Nashauri wasomi wa Chuo Kikuu kujiingiza kwenye kazi ya kutafsiri movie

Lugha na uelewa wa jumla wa mambo unahitajika. Mtu mwenye difrii anafaa sana.
Lugha na uelewa wa jumla wa mambo unahitaji degree ?

Kumbuka kuna mtu anayeweka sauti, na kuna mtu anayetafsiri hao sio kwamba ni mtu mmoja wewe unaweza ukaweka maneno movie ya kichina ingawa hujui kichina.., ila sauti yako inaendana na character ya muhusika....
 
Hao kina dj muphy nk wanasimulia matukio siyo kutafsiri movie.
Watafasiri wote wa movie ni wanasimulia ...99% ya member wa JF na waliochangia hii mada Si target market ya ma DJ ndio maana humu kawaida kuina mtu anasema 'unaangaliaje movie iliyotafairiwa' Kimsingi wale wanaojua feeling ya movies hawangalii zilizotafsiriwa.

Ma DJ wakifuatisha ushauri wa mtoa mada watapoteza soko lao 99% ambao wanaangalia hizo movie za kutafairiwa.

Mtoa mada anachitaka kufanya ni kuwasilisha Business Proposal ya kuuza PIZZA na Burger buza au Mbagala Bishara ita feli vibaya sana.
 
Digrii ni kipimo kizuri cha uelewa wa Lugha( kiingereza) na uelewa wa jumla wa mambo.

Mi nazungumzia wanaotafsiri. Na kama ni project inaanza kwa hawa walioamaliza chuo basi ni vyema wakawa waingizaji wa sauti pia.
 
Angalia hii list halafu uniambie kuwa movie zilizotafsiriwa bila mbwembwe na miluzi kuwa hazina soko.

1. Neria
2.Yellow card
3. Kirikuu
4. Movie ya Yesu
5. People of the forest

Watu wanaangalia hizi za miluzi na mbwembwe kwasababu hawana alternative.
 
Mtafte DJ afro yule jamaa ni kimoda anajua vitu vingi sana na kupitia movies zame haufaidiki tu na kutafsiriwa ila utajifunza na mambo mengi ya kitaalam,kijeshi,kisayansi anayo yafafanua bila kudanganya
Tahadhari Kuna kipindi huwa anatukana
 
Digrii ni kipimo kizuri cha uelewa wa Lugha( kiingereza) na uelewa wa jumla wa mambo.

Mi nazungumzia wanaotafsiri. Na kama ni project inaanza kwa hawa walioamaliza chuo basi ni vyema wakawa waingizaji wa sauti pia.
Wewe unaelewa kiswahili vizuri na huenda pia unaelewa kisukuma..., ila its not necessary kwamba unaweza ukaweka sauti (sauti yako ina mvuto) kuweza kuweka sauti na ikapendeza...

Haya mambo yanaendana na sauti ya mtu pia (either you have it or you don't) kuna sauti za kumtoa nyoka pangoni na kuna za kumkimbiza..., huwezi ukatafsiri sauti ya jambazi na mtu katili wakati sauti yako ni kama muubiri injili...., hii kitu ni more of experience/interest na talent kuliko certificates....
 
Mi ushauri wangu umebase kwa vijana waliomaliza chuo ambao ni ngumu kuajiri watu wenye talents za kuingiza sauti.
 
Unahisia zaidi y'all uhalisia...mimi nazungumzia Biashara wewe unazungumzia Hisia zako Hisia zako wewe haziwapi kula wafanya Biashara Boss.

Hizo Movie ulizozitaja naijua hiyo kirikuu tu, na zote si mahitajio ya Soko elewa Soko ni lipi hatupo kuridhisha hisia mimi si mpenzi wa Movie za kutafsiriwa ila hapa nachambua soko lake kwasababu na mimi nilishawai kuwa Soko So najua nini nilikuwa nakipenda kipindi nilikuwa soko.
 
Hata movie ya Yesu huijui? ile nayo ilitafsiriwa, au unafikiri wale wazungu walikuwa wanaigiza kwa kiswahil! Hakuna mtu mwenye Tv aliyekuwa anakosa movie ya Yesu na movie ya Neria. Watu wanasema hwapendi movie zilizotafsiriwa lakini huwezi kuta anasema haipendi ile ya Yesu au Neria. Movie zikitafsiriwa kwa utaratibu wote wataangalia, hata wanaosem hawapendi zilizotafsiriwa.
 
Kichwa cha habari hakiendi na unayoyasema. Nahisi hoja yako ni kwamba kutafsiri kanda za sinema kunahitaji waliofuzu Chuo Kikuu, ambapo kichwa cha habari kinaashiria waliofuzu Chuo Kikuu waende kwenye kutafsiri sinema kukidhi ajira. Kichwa cha habari kinahitaji kubadilishwa kiseme unayoyatarajia.

Pamoja na hayo, hata mimi siridhiki kabisa na tafsiri ninazoziona kwenye mikanda ya sinema. Lakini wazo lako nalo naliona linakwenda mbali mno upande mwingine. Nimeona maandishi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu (ya Kiingereza na ya Kiswahili) nikastaajabu kama kweli mwandishi ana elimu ya Chuo Kikuu. Sana sana tuseme wanaotafsiri wawe wataalamu wa lugha, bila kutaja ngazi ya chuo kikuu. Naamini kabisa kwamba kuna hata Form 4 wanaoweza kufanya kazi nzuri zaidi ya tunayoiona.
 
Mkuu si kwa kila kifaa ati mtu aelezee let's say muvi mfano za huko angani mtu anaona watu wanaelea hajui nini ni nini kuna matukio yanatakiwa mtu apate details hata kidogo alasivyo kila kitu mtu atakuwa anaamini ni uongo! Hiyo ak47 nimetolea mfano tu! Unakuta Kuna siraha inapiga umbali mrefu si kawaida mtu anaweza kudhani ni muvi tu kumbe zipo kweli! Ni kama vile unagusia ila maelezo mafupi yaliyoshiba.
 
Sasa hoja naona ni Movie sio kutafsiriwa Movie ya yesu kivyovyote lazima i takeover sikwajiri imetafsiriwa kwaajiri ni ya yesu nikianza kukulistia movie zote zilizotake over za ma DJ si itafika usiku hapa.
 
Huyo kwanza aangalie behind the scenes za Animation movies za Hollywood ndio atatambua sio kila mtu anayeweza kazi hiyo, na pia sana sana wanapendelea kutumia wasanii wa movies waliobobea tayari kwa nyanja ya uigizaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…