Nashauri hizi jezi za Taifa Stars zipigwe marufuku kabla ya kesho kuepuka sumu ya udini hapa nchini

Nashauri hizi jezi za Taifa Stars zipigwe marufuku kabla ya kesho kuepuka sumu ya udini hapa nchini

Status
Not open for further replies.
TFF wakiwa na akili nzuri hizi jezi hazitavaliwa kamwe vinginevyo kutakuwa na viroja uwanjani kuhusu jezi hizi kutoka kwa wapenzi na mashabiki wa Taifa Stars labda wazivae ugenini.

Kiukweli naona nchi yetu imeanza kuwa tofauti na jinsi ilivyokua miaka ya nyuma, yani inafika muda watu wanatafuta pointi ndogo/kubwa kuanzisha taharuki katika jamii.

Nimepita katika mitandao ya kijamii watu wamekasirika na kutuhumu kuwa taifa linagawanywa kidini kwa sababu ya alama ya msalaba iliyo katika jezi ya timu ya taifa.

Kama nchi tumefikia hatua ya kuanza kugawana namna hii? Hii chuki imeanzia wapi maana inafikia watu wanatoa maoni kuwa kesho ni Msalaba 0- Uganda 4

Tanzania inaelekea wapi aisee?
View attachment 1052312

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata isingekua na huo msalaba jezi mbaya hiyo.sijui nani kadizaini
 
Wapumbavu tu ndio wana muda wa ku debate kuhusiana na hii jezi, hata muislamu mwenye akili zake timamu anayeijua vyema dini yake hawezi kupoteza muda kuhoji stupid stuff kama hizi, ni wale muslims wa uswahilini wenye majungu majungu ndio wanaoibua hoja za kijinga namna hii! Nonsense!
 
Wakuu habari inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ni uzembe wa TFF kuja na aina ya jezi ambayo ina msalaba ndani yake.

Suala hili si la kufanyia mzaha na linaweza kuligawa taifa pamoja na kurejesha nyuma morali na hamasa ya kuishangilia Taifa Stars.

Tanzania haina dini hivyo kuingiza alama ya dini fulani katika Taasisi ya kitaifa sio tu ni kitendo cha kizembe bali ni hatari kwa mustakbali mzima wa amani ya nchi yetu.

View attachment 1052174
Wapumbavu tu ndio wana muda wa ku debate kuhusiana na hii jezi, hata muislamu mwenye akili zake timamu anayeijua vyema dini yake hawezi kupoteza muda kuhoji stupid stuff kama hizi, ni wale waislam wa uswahilini wenye majungu majungu ndio wanaoibua hoja za kijinga namna hii! Nonsense!
 
wanahangaika nini kwa kudanganywa na wabunifu uchwara wa kibongo ? mbona sare bongo ni blue na ipo poa hadi wazungu wakija bongo ndio wanaichukulia kama vazi la taifa kuonyesha uzalendo? achilia mbali huo urembo ulio sawa na alama ya kujumlisha !!! hiyo jezi ukivaa hata ukiwa mbali huwezi kujinyambulisha kuwa wewe ni mtanzania haina mvuto wowote zaidi ya marangi mengi yasio na mpangilio. Nani kawadanganya kuwa jezi ya taifa inakuwa na madoido mengi? likine wachangiaji tuache udini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom