Nashauri upinzani wafungue kesi za kupinga matokeo yote kuanzia ya udiwani mpaka urais

Nashauri upinzani wafungue kesi za kupinga matokeo yote kuanzia ya udiwani mpaka urais

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,253
Reaction score
15,748
Japo nimearifiwa kwamba matokeo ya uchaguzi wa Rais hayapingwi mahakamani, ila napendekeza wanasheria wa upinzani wafungue hiyo kesi ya kupinga hayo matokeo, tena kwa ngazi zote kuanzia udiwani.

Tunataka, kesi zipelekwe mahakamani, ili majaji na mahakimu watapozikataa, tuendelee kukusanya ushahidi wa uozo wa mfumo wetu wa demokrasia.

Huu mwaka unatakiwa ukawe wa kihistoria kwa nchi yetu, ni mwaka ambao utaamua kama Tanzania inabadilika na kuwa nchi ya kuheshimu Demokrasia au inaingia rasmi kwenye utawala wa ' Kifashisti'.

Lakini kwanza, tuhakikishe dunia inajua uovu dhidi ya demokrasia unaoendelea Tanzania.

Kesho tukaandamane, na kesi zifunguliwe kwa maelfu nchi nzima. Hatuwezi kuangalia nchi ikizama kwenye ufashisti na tutakaa kimya.

Historia itatuhukumu sana kama hatutachukua hatua kuzima huu ufashisti unaonukia mlangoni.
 
Back
Top Bottom