Nashauri hizi jezi za Taifa Stars zipigwe marufuku kabla ya kesho kuepuka sumu ya udini hapa nchini

Status
Not open for further replies.
Ni kukosa ubunifu.

Na ni vizuri kutoa tenda kwa ma-designer wote walete design zao na kuchaguliwa mmoja. Sio kutoa kwa mtu fulani alfu mwisho wako tunaletewa taka taka kama hii.
 
Rangi Nyeupe Ya Nini Wakati Rangi Za Taifa Zipo(brand National Colours). Ingependeza Zaidi Blue Na Njano, Nyeusi Na Kijani Au Njano Na Kijani. Huo Weupe Hauleti Maana Kitaifa
Tusikariri kuwa rangi za bendera lazima ziwepo ktk jezi.
 
Bila kupoteza muda

Kuna jezi inayosambaa mitandaoni ambayo wengi wa mashabiki wa soka haswa kutoka upande wa pili wa waislam wamelalamikia kuwa inayo alama ya msalaba......lakini mpaka sasa naona TFF wala hile kamati pendwa ya kusaidia stars kuwapiga uganda 5-0 hawajaongea kitu kutoa maelezo......

Sidhani kama ni kitu kizuri, zaidi zaidi itasaidia kuwagawa mashabiki kwenye misingi ya dini wakati timu ni yetu sote.

Na hata kama ni uzushi nadhani unastahili kupingwa maana unazidi kuzagaa mitandaoni ambako ndio habari zinasambaa haraka.

Kila la heri stars


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Propaganda Tu hizo, wakati Fulani maji ya Kilimanjaro yaligomewa kuuzwa Znz eti kwenye chupa kuna mfano wa kofia ya papa, kwamba ile michoro imewekwa purposely kueneza udini..kwamba ukiigeuza chupa upside down ile michoro inakua kama kofia nacho ona hapo ni kutaka kumpokonya deal La designing ki2pe..figisu Tu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…