KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Niwie radhi ndugu nadhani nimechanganya mada.........Hili nalo linahusika kwenye rushwa ndugu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niwie radhi ndugu nadhani nimechanganya mada.........Hili nalo linahusika kwenye rushwa ndugu?
Vipi wanaotoa rushwa ya ngono?Ndugu wapendwa!
"Ukitaka kuokoka lazima utambue uwepo wa shetani kwanza"
Siyo kwa ubaya ukweli ni kwamba Rushwa ipo ndiyo maana tuliunda taasisi ya kupambana na rushwa!
Huwezi kupambana na kitu ambacho hakipo!
Siku moja nikiwa nafanya kazi yangu ya ufundi umeme bosi wangu akanitania kwa kuniuliza Hivi siku watu wakiacha kutumia umeme ndugu yangu utafanya kazi gani? Nikamjibu nitafanya kazi ya kuondoa umeme uliopo majumbani ambamo kuna umeme tayali!
Nikamuuliza wewe bosi unafanya kazi gani? Akanijibu TAKUKURU! Nikamuuliza bosi wangu hivi siku rushwa ikiisha nchini kwetu utafanya kazi gani ndugu? Hajawahi kunijibu hadi leo alibakia kucheka tuu!
Hivyo basi Inabidi kama taifa tubadili mbinu ya kupambana na rushwa! Siyo lazima mbinu tutakayoitumia iwe imetumika huko kwingine duniani au imeandikwa vitabuni!
Nashauri kila taasisi inayotoa huduma kwa mifumo ya kisasa ya control number! Pia kuwepo na dirisha la huduma ya haraka (fast corridors)
yaani ni hivi Mteja anapolipia huduma ya umma kwa utaratibu AWE na hiari ya kusubili kwa mujibu wa taratibu zilizopo au kama hawezi kusubiri aelekezwe dirisha la huduma ya haraka (Fast corridor or VIP corridor) ili akalipie ziada ya 45% ya malipo halisi kwa CASH palepale ofisini na apewe risiti nyingine ya huduma ya haraka!
kwa mfano! Mtu aliyelipia huduma ya kawaida ya kusubili mwezi mzima, apewe utaratibu wa haraka ndani ya siku mbili kupitia Fast service aliyolipia!
Hili litaondoa au kupunguza kabisa rushwa! Pia Litaondoa watu wa katikati katika kupata huduma!
Hayo mapato ya ndani yataisaidia taasisi kujiendesha kwa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza ndani ya taasisi ikiwemo matengenezo ya magari, ukarabati, misiba,allowance n.k
Watu wachache watakao toa rushwa inje mfumo huo wa FAST SERVICE, basi ALIYETOA NA ALIYEPOKEA wote wakamatwe ili iwe fundisho kwa wengine!
Mchawi mpe mwanao! Rushwa ni fursa ya mapato!
Waziri wa fedha na waziri wa katiba na sheria kaeni chini mnaweza kuliweka kitaalam zaidi kwasababu litakuwa jambo la hiari kama ilivyo vyombo vya usafiri (Business class & Economic class)
Haiwezekani watu wooote wenye matabaka mbalimbali kuwasubilisha kwa muda mrefu kwenye huduma za umma!
Wengine hawataki kusubili na wana hoja za msingi kutokusubili!
Mnataka watu wa namna hii waende wapi?
Hata kwenye kazi zangu za ufundi umeme na ujenzi nimeweka utaratibu kwamba kwa huduma ya kawaida tunakuhudumia mchana tu, lakini kwa dharula na haraka watu hunipigia kwa 0711756341 hata usiku wa manane umeme unapokatika na huwa ninakwenda fasta kama upepo!
Ngono haiwezi kuwa ni mali ya umma! Kwanza ni kinyume na sheria kuchungulia faragha za watu!Vipi wanaotoa rushwa ya ngono?
UTELEZI SUBSTATION KIPOCHI MANYOYA
Vipi unashauri tujengwe na tuvyumba twa aina hii ya rushwa.
Natania,
Naitwa Machepele.
Yaani kwa kifupi tafsiri ya Rushwa ni pesa ya serekali inayoingia mfukoni mwa mtu binafsi!!Rushwa ni nje ya malipo ya kawaida, yani kifupi hiyo 45% itakuwa nayo ni ya serikali, hivyo watatengeneza mazingira nao wapate chao.
Foleni gan nyingineHoja yako sio mbaya sana ila hata ukiweka hiyo fast track kuna watu watatoa tena rushwa ili wakwepe foleni pamoja na hiyo fast track. Mimi ninashauri kama nchi tuwe tu wabunifu ili uchumi ukue ambapo mishahara itapanda na kupunguza ugumu wa maisha. Rushwa kuisha ni ngumu ila kukiwa na unafuu wa maisha itapungua sana.... kwa mfano hakuna sababu ya Tanzania yenye mvua takribani 1150mm kwa mwaka kuzalisha 68000 metric tonnes za ngano wakati Saudi Arabia yenye 150mm ikizalisha 1.2million metric tonnes za ngano. Ikumbukwe Saudi hawana hata mito kama kwetu.