Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Baada ya kukiri kuwa alikosea na kuomba msamaha Ndugai amezika kabisa kaheshima kadogo alichobaki nacho. Simpendi kabisa Ndugai, nadhani ni spika wa hovyo zaidi kuwahi kukalia hicho.Hapa lazima uelewe hoja ni nini
Kumpinga Rais kama kiongozi wa mhimili mwingine si jambo geni au baya.
Alichozungumza si kibaya au kigeni
Tatizo ni hili, kusingizia alinukuliwa vibaya
Kuomba msamaha kwa aliyosema kwa maana hajui alisema nini au alikusudia nini
Kuzungumzia miswada iliyopita mikononi mwake kinafiki
Kuhojiwa uwezo wake ''kiakili'' na Viongozi wote wakuu wa nchi
Heshima yake haipo kwasasa mbele ya jamii. Ajiuzulu tu
Hata hivyo kama angejipa ujasiri wa kusimamia alichokisema juzi hadharani, ningempa benefit of doubt kwani hata saa mbovu mara moja katika saa ishirini na nne husema kweli.
CCM imeiharibu sana hii nchi yetu kwa kutusukumizia viongozi wabovu moja baada ya mwingine na ilijulikana wazi kwa kila mwenye akili kwamba kuna siku tutakwama na bado.
Hili la Ndugai ni mwanzo tu na kama Watanzani hatutachukua hatua tukae tukijua tunaelekea shimoni. Kama nilivyoanza simpendi Ndugai lakini nitatetea haki yake ya kutoa maoni kama Mtanzania.
Ni bahati mbaya sana kaomba msamaha kwani amedhihirisha jinsi CCM ilivyojaa viongozi wanafiki waliopo pale tu kutetea matumbo yao hivyo hana namna bali kujiuzulu nafasi yake mara moja.