Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Kama kweli serikali ina mpango wa kuhamasisha wanazuoni wa vyuo vikuu vya Tanzania kufanya tafiti na kuchapisha maandiko katika majarida makubwa ya kimataifa, napendekeza yafuatayo:
1. Serikali itenge fedha kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi wa masters, PhD na PostDoc kila mwaka kama mataifa mengine yanavyofanya.
2. Serikali itenge fedha za kumzawadia kila mwanazuoni atakayechapisha makala kulingana na sifa ya jarida kwa kuangalia impact factor ya jarida hilo.
3. Serikali iwaajiri zaidi wanafunzi wa PostDoc kwa mkataba kushughulikia suala zima la kufanya tafiti na uchapishaji wa maandiko ili kuhakikisha vyuo vyetu vinachapisha mara kwa mara na kuendelea kubakia kwenye nafasi za juu kidunia.
4. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau andiko moja kwenye jarida lenye sifa ya kimataifa ili mwanafunzi aweze kuhitimu Masters katika vyuo vyetu.
5. Serikali iweke sharti la kuchapisha angalau makala mbili kwenye majarida yenye impact factor kubwa ili mwanafunzi aweze kuhitimu PhD katika vyuo vyetu.
Katika hili, serikali inapaswa kuwatumia zaidi wanafunzi waliofaulu vizuri katika shahada zao, yaani wenye GPA kubwa kutoka vyuo vikuu vikubwa zaidi. Wanafunzi waliofuzu vizuri ndio wenye uwezo wa kuandika zaidi na kufanya tafiti kwa sababu wanapenda kusoma.
Wahadhiri wasisitizwe zaidi kuwa wasimamizi na kuwaongoza wanafunzi katika mchakato mzima wa kufanya tafiti na kuchapisha maandiko. Katika kufanikisha hili, panahitajika ushirikiano mkubwa kati ya serikali, wahadhiri na wanafunzi.
Mwisho, naomba kuishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa suala zima la utafiti katika taifa letu.