Dunia ya leo Kumzuia au Kumpunguzia Rais access ya Mitandao ni Kitendo cha Kipumbavu na Kisichovumilika na pia Kinakera kama kikitoka kwa Great Thinker wa JamiiForums.
Yaani mnataka Rais Mama Samia Suluhu Hassan asiwabadilishe au asiwaondoe hao Manyang'au yenu ili yaendelee Kuharibu na Kuwalinda Kiuchumi kwa Gharama ya Kuwafisadi Watanzania Wanyonge?
Tena sasa nakuambia hakuna Rais ambaye kama akiwa anapenda Kuipitia Mitandao ya Kijamii na hasa huu huu wa JamiiForums ataongoza nchi vizuri mno kama Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan.
Katika dunia ya leo kamwe huwezi Kushindana na Nguvu ya Mtandao hasa katika Suala zima la Ushawishi ndani ya nchi yoyote ile. Mbona Marais wengine wakubwa tu duniani akina Biden, Putin na Kagame wapo mno Mitandaoni tena 24/7 na nchi zao zinapiga hatua za Kimaendeleo?
Huyo Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan amekuambia huwa anakesha fully humu Mitandaoni? Acha Kumpangia cha Kufanya na kama haya Mabadiliko yamekugusa pole sana anza Kujiandaa Kisaikolojia na tambua kuwa kutesa ni kwa zamu na sasa Rais ni SSH na siyo tena Hayati JPM.