Nashauri motisha ya Rais itolewe kwa timu za taifa na siyo vilabu

Ukimsikiliza mtangazaji anapokuwa anaelezea wachezaji utasikia mara kenyan international, mara congolese international nk, yaani klabu ya kitanzania imejaa wakongoman
Uko sahihi kabisa. Ni kosa kubwa hiki kinachofanyika. Nchi zinazojitambua hauwezi kuona wanafanya kitu kama hiki. Hakuna anayejua hata klabu moja ya Senegal ila timu zao zote za taifa kuanzia za chipukizi zinaongoza kwa mataji Africa na duniani na kwenye ranking ni wa pili Afrika. Morocco ndiyo wanapiga kote kote vilabu na taifa ila sidhani kama serikali imeweka mkono wake moja kwa moja kwenye vilabu zaidi ya kuweka sera na mazingira wezeshi.

Pia nadhani kuna wachezaji wakikumbushwa wanapigania taifa lingine na siyo club wanayochezea wanaweza kukwazika. Ndiyo maana unaona baadhi ya wakongo wanapepea bendera zao uwanjani wakati wanachezea vilabu vya nje.
 
Kwa bahati mbaya kuna mambo mengi ya msingi nchi hii yanafanyika bila tafakuri ya kutosha.

Hata issue hii ya kulipia magoli niliikosoa nikasema kuna timu itakuja kulipwa pesa nyingi pamoja na kwamba imefungwa, kuna mtu akanitisha eti namsema Rais vibaya, nikamwambia kuna siku hili jambo litamuaibisha Rais ndiyo watakumbuka. Juzi nimesikia wamebadili sasa hivi watalipwa pale tu watakaposhinda.
 
Magonjwa mengine mnajitakia wenyewe asee!!.
 
Ujinga mwingine bana.... Mbona hukusema na azikuonekana Kama pesa zimapotea pale Simba anazichukua?, Hamkushangilia Simba aliposhinda gori 7×5m!. Acheni upuuzi kinachopiganiwa ni kwa manufa ya Taifa na sio wachezaji pekee Wala timu!.

Hata Simba mwaka 1993 alipocheza fainali alipewa ndege na pesa au mmesahau ndugu zangu 🤣🤣🤣
 
Fuatilia post zangu ujiridhishe kweli sikusema. Hata tukiongelea kimbinu, kutoa motisha ya magoli siyo sahihi. Ni kwamba tu watu wanaogopa Mamlaka ya Rais kwa hiyo wanashindwa kukosoa vitu kama hivi wazi wazi.
 
Fuatilia post zangu ujiridhishe kweli sikusema. Hata tukiongelea kimbinu, kutoa motisha ya magoli siyo sahihi. Ni kwamba tu watu wanaogopa Mamlaka ya Rais kwa hiyo wanashindwa kukosoa vitu kama hivi wazi wazi.
Ndio katoa basi hamia Kenya🤣
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa mpaka sasa raisi ameshatoa zaidi ya ml100 kwa simba na yanga kwenye kinunua magoli , ila hata Magufuli kuna kipindi fulani alisha wazawadia viwanja kule dodoma wachezaji wa timu ya taifa. Taifa Stars
 
Kuweka kipaumbele kwa taifa na siyo wageni wale tozo yangu, sawa?
Tukikupigia hesabu tunaweza kukuta unachotozwa ni "kiduchu" kuliko unachotumia na wewe hapo ukawa unakula tozo za watu wengine na inawezekana ni hao hao wageni usiowapenda.
 
Achia moyo ndugu yangu maana final yanga anakunja 100ml
 
Tunawekeza kwenye kuandaa timu bora za taifa ili ziletee nchi heshima ikiwemo michezo kama riadha kama ilivyo kule kenya.
Team ya taifa waliambiwa IPO 500 ml wakifuzu dk za mwisho waganda wakaweka
 
Kama vipi tuweke sheria ya idadi ya wageni wanaoruhusiwa kusajiliwa na vilabu vyetu ili tujenge timu imara ya taifa inayotokana na wachezaji wa vilabu vyetu vya ndani, ukichukulia kwamba hatuna wachezaji wengi wanaosakata kabumbu huko majuu kama walivyo nchi kama Senegal, Nigeria, Ghana nk.
 
Hiyo sheria mbona ipo. Zamani iliwekwa idadi ndogo halafu idadi ikaongezwa. Sheria ingeweka limit ya idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoweza kucheza katika mechi moja kwa pamoja badala ya kusema tu idadi ya wanaoweza kusajiliwa.
 
Hiyo sheria mbona ipo. Zamani iliwekwa idadi ndogo halafu idadi ikaongezwa. Sheria ingeweka limit ya idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoweza kucheza katika mechi moja kwa pamoja badala ya kusema tu idadi ya wanaoweza kusajiliwa.
Sahihi kabisa, inakuwa rahisi hata kutengeneza combination nzuri ya timu ya taifa.......chukulia mfano wa timu ya taifa ya spain wamejaa wachezaji wa Real Madrid na Barcelona na vile vilabu vingine vya spain.
 
Sahihi mkuu, Urais ni taasisi kwa maana ya nchi .
 
Kiongozi mwenye maono makubwa na taifa lake, mwenye uchungu na hali za wananchi wake hawezi hangaika na issues za kijinga kama hizo, ila tu ni kwa hao wanaotafuta cheap popularity
Inasikitisha hasa ukisikia taa za uwanjani zimezima tena kwa dakika takriban 40 halafu mamilioni yanatoka kwa kufunga magoli tu hata kama timu haikupata ushindi kwenye mechi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…