Nashauri Uongozi Wa Yanga SC utumie Kikosi cha Kagame Cup kumenyana na Rivers United FC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Hapa hamna timu kabisa unaweza kuta mmeikamia mechi kumbe hata madogo wa U20 wangeweza kuitafuna kirahisi. Kupangiwa kiTeam ambacho kimemaliza ligi ya Nigeria nafasi ya ni sawa na kucheza na Polisi Tanzania ya Ligi KUU Tanzania Bara.



Inaonekana hii timu imepata mbeleko ya kubeba kombe la NPFL ndio maana akapata nafasi ya ushiriki. Hebu tazama nafasi yao ya Ligi msimu ulio pita.



Yaani timu ya nafasi ya sita huko ndio tuwawekee full mkoko, Huo utakuwa 1. Uonevu 2. Matumizi mabaya ya wachezaji na 3. Sio fair play.


Na hata ushindi wao ni kuwafunda timu zilizo chini ya nafasi yake katika msimamo wa Ligi.
 
Kweli kabisa!! Pale mbele tunamuweka striker wetu hatari Waziri Junior Shentembo!!

Ni mwendo tu wa hatrick!!!
 
Anyway, hii Yanga ya msimu huu, kiukweli inaniogopesha sana! Yaani Mwalimu atakua na wakati mgumu sana wa kumpanga nani ndani, na amuache nani nje!
 
Hesabu zako, sijazielewa! Ni kweli hiyo timu, ni ya sita kwenye ligi yao. Na Polisi, ni ya sita hapa kwetu. Lakini Polisi imezidiwa pointi 38 na bingwa. Lakini wao wamezidiwa pointi 8, na bingwa. Papo hapo, wewe UTOPOLO umezidiwa pointi 9 na bingwa.
Kwa hesabu hizo, wewe uliyezidiwa pointi 9 ni nafuu kuliko aliyezidiwa pointi 8 na Mshindi?
 
Hahaha, mkuu umemaliza kila kitu.
 
Acha nadharia wewe sisi tutachapa kila mtu ata ww tarehe 25 tunaanza na wewe ndo wafuate ao mto fc
 
uzi umeishia hapa. 🤣🤣🤣
 
Manchester UTD kapitwa alama 12 na Bingwa Manchester City.

Rivers United FC kapitwa alama 8 na Bingwa Akwa United.

Unataka kuniambia kuwa Rivers United FC ya Nigeria ni timu bora zaidi kuliko Manchester UTD...(Kwasababu tu kapitwa alama chache na Bingwa)?


Mtani jiangalie Aisee! Usije ukawa umedondokewa na kitu kizito kichwani hadi ukapoteza signals.
 
uzi umeishia hapa. 🤣🤣🤣
Manchester UTD kapitwa alama 12 na Bingwa Manchester City.

Rivers United FC kapitwa alama 8 na Bingwa Akwa United.

Unataka kuniambia kuwa Rivers United FC ya Nigeria ni timu bora zaidi kuliko Manchester UTD...(Kwasababu tu kapitwa alama chache na Bingwa)?


Mtani jiangalie Aisee! Usije ukawa umedondokewa na kitu kizito kichwani hadi ukapoteza signals.
 
Mkuu, ligi yao ilikuwa ina ushindani mkubwa sana. Hiyo timu mnayoidharau, ilizidiwa pointi tatu tu, na timu ya pili. Huwezi kulinganisha na matokeo ya hapa kwetu. Yanga wajiandae vizuri tu, sio kwa kuwaaminisha kuwa wapinzani wao, ni VIBONDE!
 
Hiv kwann hii timu ya sita katika msimamo lakini inashiriki caf champion

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] umemkomesha huyu chura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…