acheze holding midfielder! Sure boy mtam akicheza namba 8!

Mudadhiri ni mchezaji mzuri ila changamoto transition passes hawez, yeye ni kupiga tu mipasi ya pemben🚮🚮
 
Nabi aliwapa nafasi akina Job na Bacca na Sasa ndo mabeki tegemeo wa timu ya Taifa
Nabi alimpa nafasi Mzize mbele ya striker kama Mayele hadi akacheza final na Sasa ndo anatufaa kama strike
Gamondi yeye amekariri Aziz ki tu
Yanga ya vijana Kuna dogo nilimwona ni beki mzuri kwanini hakumpandisha akawa anampa hata dakika 10
 
Upo sahihi kabisa yaan Yanga wanachofanyiwa ni kujaziwa msitu wa wachezaji kwenye goli pinzani wanakosa pa kupita sasa wanatumia mfumo wa kutaka kupita pale pale kati na kutaka kuzama kwenye box huku wakipasiana wakati wanatakiwa kuachia mashuti nje ya 18 tu goli linaingia ila wao wamekazana wanataka wakafunge mbele ya kipa hio ni ngumu wabadirishe mfumo mambo ya pass pass mpaka kwenye box ni uboya nje ya box pale pale wakipata mwanya waachie madongo lazima goli liiingie jana wamepoteza nafasi nyingi za magoli ya nje ya box kisa mipass pass mpaka ndani ya box mipass pass mpaka ndani ya box ya nini waachie madongo hata nje ya box tu goli lazima liingie

Kingine kuna wachezaji hawatakiwa kuanza dakika 45 za kwanza nimewaona jana wakianza wanapoteana mfano mdogo Aziz Ki Pacome Maxi hawa inabidi watokee bench ila Gamond sijui haoni au anafanya makusudi tu Chama Dube Mzize hawa inabidi waanze dakika 45 za kwanza ukiangalia mechi nyingi ambazo Aziz Ki Maxi Pacome wametokea bench ushindi lazima kwa Yanga ila Gamond sijui hili halioni au anafanya makusufi tu

Chama Dube Mzize wanatakiwa waanze kipindi cha kwanza dakika 45 kisha cha pili Maxi Pacome Aziz Ki waongezee pumzi na akitaka kumuongeza Baleke amuingize kipinda cha pili dakika za mwishoni hapo lazima Yanga ishinde tu kinyume na hapo Yanga itakua inachezea magoli kwa kwenda mbele

Kingine Gamond awahimize wachezaji wawahi kurudi golini wanaposhambuliwa sio wanabakia nyuma wakati wakiwa wanashambuliwa huku nyuma kunakua hakuna mtu timu haina mabeki kwa hio inabidi wajue hilo sio wanabaki nyuma wakiwa wanashambuliwa watafungwa sana kila mechi maana wengi wameshawasoma mfumo wao ulivyo Mwamnyeto na Aucho peke yao hawawezi kuzuia goli lisifungwe mbele ya wachezaji 7 wa Tabora wanaopigiana pass huku na huku kuwatoka lazima goli liingie

Kingine Diarra aongezewe mazoezi ya kudaka jamaa hafuati mipira kabisa magoli ya jana yote hakuna hata 1 alilofuata mpira, ukiangalia kipa wa Tabora aliedaka ile penati ya Aziz Ki utagundua kitu yule kipa anafuata mipira ila Diarra mipira anaiacha iingie golini afuaati mpira hata kuruka haruki sana sana atarukia mipira inayopigwa juu kudaka, kwa uzuri ukiangalia goli la pili km sio la tatu lile goli ambalo Mwamnyeto na Aucho walikua wanajaribu kuzuia wakati Tabora washafika golini kwa Yanga wakipasiana pale Diarra angeruka kufuata mpira angeupangua na lingekua sio goli labda yule mchezaji wa Tabora angelazimisha kufunga tena

Kingine Nickson Kibabage anajituma sana jana amecheza kwa kujituma kweli kweli ila ndio hivyo tu mmaliziaji wa goli hakuwepo, tukija kwa Chama Sureboy Mzize Pocome Maxi hawa inabidi waachie madogo kila wanapolikaribia goli Aziz Ki mara nyingi amekua akipiga madongo ila madongo yake yanakua hayana faida yoyote anababatiza mtu mpira anambabua sasa hio haileti goli

Yaan mapungufu ni mengi sana wachezaji wa Yanga wanafika goli la Tabora wanaanza kuogopaa kufunga goli wanazungukia tu hapo hapo kwa hio Gamond aelekeze hilo, wachezaji wasipoteze confidence uwanjani maana sasa kila timu imeamua iwakazie na kuwakamia na wenyewe wanatakiwa wakamie bai ene minzi goli lazima liingie lazima wafunge kivyovyote tu wakicheza kurembaremba ndio wanaishia kufungwa fungwa tu, golini wakifika wasilembeee waachie madongo golini waache mambo ya penetration pass mpaka ndani ya 18
 
Mkuu kaaa kwa kutulia. Kazi ya ukocha sio rahisi kama unavyodhani.
 
Hapa bado kabisa hamjasema...

Tunahitaji muwe mahili wa kunena kwa lugha.
 
Yani Yanga kweli timu kubwa,kila nyuzi ukifungua ni Yanga tu,mbona timu zipo nyingi ongeleeni basi ata Mashujaa ,inaonekana Yanga ametesa sana timu nyingi hapa bongo.
 
Kipa anataka kuondoka hivyo kwanza anachukua fungu lake
 
Kwanini mnaingia gharama kuajiri makocha iwapo kuna mashabiki mnajua hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…