Hivi wewe una akili kweli!!
Hakuna sababu ya kuwekwa picha yake kwenye pesa. Ikiwekwa picha yake kwenye vitabu vya kumbukumbu kuwa huyo ndiye alikuwa Rais wa kwanza mwanamke, muuaji kuliko marais wote waliowahi kutokea Afrika, mdhulumaji haki kuliko mtawala wa Taifa lolote Afrika, inatosha.
Na kila siku ya maadhimisho ya haki Duniani, taarifa ya mauaji aliyoyafanya ziwe zinasomwa Duniani kote ili kuitahadharisha Dunia, na kuhakikisha mataifa yanaweka mifumo ya kuzuia kabisa watawala dhulumati wa haki za binadamu, wa kiwango chake hawatikei tena katika Ulimwengu huu. Viongozi wabaya wa kiwango chake, wasioheshimu uhai wa binadamu wenzao, wadhulumaji wakuu wa haki za binadamu hawatokei tena. Pembeni yake ziwekwe picha za waliokuwa wasaidizi wake katika kuwaua binadamu, kuwateka na kuwatesa. Hiyo itakuwa ni kumbukumbu yenye kumfaa kutokana na matendo yake, yenye kuisaidia Dunia.