Nashindwa fanya maamuzi kati ya wanawake hawa wawili

Nashindwa fanya maamuzi kati ya wanawake hawa wawili

Ana watoto huyo angekuwa hana hata akionga nyumba sawa
Tuliza hasira kijana pesa kwake ni kawaidana pengine ata akumbuki km alipungukiwa sehemu kisa kununua kiwanja, watu wanahonga mnooo ni vile tu labda huna ela, pesa matumizi yake ndo kama hayo bana....cha muhimu akae na uyo wa tatu amchunguze taratibu sana japo ashakurupuka kupeleka barua ya posa ndo kaja jf sa sjui itasaidiaje
 
Ana watoto huyo angekuwa hana hata akionga nyumba sawa
Suala sio watoto, ye anajua akiba ya watoto iko wapi bana msimpangie alimpa akiwa na akili timamu nauhakika ndo maana adi leo anakumbuka, ila hakuna alipolalamikia alijibana, nooo alimpa akiwa na uwezo navyo
 
Nakutukana sababu vitu vingine vinauzi vinatia hasira unamnunuliaje hawara kiwanja bora angekua mke kiufupi hapo wote watatu hamna kitu ulikosea kutumia pesa sanaa kweny mapenz hapo hapendwi mtu linapendwa pochi



Pesa ni muhimu kweny mapenz ila isizidi MTU akupende wewe na hali yako anzaa upya .narudia anza upya


Au huyo wa tatu japo nae huyo sina imani ushamzoesha pesa ila huyo single mama big Noooo


Ushaur wa mwisho Fanya juu chini pokonya huyo mwanamke (hawara)kiwanja
Nashukuru kwa ushauri. Nimeelewa na ndio maana nimeona nimekwama kifikra Kwani naimani kuanza upya sio ujinga bali kujua hatua nilizopiga vibaya.
Na sikutumia pesa ili nipate kupendwa bali nilikuwa naona natimiza majukumu ila shukrani kuna mambo nayapata kwa mawazo yenu
 
Ukifeli kwenye mke wa kwanza mara nyingi huwa ndo umefeli jumla hutapata mwanamke aliekamilika duniani hayo mapungufu yake ni ya kawaida sana unajenga familia nzuri na mkeo huyo wa pili ni jini Bora umsahau kabisa kabla hujajuta wa tatu humjui bado unabahatisha
 
Tuliza hasira kijana pesa kwake ni kawaidana pengine ata akumbuki km alipungukiwa sehemu kisa kununua kiwanja, watu wanahonga mnooo ni vile tu labda huna ela, pesa matumizi yake ndo kama hayo bana....cha muhimu akae na uyo wa tatu amchunguze taratibu sana japo ashakurupuka kupeleka barua ya posa ndo kaja jf sa sjui itasaidiaje
Kuposa sio kuoa ndio maana natafuta uyakini wa matendo yangu kabla sijaumia zaidi
 
Fanya vyote ila kumbuka ujana una mwisho. Hizo mali unazo wagawia wanawake ndio msaada wako wa uzeeni .Ridhika ,kamwe uwezi iridhisha nafsi .
Nashukuru kwa ukumbusho na nashukuru kwa Mungu nimewekeza huko kwenye uzee
 
I see wewe jamaa pamoja na kwamba unataka ushauri,lakini kipato chako unakitumia vibaya sana. Unajihisi miaka yote utakuwa kwenye pepo ya hela,bila kujua mambo huwa yanabadirika,tena huwa yanabadirika haraka sana. Kwa mtindo wako ukimuona tu mwanamke unaanza kumgawia mali kwa kumjengea kwa haraka tu bila sababu ili mradi tu ni mpenzi wako. Hata kama una hela zimejaa magunia lakini si kwa matumizi ya kijinga namna hiyo. MUNGU huwa anaona,amekupa wewe,wapo wenye uhitaji wengi,shukuru,kitumie vizuri. (Hata kama una hela lakini kikubwa wewe ni limbukeni wa mapenzi). Cha kufanya sasa,kama hakuna tatizo kubwa kati yenu na yule uliezaa nae wa kwanza mrudie huyo ishi nae. Kama unaona si lazima huyo basi muoe huyu wa sasa. Ila huyo wa pili uliemjengea bila sababu huyo umempa tu sadaka. Hakikisha unakuwa na mke wako huko ulikohamia.
 
Ukifeli kwenye mke wa kwanza mara nyingi huwa ndo umefeli jumla hutapata mwanamke aliekamilika duniani hayo mapungufu yake ni ya kawaida sana unajenga familia nzuri na mkeo huyo wa pili ni jini Bora umsahau kabisa kabla hujajuta wa tatu humjui bado unabahatisha
Shukrani ndugu na ndio maana najiuliza wapi nitakuwa sahihi.
 
I see wewe jamaa pamoja na kwamba unataka ushauri,lakini kipato chako unakitumia vibaya sana. Unajihisi miaka yote utakuwa kwenye pepo ya hela,bila kujua mambo huwa yanabadirika,tena huwa yanabadirika haraka sana. Kwa mtindo wako ukimuona tu mwanamke unaanza kumgawia mali kwa kumjengea kwa haraka tu bila sababu ili mradi tu ni mpenzi wako. Hata kama una hela zimejaa magunia lakini si kwa matumizi ya kijinga namna hiyo. MUNGU huwa anaona,amekupa wewe,wapo wenye uhitaji wengi,shukuru,kitumie vizuri. (Hata kama una hela lakini kikubwa wewe ni limbukeni wa mapenzi). Cha kufanya sasa,kama hakuna tatizo kubwa kati yenu na yule uliezaa nae wa kwanza mrudie huyo ishi nae. Kama unaona si lazima huyo basi muoe huyu wa sasa. Ila huyo wa pili uliemjengea bila sababu huyo umempa tu sadaka. Hakikisha unakuwa na mke wako huko ulikohamia.
Shukrani kwa ushauri. Hakuna aliekamilika ndio maana nimekujaomba ushauri. Labda nikweli mshamba ndio maana nilifanya yote hayo. Ila sikuwa na fikra ya hayo niliona natimiza majukumu. Huyo wa pili sijamjengea ni kiwanja tu.
Na naimani kama ningekuwa na usahihi basi huko kutumia vibaya kipato nisingekuwanako
 
Mke mwema hutoka kwa Mungu

tuliza boli maana kwa speed unayoenda nayo huenda ukaopoa tena bonge la fafa

Pesa ndio kila kitu;lakini sio kwa kila ki2..hasa ktk kumpata mwenza wa maisha wa raha na shida
 
Kikubwa jitaidi sana kufanya mambo yako wewe mwenyewe, usiwe mtu wa kushirikisha wapenzi katika mambo unayofanya, pia jitaidi kuwa karibu na Muumba wako mana yeye ndo mfariji wa mwisho na awezaye kukupa mwenza sahihi wa maisha yako yote.Mkalibie Mungu, wengine tuliachwa na wake zetu baada ya kutumbuliwa na tumezaa nao watoto wakutosha, hapo ndo utajua kuwa pesa ndo ilikuwa inasimamia mji.

Tafuta mwanamke anayeweza kulea watoto wako na kukulea wewe pia. Ukipata anaejue kulea mwili wake pekee utajuta pamoja na kuwa na kila kitu .
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Uyo wa pili alikuwa kwanza anataka ajaze kibubu ndo akuoneshe kuwa hakuitaji, wa tatu mhhhhh ujamiiani naye lakini sio bikra, yupo anayemuelewa kitandani kwa muda huo anaowapima mizani wote kwa pamoja achague yupi, cha muhimu usitumie nguvu sana Mungu anajua wako ni yupi
Kwamba Kuna ambae Yuko vizuri kitandani
 
Hongra kwa kuwa na kipato kizur

Mengne nawaachia wakuu wakushaur
Naunga mkono hoja, hongera zake kwa kutapanya mali, kanikumbusha kisa cha kwenye biblia, mwana mpotevu, aliyetapanya mali zake kisha akafikia uamuzi wa kurudi kwa baba'ke baada ya mali kuisha. Wengine wamshauri tu.
 
Kwa maelezo yako unampenda sana wa pili.Ila wa tatu ndio anaonekana bora kwako japo unahitaji muda wa kutosha kumfahamu vyema.All in all hizi zote blah blah cha msingi sikiliza moyo wako unataka nini.
 
Kuposa sio kuoa ndio maana natafuta uyakini wa matendo yangu kabla sijaumia zaidi
Basi kumbe ata mimi naweza kupata chance nsikate tamaa😛😛😛😛 cha muhimu usiwe na araka Mungu ni wetu sote ila pia jitafakari mama watoto alikosa nn na kuamua kuondoka, sio rahisi sana mwanamke bila sababu na watoto wake aamue kutengana na baba wa watoto, na je uyo wa pili alisoma nini akaamua kubadilika??? Labda kuna vitu vilimdisapoint na kumkatisha tamaa ya kutamani safari ya maisha na wewe
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Kwamba Kuna ambae Yuko vizuri kitandani
Asa unafikiri mwanamke kabisa mtu mzima nakutana na mwanaume eti anifanyi adi anioe, wakati huo tunachunguzana labda ndani ya mwaka mzima ni nini kinafanyika?????
 
Upendo pekee hausababishi Ndoa.
Oa mwanamke atakaye simama na wewe katika hali zote, bila kusahau mwenye utayari wa kutimiza ndoto zako na kinyume chake. (Na wewe timiza ndoto zake pia)
 
Back
Top Bottom