Nashindwa fanya maamuzi kati ya wanawake hawa wawili

chavka

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
223
Reaction score
46
Habari wana jamiii.

Naombeni ushauri kwa hili jambo linalonitatiza.

Nilidumu kwa muda wa miaka 9 katika ndoa yangu kabla ya kuamua kumuacha Mke wangu japo katika miaka hiyo nimeishi maisha ya aina zote yaani ya raha na ya karaha.

Siku zote nakiri na nasema mimi huenda sikuwa mume bora kwa Mzazi mwenzangu Kwani siwezi sema mapungufu yake ila huenda nimeishi kwaajili ya kimaisha sana nafikiria maendeleo sana na uzalishaji yeye alishindwa kuendana na speed yangu na hofu yangu ilikuwa ataimudu vipi familia nikiwa Sipo kabisa biashara zote kaziua na kila moja anaitolea sababu zisizo za msingi.

Nikaja kutoa barua kwa binti mwengine nikawa namlipia chakula na mahala pa kulala na maana ya Kodi nikamnunulia kiwanja kwa jina lake sikujali Mali niliompa bali nilitaka yale nilioyakosa kwa mtalaka wangu.

Ilichukua muda wa mwaka na nusu bila ya majibu ya ile posa. Na nilipouliza sikupata majibu ya msingi nilijaribu kuibembeleza ndoa lakini ikawa kama mi ndio muhitaji sana yeye hana muda huo.

Baada ya mwaka na nusu kuna siku aliniambia yuko tayaru kuolewa kwa mahari ya M2.5. Nikamwambia asijibu barua kwakuwa imesha expire nitaituma nyingine.

Nikasafiri nje ya nchi nikarudi na kununua uwanja mwengine nikaamua kujenga na yeye akawa ndio msimamizi.

Wakati najenga nikahamishiwa nje ya jiji la Dsm na kwenda kanda ya kaskazini. Mawasiliano yalianza kuyumba na mara ya mwisho tulikwazana kwa yeye kunipandishia sauti nikaamua kukata simu.

Siku iliyofuata nikampigia hakupokea akaikata. Baada ya hapo sikumtafuta wala kutaja kujua mzima au mgonjwa japo kila mwisho wa mwezi nilikuwa natuma pesa yake ya matumizi.

Ni mwanamke ambaye amezaa, ana mtoto ambate haishi naye yupo kwa mzazi mwenzie na mzazi mwenzie kaoa. Ni mwanamke niliempenda kwa dhati lakini nilipoona hana matamanio niliokuwa nayo nikaanza kumuweka pembeni katika nafsi yangu japo nimemshirikisha mambo yangu mengi na ujenzi huu mpya yeye ndio kasimamia.

Nimekuwa na mawasiliano na mwanamke mwengine ambaye nilimwambia nataka kumuoa. Sijawahi kulala naye zaidi ya mawasiliano na hapa ndio nashindwa elewa. Huyu ni mfanyakazi, hana mtoto ni mchapakazi anaonesha mapenzi kwa wanangu na ni mtu wa dini.

Nimepeleka posa kwao imejibiwa ndani ya siku mbili. Mahari yake ni ya kawaida kabida. Sasa nashindwa amua nikimfikiria yule niliyemjibu barua ime expire.

Mke niliyemuacha nilimpa nyumba mbili na viwanja viwili yeye na watoto niliozaa naye ili watoto wasipate tabu.

Huyu niliyeishi naye miaka 3 nilimnunulia kiwanja bila kumuoa na sababu za kutokumuoa ni yeye mwenyewe kuchelewa kujibu majibu ya posa japo ndio nilimpa usimamizi wa nyumba yangu niliyokuwa najenga kwa siri bila familia kujua.

Huyu wa tatu niliemposa na kurudisha majibu haraka ni mtu mhangaikaji yupo katika maisha ya kawaida ambayo hayana makuu na ni mtu wa dini.

Naombeni msaada wa mawazo kwakuwa najiona Mungu kanipa kila kitu lakini nakosa kuamua ili nipate faraja ya nafsi.
 
Oa huyu wa mwisho. Ila mali zote weka kwa jina lako. Utapata depression.
 
Mkuu unafanya kazi gani? Sio kwa majumba na viwanja hvyo ukiachilia mali sponsorship kama zote. Nitonye na mimi nikaitafute hiyo kazi
Ndugu natafuta mawazo na aaamin humu kuna watu wa fikra yakinifu.
 
Shkamoo mkubwa, mi nikushauri tuu upunguze kutumia pesa kwenye mapenzi kwa sababu hazitakufanya ujue ukweli kama wanakupenda wewe au wanapenda pesa zako..huyo wa pili ni wazi kabisa kuwa hakupendi na kuna uwezekano mkubwa yuko kwako anachuma aje kutumia na the love of her life. Na ndo maana kujibu posa yako imemchukua muda mrefu,

Chukua muda wako kumchunguza huyu wa tatu huku ukiwa unajitahidi kutokumuonesha kuwa unamhitaji/una uhitaji sana.

All the best chief
 
Mkuu usitumie pesa sana kwenye mapenzi msome tabia kabla ya kumuhakikishia maisha lingine jitahidi mali uandike jina lako maan hawa wenzetu wanaridhika kirahisi na kukuchukulia kama buzi
Shukrani
 
Ahsante ndugu
 
Nakutukana sababu vitu vingine vinauzi vinatia hasira unamnunuliaje hawara kiwanja bora angekua mke kiufupi hapo wote watatu hamna kitu ulikosea kutumia pesa sanaa kweny mapenz hapo hapendwi mtu linapendwa pochi



Pesa ni muhimu kweny mapenz ila isizidi MTU akupende wewe na hali yako anzaa upya .narudia anza upya


Au huyo wa tatu japo nae huyo sina imani ushamzoesha pesa ila huyo single mama big Noooo


Ushaur wa mwisho Fanya juu chini pokonya huyo mwanamke (hawara)kiwanja
 
Uyo wa pili alikuwa kwanza anataka ajaze kibubu ndo akuoneshe kuwa hakuitaji, wa tatu mhhhhh ujamiiani naye lakini sio bikra, yupo anayemuelewa kitandani kwa muda huo anaowapima mizani wote kwa pamoja achague yupi, cha muhimu usitumie nguvu sana Mungu anajua wako ni yupi
 
Tuliza hasira kijana pesa kwake ni kawaidana pengine ata akumbuki km alipungukiwa sehemu kisa kununua kiwanja, watu wanahonga mnooo ni vile tu labda huna ela, pesa matumizi yake ndo kama hayo bana....cha muhimu akae na uyo wa tatu amchunguze taratibu sana japo ashakurupuka kupeleka barua ya posa ndo kaja jf sa sjui itasaidiaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…