Nashindwa fanya maamuzi kati ya wanawake hawa wawili

Hongera sana, huyu wa tatu ndio mke sasa.
Kama una majigambo, kauli za kujikweza au dharau jaribu kuziacha.

Baadhi ya wanaume wenye fedha hujiinua mpaka juu mawinguni na kukosa kauli kwa wake zao.
 
Habari wana jamiii. Naombeni ushauri kwa hili
Nilidumu kwa muda wa miaka 9 katika ndoa yangu kabla ya kuamua kumuacha Mke wangu japo katika miaka hiyo nimeishi maisha ya aina zote namaana raha na karaha. Siku zote nakiri na nasema mm huenda sikuwa mume bora kwa Mzazi mwenzangu. Kwani siwezi sema mapungufu yake ila huenda nimeishi kwaajili ya kimaisha sana nafikiria maendeleo sana na uzalishaji yy alishindwa kuendana na speed yangu na hofu yangu ilikuwa ataimudu vipi familia nikiwa Sipo kabisa. Kama biashara zote kaziua na kila moja anaitolea sababu zisizo za msingi.
Nikaja kutoa barua kwa binti mwengine nikawa namlipia chakula na mahala pa kulala na maana ya Kodi nikamnunulia kiwanja kwa jina lake sikujali Mali niliompa bali nilitaka yale nilioyakosa kwa mtalaka wangu. Ilichukua muda wa mwaka na nusu bila ya majibu ya ile posa. Na nilipouliza sikupata majibu ya msingi nilijaribu kuibembeleza ndoa lkn ikawa kama mm ndio muhitaji sana yy hana muda huo. Baada ya mwaka na nusu kunasiku aliniambia yuko teyari kuolewa kwa mahari ya M2.5 nikamwambia asijibu barua kwakuwa imesha expire nitaituma nyengine. Nikasafiri nje ya nchi Nilirudi na kununua uwanja mwengine nikaamua kujenga na yy ndio msimamizi wakati najenga nikaamishwa nje ya jiji la Dsm na kwenda kanda ya kaskazini. Mawasiliano yalianza kuyumba na mara ya mwisho tulikwazana kwa yeye kunipandishia sauti nikaamua kukata cm siku iliofata nikampigia hakupokea akaikata. Baada ya hapo sikumtafuta wala kutaja kujua mzima au mgonjwa japo kila mwisho wa mwezi nilikuwa na tuma pesa yake ya matumizi. Ni mwanamke ambae amezaa anamtoto ambae haishinae yupo kwa mzazi mwenzie na mzazi mwenzie kaoa. Ni mwanamke niliempenda kwa dhati lkn nilipoona hana matamanio niliokuwanayo nikaanza kumuweka pembeni katika nafsi yangu. Japo nimemshirikisha mambo yangu mengi na ujenzi huu mpya yy ndio kasimamia. Nimekuwa na mawasiliano na mwanamke mwengine ambae nilimwambia nataka kumuoa sijawahi kulalanae zaidi ya mawasiliano hapa ndio nashindwa elewa huyu ni mfanyakazi hana mtoto ni mchapakazi anaonyesha mapenzi kwa wanangu na ni mtu wa dini. Nimepeleka posa kwao imejibiwa ndani ya siku mbili. Mahari yake niyakawaida nashindwa amua nikimfikiria yule niliomjibu barua ime expire.

Nashindwa kuamua.
Mke nilie muacha nilimpa nyumba mbili na viwanja viwili yy na watoto niliozaanae ili watoto wasipate tabu.

Huyu nilieishinae miaka 3 nilimnunulia kiwanja bila kumuoa na sababu za kutokumuoa ni yy mwenyewe kuchelewa kujibu majibu ya posa japo ndio nilimpa usimamizi wa nyumba yangu nilikuwa najenga kwa siri bila familia kujua.

Huyu wa tatu niliemposa na kurudisha majibu haraka ni mtu mwangaikaji yupo katika maisha ya kawaida ambayo hana makuu na mtu wa dini sijawahi kujamii yananae. Anajua kama nina watoto

Naombeni msaada wa mawazo kwakuwa najiona Mungu kanipa kila kitu lkn nakosa kuamua ili nipate faraja ya nafsi

Kama hadithi yako ni ya kweli basi una mapepo
 
Upendo pekee hausababishi Ndoa.
Oa mwanamke atakaye simama na wewe katika hali zote, bila kusahau mwenye utayari wa kutimiza ndoto zako na kinyume chake. (Na wewe timiza ndoto zake pia)
Na bila upendo hayo yote hayataweza kuwepo kati ya wawili hao
 
Ila ninachokiwaza ni namna uyo mama watoto wa miaka 9 akaondoka, wa pili nafikiri akakusoma akajitoa kijanja bila kukutamkia, kuna mahali unatakiwa kujitafakari nadhani
 
Shukrani kwa ushauri. Hakuna aliekamilika ndio maana nimekujaomba ushauri. Labda nikweli mshamba ndio maana nilifanya yote hayo. Ila sikuwa na fikra ya hayo niliona natimiza majukumu. Huyo wa pili sijamjengea ni kiwanja tu.
Na naimani kama ningekuwa na usahihi basi huko kutumia vibaya kipato nisingekuwanako
Sorry kwa pale nilipotumia lugha kali unisamehe. Nimeongea na wewe kama naongea na wewe ana kwa ana. Ni vile nimeenda mbali sana nimefikiria vijana wanavyopotea,kama vile story yako haitofautiana sana wale wanaowekeza kuwasomesha wanawake mwisho anaishia nyuma ya nondo. Mwisho ksbb unakuwa una nia ya kuoa kwa nini uwekeze kwa kumnunua vyake peke yake? Nunua kama vyako,andika jina lako simamia ujenzi wewe mwenyewe au ndugu yako unaemwamini
 
Japo halinihusu mzee kuwa mbinafsi kwenye Mali zako usitumie pesa roughly hivyo mwisho wa mchezo tutakucheka utakapo kosa kitu na wote hao watakukimbia na kukuacha na kende zako
 
Chukua huyo uliyempa usimamizi wa nyumba ili baadae akufurahishe vizuri..

Wanaume bwana
 
Habari wana jamiii. Naombeni ushauri kwa hili
Nilidumu kwa muda wa miaka 9 katika ndoa yangu kabla ya kuamua kumuacha Mke wangu japo katika miaka hiyo nimeishi maisha ya aina zote namaana raha na karaha. Siku zote nakiri na nasema mm huenda sikuwa mume bora kwa Mzazi mwenzangu. Kwani siwezi sema mapungufu yake ila huenda nimeishi kwaajili ya kimaisha sana nafikiria maendeleo sana na uzalishaji yy alishindwa kuendana na speed yangu na hofu yangu ilikuwa ataimudu vipi familia nikiwa Sipo kabisa. Kama biashara zote kaziua na kila moja anaitolea sababu zisizo za msingi.
Nikaja kutoa barua kwa binti mwengine nikawa namlipia chakula na mahala pa kulala na maana ya Kodi nikamnunulia kiwanja kwa jina lake sikujali Mali niliompa bali nilitaka yale nilioyakosa kwa mtalaka wangu. Ilichukua muda wa mwaka na nusu bila ya majibu ya ile posa. Na nilipouliza sikupata majibu ya msingi nilijaribu kuibembeleza ndoa lkn ikawa kama mm ndio muhitaji sana yy hana muda huo. Baada ya mwaka na nusu kunasiku aliniambia yuko teyari kuolewa kwa mahari ya M2.5 nikamwambia asijibu barua kwakuwa imesha expire nitaituma nyengine. Nikasafiri nje ya nchi Nilirudi na kununua uwanja mwengine nikaamua kujenga na yy ndio msimamizi wakati najenga nikaamishwa nje ya jiji la Dsm na kwenda kanda ya kaskazini. Mawasiliano yalianza kuyumba na mara ya mwisho tulikwazana kwa yeye kunipandishia sauti nikaamua kukata cm siku iliofata nikampigia hakupokea akaikata. Baada ya hapo sikumtafuta wala kutaja kujua mzima au mgonjwa japo kila mwisho wa mwezi nilikuwa na tuma pesa yake ya matumizi. Ni mwanamke ambae amezaa anamtoto ambae haishinae yupo kwa mzazi mwenzie na mzazi mwenzie kaoa. Ni mwanamke niliempenda kwa dhati lkn nilipoona hana matamanio niliokuwanayo nikaanza kumuweka pembeni katika nafsi yangu. Japo nimemshirikisha mambo yangu mengi na ujenzi huu mpya yy ndio kasimamia. Nimekuwa na mawasiliano na mwanamke mwengine ambae nilimwambia nataka kumuoa sijawahi kulalanae zaidi ya mawasiliano hapa ndio nashindwa elewa huyu ni mfanyakazi hana mtoto ni mchapakazi anaonyesha mapenzi kwa wanangu na ni mtu wa dini. Nimepeleka posa kwao imejibiwa ndani ya siku mbili. Mahari yake niyakawaida nashindwa amua nikimfikiria yule niliomjibu barua ime expire.

Nashindwa kuamua.
Mke nilie muacha nilimpa nyumba mbili na viwanja viwili yy na watoto niliozaanae ili watoto wasipate tabu.

Huyu nilieishinae miaka 3 nilimnunulia kiwanja bila kumuoa na sababu za kutokumuoa ni yy mwenyewe kuchelewa kujibu majibu ya posa japo ndio nilimpa usimamizi wa nyumba yangu nilikuwa najenga kwa siri bila familia kujua.

Huyu wa tatu niliemposa na kurudisha majibu haraka ni mtu mwangaikaji yupo katika maisha ya kawaida ambayo hana makuu na mtu wa dini sijawahi kujamii yananae. Anajua kama nina watoto

Naombeni msaada wa mawazo kwakuwa najiona Mungu kanipa kila kitu lkn nakosa kuamua ili nipate faraja ya nafsi
Changamoto kubwa inayokusababishia haya yote ni kwamba unatumia fedha nyingi kujustify love something which is difficult ndio maana umekuwa unapata changamoto kujua yupi ana real love and yupi ana fake love and she is after money!
 
Shukrani sana ndugu zangu kiukweli nimepata unafuu mkubwa kiakili kwa mawazo yenu. Na namuomba Mungu nisimame kwenye njia ilio sahihi kama mnavyonipa mawazo.

Na kiukweli nimejikuta naona nilivyo wapunja hata wanangu kwa kutoa kiwanja ambacho kama ningekuwa muulizaji tangu mwanzo basi ingekuwa ni milki yao.

Nilikuwa mshirikishaji kwao nikiamini tunajenga nguzo moja na sio nguzo tofauti na mm binafsi sikuweza kuwa msimamizi kwakuwa kazi yangu sio ya mji mmoja ni mtu wa kusafiri sana. Kwahiyo imani yangu ya kuona hiki chetu na sio changu. Ndio ilionifikisha hapa.

Kubwa nashukuru kwa kila alienipa ushauri na nazidi kupokea ushauri Mungu awabariki sana.
 
Sorry kwa pale nilipotumia lugha kali unisamehe. Nimeongea na wewe kama naongea na wewe ana kwa ana. Ni vile nimeenda mbali sana nimefikiria vijana wanavyopotea,kama vile story yako haitofautiana sana wale wanaowekeza kuwasomesha wanawake mwisho anaishia nyuma ya nondo. Mwisho ksbb unakuwa una nia ya kuoa kwa nini uwekeze kwa kumnunua vyake peke yake? Nunua kama vyako,andika jina lako simamia ujenzi wewe mwenyewe au ndugu yako unaemwamini
Nilikuelewa ndugu na huwa naheshimu mawazo yamtu nikijua natakiwa kujifunza na sio kuhamaki.
 
Asa unafikiri mwanamke kabisa mtu mzima nakutana na mwanaume eti anifanyi adi anioe, wakati huo tunachunguzana labda ndani ya mwaka mzima ni nini kinafanyika?????
Nimefurahi japo sio vya kufurahi tatizo nipo mji tofauti na yy na nimtumishi japo ni shirika binafsi
 
Ila ninachokiwaza ni namna uyo mama watoto wa miaka 9 akaondoka, wa pili nafikiri akakusoma akajitoa kijanja bila kukutamkia, kuna mahali unatakiwa kujitafakari nadhani
Miaka 9 nimingi kukaa na mwenza na kwahekima ya ndoa nilikaa vikao vyakukanyana na Kunakipindi nilimrudisha kwao kwa miezi 6. Nilitaraji akirudi atatambua na kujua namna ya kuishi na majukumu ya familia na sio ukoo.
Lkn sikuwa nimetibu bali niliongeza shida. Ndipo nikamuacha
 
Kwa maelezo yako unampenda sana wa pili.Ila wa tatu ndio anaonekana bora kwako japo unahitaji muda wa kutosha kumfahamu vyema.All in all hizi zote blah blah cha msingi sikiliza moyo wako unataka nini.
Shukrani huwenda ni huruma niliokuwanayo namuonea kulingana na Historia yake. Nikaona kumfanyia wema ndio njia sahihi ya kumtoa alipo. Nikihisi mateso na misukosuko aliopitia nikaona anastahiki kufanyiwa wema. Kwakuwa Historia yake haikuachana mbali sana na yangu kwamba wote tulipoteza wazazi wetu wa kiume kipindi cha kati ya ukuwaji manyanyaso na misukosuko baada ya vivo vyao.

Nikaona mm mwanaume nimepambana na ninaendelea kupambana ila yy mtoto wa kike anatakiwa huruma. Nikiwa na fikra ikiwa ni mwangu au dada yangu.

Ila nashukuru Umenipa ushauri mwema
 
Naunga mkono hoja, hongera zake kwa kutapanya mali, kanikumbusha kisa cha kwenye biblia, mwana mpotevu, aliyetapanya mali zake kisha akafikia uamuzi wa kurudi kwa baba'ke baada ya mali kuisha. Wengine wamshauri tu.
Shukrani kwa kunipa ukumbusho naimani hakuna anaependa kupotea Mungu atuongoze sote tusipotee
 
Nimefurahi japo sio vya kufurahi tatizo nipo mji tofauti na yy na nimtumishi japo ni shirika binafsi
Kila la heri.....kuna wenzio wanatumia wanatumia taratibu maana kabla ya wewe alikuwepo ingawa tunapendaga kusema alikuwepo 😀 😀 😀 😀 unaendelea kushika pembe uku tumekuweka kwenye probation
 
Miaka 9 nimingi kukaa na mwenza na kwahekima ya ndoa nilikaa vikao vyakukanyana na Kunakipindi nilimrudisha kwao kwa miezi 6. Nilitaraji akirudi atatambua na kujua namna ya kuishi na majukumu ya familia na sio ukoo.
Lkn sikuwa nimetibu bali niliongeza shida. Ndipo nikamuacha
Unampa mwanamke miezi 6 ya kukaa mwenyewe kwao badala wewe ndo uwe karibu naye ktk kumwelewesha na kumshape vile unataka awe?? Kwa mimi ata nsingerudi maana dah hahahahaaaa sema wanaume mnalazimishaga wanawake kuonekana wakosaji ata km wewe ndo mwenye mapungufu
 
Changamoto kubwa inayokusababishia haya yote ni kwamba unatumia fedha nyingi kujustify love something which is difficult ndio maana umekuwa unapata changamoto kujua yupi ana real love and yupi ana fake love and she is after money!
Na pengine yeye hana ushawishi mkubwa wa mapenzi ili wampende na sio kupenda alichonacho he is just thinking money can do everything
 
Shukrani sana ndugu zangu kiukweli nimepata unafuu mkubwa kiakili kwa mawazo yenu. Na namuomba Mungu nisimame kwenye njia ilio sahihi kama mnavyonipa mawazo.

Na kiukweli nimejikuta naona nilivyo wapunja hata wanangu kwa kutoa kiwanja ambacho kama ningekuwa muulizaji tangu mwanzo basi ingekuwa ni milki yao.

Nilikuwa mshirikishaji kwao nikiamini tunajenga nguzo moja na sio nguzo tofauti na mm binafsi sikuweza kuwa msimamizi kwakuwa kazi yangu sio ya mji mmoja ni mtu wa kusafiri sana. Kwahiyo imani yangu ya kuona hiki chetu na sio changu. Ndio ilionifikisha hapa.

Kubwa nashukuru kwa kila alienipa ushauri na nazidi kupokea ushauri Mungu awabariki sana.
Come on man....huwezi wekeza kwa ajili ya wawili na mpenz tu ambaye hajawa mke, ni kweli hukupata wazo km hilo kwa vile mapenzi ndo yalikuwa yanasimamia kila maamuzi yako
 
Back
Top Bottom