Nashauri magari yote ya Serikali na Taasisi za Umma yapakwe rangi za nembo zao kupunguza ukiritimba

Ukiondoa magari ya IKULU na yale ya Viongozi wa kitaifa;

Naishauri ofisi ya waziri mkuu ikiongozwa na Mh Majaliwa Kassimu kwa kushirikiana na Tamisemi chini ya Bashungwa!

Waelekeze magari yote ya serikali yapakwe rangi ya nembo ya taasisi husika kama ilivyo kwa taasisi chache kama (Polisi,Tanesco, NHC, NSSF n.k)

Na hili lisiishie tu kupaka magari ya SITE na kuacha mashangingi au magari mengine ya mameneja na wakurugenzi pasipo kuwa na rangi za nembo zao!

Ili wanainchi waone nani mharibifu, nani anakimbia mbio za hatari barabarani, nani kaenda kulewa muda wa kazi, nani yuko gesti mida ya kazi, nani kabebea mbuzi wake kwenye shangingi la serikali! N.k

Watu wa masijala wahakikishe kila chombo cha moto cha serikali kiwe na rangi za nembo husika ili kuongeza uwajibikaji na kupunguza ukilitimba.

Hili litasaidia mambo kama haya!
1. Madereva wa serikali siku hizi wamebuni mbinu ya kuwa na namba za usajili feki (fake plate number) ambazo hubandika siku za weekend na kutumia gari jambo linalochangia uchakavu wa haraka na kuighalimu serikali kufanya matengenezo

2. Madereva wanapokuwa na hayo magari yasiyo na nembo (waliyoweka feki namba binafsi) ni rahisi sana kuuza au kubadilisha vipuli orijino kwenye gereji bubu na kuitia hasara serikali
3. Matumizi ya mafuta yako juu kwasababu magari yasiyo na nembo yanashawishi mizunguko isiyokuwa ya lazima
4. Magari yasiyo na nembo hayaoneshi uwajibikaji kwa wananchi (hili lipo kisaikolojia zaidi)

Nasema hivi kwasababu nimeshuhudia mashangingi kadhaa ya serikali STL au DFPA lakini wakifika mtaani wanabandika namba binafsi mfano DZA!

Kwahiyo mtu kama huyu akiuza kipuli gereji yoyote hakuna atakaye mshitukia!
Acha wale kwa urefu wa kamba zao mkuu. Ubaya ni kwamba hata wakifuata ushauri wako, pesa zitaliwa na wajuu yao hivyo haipunguzi ugumu wa maisha kwa raia.
 
V8 likiisha badilik plate number inakua mali ya dereva,muhimu kupiga kaunda suit safiii anakula maisha mjini na watoto wazuri.
Umenichekesha sana. Zama Mkete alimkimbia Ruge kwa mtego wa aina hiii. Yule dogo pia alikua na V8 katupia kiunoni na Kabastola ka Boss wake Zama akazama mzima mzima kuja kustuka watoto wa3 kaishia kumweka jamaa Billboards ili tujue amempenda kuuuumbe ana maumivu ya karne
 
Umenichekesha sana. Zama Mkete alimkimbia Ruge kwa mtego wa aina hiii. Yule dogo pia alikua na V8 katupia kiunoni na Kabastola ka Boss wake Zama akazama mzima mzima kuja kustuka watoto wa3 kaishia kumweka jamaa Billboards ili tujue amempenda kuuuumbe ana maumivu ya karne
 
Ukiondoa magari ya IKULU na yale ya Viongozi wa kitaifa;

Naishauri ofisi ya waziri mkuu ikiongozwa na Mh Majaliwa Kassimu kwa kushirikiana na Tamisemi chini ya Bashungwa!

Waelekeze magari yote ya serikali yapakwe rangi ya nembo ya taasisi husika kama ilivyo kwa taasisi chache kama (Polisi,Tanesco, NHC, NSSF n.k)

Na hili lisiishie tu kupaka magari ya SITE na kuacha mashangingi au magari mengine ya mameneja na wakurugenzi pasipo kuwa na rangi za nembo zao!

Ili wanainchi waone nani mharibifu, nani anakimbia mbio za hatari barabarani, nani kaenda kulewa muda wa kazi, nani yuko gesti mida ya kazi, nani kabebea mbuzi wake kwenye shangingi la serikali! N.k

Watu wa masijala wahakikishe kila chombo cha moto cha serikali kiwe na rangi za nembo husika ili kuongeza uwajibikaji na kupunguza ukilitimba.

Hili litasaidia mambo kama haya!
1. Madereva wa serikali siku hizi wamebuni mbinu ya kuwa na namba za usajili feki (fake plate number) ambazo hubandika siku za weekend na kutumia gari jambo linalochangia uchakavu wa haraka na kuighalimu serikali kufanya matengenezo

2. Madereva wanapokuwa na hayo magari yasiyo na nembo (waliyoweka feki namba binafsi) ni rahisi sana kuuza au kubadilisha vipuli orijino kwenye gereji bubu na kuitia hasara serikali
3. Matumizi ya mafuta yako juu kwasababu magari yasiyo na nembo yanashawishi mizunguko isiyokuwa ya lazima
4. Magari yasiyo na nembo hayaoneshi uwajibikaji kwa wananchi (hili lipo kisaikolojia zaidi)

Nasema hivi kwasababu nimeshuhudia mashangingi kadhaa ya serikali STL au DFPA lakini wakifika mtaani wanabandika namba binafsi mfano DZA!

Kwahiyo mtu kama huyu akiuza kipuli gereji yoyote hakuna atakaye mshitukia!
UKUDA HUU na ROHO YA UCHAWI .....hayo unadhani serikali HAIYAJUWI ??

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
unaku na ukuda.hujafikiria suala la usalama. kaz hizi muda mwingine zimahitaji kutotambulika hv nikupe mfano we unafikr gar flan ikujulikana huona kama inahatarisha usalama wa wafanyakaz
unafikir watu wote wanapenda maamuz ya taasisi mbalimbal.hujafikria vizur labda kwa vile haupo huko
 
Kila gari la serikal huwa Linakuwa na namba ya usajili wa gari wa kawaida. Matumiz ya kiserikal ni mengi jombi.
hajui huyu ndio mana nilimuuliza anajua kama kila taasisi na idara huwa muda mwingine haitakiw kufahamika ili kazi ziende
anataka zikaririwe kama zile difenda na landcruiser za bluu za poti
 
UKUDA HUU na ROHO YA UCHAWI .....hayo unadhani serikali HAIYAJUWI ??

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
NJIA NI RAHISI SANA! Traffic wawe wanakagua kadi za gari hususani mashangingi na Nissan na ukikutwa umebandika namba feki kesi ya uhujumu uchumi inakuhusu, vinginevyo uhonge pesa ndefu ili polisi wakuachie
Mbwai mbwai
 
unaku na ukuda.hujafikiria suala la usalama. kaz hizi muda mwingine zimahitaji kutotambulika hv nikupe mfano we unafikr gar flan ikujulikana huona kama inahatarisha usalama wa wafanyakaz
unafikir watu wote wanapenda maamuz ya taasisi mbalimbal.hujafikria vizur labda kwa vile haupo huko
Hahahah usalama gan! Yaani gari ikiwa na nembo ndo security inaongezeka kama hujui!
Gari lenye nembo haliibiki!
Kama huamini kaibe magari ya mwendokasi au polisi!
Utetezi wa kitoto sana umeleta
 
hajui huyu ndio mana nilimuuliza anajua kama kila taasisi na idara huwa muda mwingine haitakiw kufahamika ili kazi ziende
anataka zikaririwe kama zile difenda na landcruiser za bluu za poti
Madereva naona jamaa kawagusa kunako
 
unaku na ukuda.hujafikiria suala la usalama. kaz hizi muda mwingine zimahitaji kutotambulika hv nikupe mfano we unafikr gar flan ikujulikana huona kama inahatarisha usalama wa wafanyakaz
unafikir watu wote wanapenda maamuz ya taasisi mbalimbal.hujafikria vizur labda kwa vile haupo huko
Anaogopa kugongewa au niaje
 
Back
Top Bottom