Nashindwa fanya maamuzi kati ya wanawake hawa wawili

Nashindwa fanya maamuzi kati ya wanawake hawa wawili

Nimefurahi japo sio vya kufurahi tatizo nipo mji tofauti na yy na nimtumishi japo ni shirika binafsi
Mi mwenyewe niko apa natamani nikupate ila usinipe chochote zaidi yazile care za mwanaume kwa mwanamke 😉 😉 😉 😛 😛 😛 hautojutia
 
Mi mwenyewe niko apa natamani nikupate ila usinipe chochote zaidi yazile care za mwanaume kwa mwanamke 😉 😉 😉 [emoji14] [emoji14] [emoji14] hautojutia
Mwongaji mzuri sana pesa zako ziko nje nje hongera
 
Sababu za kumuacha mke wako wa kwanza in nyepesi Sana. Ni Kama ilikuwa unamtafutia sababu ya kumuacha. Biashara watu Kila siku zinafungwa ndo umuache mke wako wa ndoa sababu kaua biashara hapohapo wewe unahonga viwanja?acha hizo mrudie mke wa Kwanza umuombe msamaha.
 
Ndio huyu huyu uliekuwa humuelewi au ulioa mwingine, bila shaka jichunguze huenda kosa lipo kwako nimefatilia thread zako...
 
Na pengine yeye hana ushawishi mkubwa wa mapenzi ili wampende na sio kupenda alichonacho he is just thinking money can do everything
Dada pesa hainunui kila kitu na sijapenda kupoteza Mke niliezaanae na sijasema yy mkosefu na sitosema hilo. Tungekuwa tuna mwaka mmoja sawa lkn ni miaka.

Na ningekuwa nahisi pesa ni kila kitu tunakutana na madadapoa wengi kwenye kazi zetu ndani na nje ya nchi lkn siko interest na wao. Tena dadapoa unalala nae gharama ni pesa ya muda huo tu hana gharama nyengine.

Nahitaji kuishi na sio kuigiza kuishi.
 
Suala sio watoto, ye anajua akiba ya watoto iko wapi bana msimpangie alimpa akiwa na akili timamu nauhakika ndo maana adi leo anakumbuka, ila hakuna alipolalamikia alijibana, nooo alimpa akiwa na uwezo navyo
Wewe utakua ni mhongwaji mahiri sana maana sio kwa utetezi huu
 
Kuna ule wimbo wazee waliimba .. “usitumiee pesaaa kama fimbo babaa, mambo ya pesa mpaka makubaliano hapo pesa huwa na thamani eehh
 
Dada pesa hainunui kila kitu na sijapenda kupoteza Mke niliezaanae na sijasema yy mkosefu na sitosema hilo. Tungekuwa tuna mwaka mmoja sawa lkn ni miaka.

Na ningekuwa nahisi pesa ni kila kitu tunakutana na madadapoa wengi kwenye kazi zetu ndani na nje ya nchi lkn siko interest na wao. Tena dadapoa unalala nae gharama ni pesa ya muda huo tu hana gharama nyengine.

Nahitaji kuishi na sio kuigiza kuishi.
You sounds like a real man nimekuwa nikimuota manengelo njoo saidia mm
 
Habari wana jamiii.

Naombeni ushauri kwa hili jambo linalonitatiza.

Nilidumu kwa muda wa miaka 9 katika ndoa yangu kabla ya kuamua kumuacha Mke wangu japo katika miaka hiyo nimeishi maisha ya aina zote yaani ya raha na ya karaha.

Siku zote nakiri na nasema mimi huenda sikuwa mume bora kwa Mzazi mwenzangu Kwani siwezi sema mapungufu yake ila huenda nimeishi kwaajili ya kimaisha sana nafikiria maendeleo sana na uzalishaji yeye alishindwa kuendana na speed yangu na hofu yangu ilikuwa ataimudu vipi familia nikiwa Sipo kabisa biashara zote kaziua na kila moja anaitolea sababu zisizo za msingi.

Nikaja kutoa barua kwa binti mwengine nikawa namlipia chakula na mahala pa kulala na maana ya Kodi nikamnunulia kiwanja kwa jina lake sikujali Mali niliompa bali nilitaka yale nilioyakosa kwa mtalaka wangu.

Ilichukua muda wa mwaka na nusu bila ya majibu ya ile posa. Na nilipouliza sikupata majibu ya msingi nilijaribu kuibembeleza ndoa lakini ikawa kama mi ndio muhitaji sana yeye hana muda huo.

Baada ya mwaka na nusu kuna siku aliniambia yuko tayaru kuolewa kwa mahari ya M2.5. Nikamwambia asijibu barua kwakuwa imesha expire nitaituma nyingine.

Nikasafiri nje ya nchi nikarudi na kununua uwanja mwengine nikaamua kujenga na yeye akawa ndio msimamizi.

Wakati najenga nikahamishiwa nje ya jiji la Dsm na kwenda kanda ya kaskazini. Mawasiliano yalianza kuyumba na mara ya mwisho tulikwazana kwa yeye kunipandishia sauti nikaamua kukata simu.

Siku iliyofuata nikampigia hakupokea akaikata. Baada ya hapo sikumtafuta wala kutaja kujua mzima au mgonjwa japo kila mwisho wa mwezi nilikuwa natuma pesa yake ya matumizi.

Ni mwanamke ambaye amezaa, ana mtoto ambate haishi naye yupo kwa mzazi mwenzie na mzazi mwenzie kaoa. Ni mwanamke niliempenda kwa dhati lakini nilipoona hana matamanio niliokuwa nayo nikaanza kumuweka pembeni katika nafsi yangu japo nimemshirikisha mambo yangu mengi na ujenzi huu mpya yeye ndio kasimamia.

Nimekuwa na mawasiliano na mwanamke mwengine ambaye nilimwambia nataka kumuoa. Sijawahi kulala naye zaidi ya mawasiliano na hapa ndio nashindwa elewa. Huyu ni mfanyakazi, hana mtoto ni mchapakazi anaonesha mapenzi kwa wanangu na ni mtu wa dini.

Nimepeleka posa kwao imejibiwa ndani ya siku mbili. Mahari yake ni ya kawaida kabida. Sasa nashindwa amua nikimfikiria yule niliyemjibu barua ime expire.

Mke niliyemuacha nilimpa nyumba mbili na viwanja viwili yeye na watoto niliozaa naye ili watoto wasipate tabu.

Huyu niliyeishi naye miaka 3 nilimnunulia kiwanja bila kumuoa na sababu za kutokumuoa ni yeye mwenyewe kuchelewa kujibu majibu ya posa japo ndio nilimpa usimamizi wa nyumba yangu niliyokuwa najenga kwa siri bila familia kujua.

Huyu wa tatu niliemposa na kurudisha majibu haraka ni mtu mhangaikaji yupo katika maisha ya kawaida ambayo hayana makuu na ni mtu wa dini.

Naombeni msaada wa mawazo kwakuwa najiona Mungu kanipa kila kitu lakini nakosa kuamua ili nipate faraja ya nafsi.

Wa dini ni muhimu sana katika nyakati hizi
Umefanya vema kutokujamiiana nae
Ili
Moja upime
Pili utajenga uaminifu kwake kwamba huendekezi tamaa za ngono
Tatu hata ukisafiri hawezi kukuwazia mambo ya ngono maana ulivumilia

Nne atakuombea mafanikio popote uendapo


Huyo mwenye mtoto kumbuka atakuwa hamsini hamsini maana nae alishatendwa na mtaachana tu maana hataishi kukunung’unikia
 
Rudiana na mke wako tu mzee kama umeweza kuishi naye miaka 9 unashindwaje kuvumilia vitu vidogo vidogo usikate tamaa rudiana na mzazi mwenzio mlee watt vzr tu huku kwengine utapoteza muda tu.
 
Labda hujiamin kwenye mapenzi, labda unapenda sana, au unaangalia uzuri zaidi kuliko tabia ila uyo wa tatu jaribu kuteka hisia zake zaidi kabla ya kuanza kuishi naye na jaribu kumjua zaidi kiundani kabla ya kuishi naye
 
Back
Top Bottom