Nashindwa kuelewa tukio hili ambalo nimekutana nao

Nashindwa kuelewa tukio hili ambalo nimekutana nao

Nkuulze umesema akizinduka uko kaburini ataishiwa pumzi na atakufa, kwani muda huo kazikwa niseme watu wamekaa msibani siku tatu kwamba muda wote wa siku tatu anaweza kusurvive bila pumzi uko chini?, pls make it make sense nielewe.
Ndio anaweza moyo wake unakuwa unatumia energy ndogo mnoo kiufupi anakuwa nusu mfu hata damu huanza kuganda kwa mbalii
 
Hua wanawaficha wapi wasiweze kuonekana kabisa na binadamu wengine?Hiyo misukule anaiukuaje kwa kufukua kile kifusi au Kuna njia mbadala wanatumia?
Anafukua kabisa kifusi, wala hakuna njia nyingne anayofanya zaidi ya kufukua kabuli zima na kumtoa kisha kulifukia tena, kwan hujawah kuskia watu wameenda kufukua kaburi wamelikuta tupu marehemu hayupo ? Nadhani umeanza kuelewa huo mchezo.
 
Anafukua kabisa kifusi, wala hakuna njia nyingne anayofanya zaidi ya kufukua kabuli zima na kumtoa kisha kulifukia tena, kwan hujawah kuskia watu wameenda kufukua kaburi wamelikuta tupu marehemu hayupo ? Nadhani umeanza kuelewa huo mchezo.
kama ni hvi, itabdi tuanze kuzika kwa zege na siment kali.

Na ingetakiwa dawa ya kukata ile sumu iwepo, ili mtu akifa kwa utata, tumpake kujihakikishia kifo chake cha kweli au mchongo?

Sema kuna wachawi wengne wanaweza kuja kukuteka na kukupoteza au wanakusubiria njian wanakukamata na kukufanya usionekane kwa watu.
Kisha wanatengeneza kifo cha mchongo.
Hao nao kinga kali inatakiwa ya mwili na kiroho.
 
Anafukua kabisa kifusi, wala hakuna njia nyingne anayofanya zaidi ya kufukua kabuli zima na kumtoa kisha kulifukia tena, kwan hujawah kuskia watu wameenda kufukua kaburi wamelikuta tupu marehemu hayupo ? Nadhani umeanza kuelewa huo mchezo.
Vipi misiba yetu ya kikiristo ambayo wakati mwingine mtu anazikwa baada ya wiki,na kaburi linawekewa zege kabisa hapo inakuaje mkuu?
 
KUna tukio nimekutana nalo shambani siamini mpaka kwasasa naona kama ni ndoto au ni uoga wangu au nini sielewi chochote mpaka sasa hivi kwa nilichokiona . Miezi kazaa hapo nyuma

Katika kijiji chetu tulikuwa na msiba wa mama fulani ambaye alifariki baada ya kuugua mgonjwa wa kupooza kwa mda mfupi akafariki kwenye msiba wa mama uyo kulitokea vurugo ambazo ndugu za marehemu walikuwa wana attack mke mwenzake pamoja na mume wao kuwa ndo chanzo cha ndugu yao kufa

Vurugo iyo ambayo ilipelekea polisi kuja kuingilia kati na kuruhusu maiti izikwe kitu ambacho ndugu walikuwa wanakataa kuwa maiti haizikwi kwasasa imepita karibia miezi 7 toka tukio ilo litokee leo nilivyokuwa nakwenda shambani nimekutana na mama uyo ambaye tulimzika akiwa ndani ya shamba lake ambalo ilikuwa ndo njia ambayo mimi nilikuwa napitia kila siku nikienda shambani kwangu nilimkuta akiwa chini ya mtu akiwa amepooza vile vile

Kitu ambacho mpaka kwasasa nashindwa kuelewa kama ni uoga wangu tu au vipi sielewi chochote mpaka kwasasa
Swali ,wewe ni ccm ,kama ndivyo , tumewazoea na maneno ya maji taka
 
Vipi misiba yetu ya kikiristo ambayo wakati mwingine mtu anazikwa baada ya wiki,na kaburi linawekewa zege kabisa hapo inakuaje mkuu?
ila mim navojua mtu kamili huchukuliwa na kwenda kufichwa nyuma ya mlango, na ile maiti inakua ya mtu mwingne au kizee kimsukule hakina nguvu wala msaada kwa wachaw tena.
Sema mazingara ombe hufanyka, nyie mtaona sura ya ndugu yenu ila sie.
Mtazika mtu mwingne ila ndugu yenu anakua kafichwa ndan.

Ukitaka ujue hii endapo atafarik mama anae nyonyesha huwa ule msukule unawasumbua ukitaka mwanae umnyonyeshe.
huwa wanamrudisha kuja kunyonyesha.
Au mtoto huijiwa usiku akanyonye
wakiona usumbufu sana kale katoto wanakaua kwa kifo cha mchongo pia kaje kaishi na mama ake kapate ziwa.

Ila hua nasikia, ukiuvunja mlango kwa shoka alipo fichwa malehem, huwa anatoka. au kuwachimba mkwara watu kwa kujifanya umemjua alie mchukua ndugu yenu kwa kunoa panga.
huwa wanaogopa anaweza achiliwa ndugu yenu, kama mchaw ni mwoga.
 
Inaendelea

Basi mchawi akisha hakikisha aidha kampuliza mlengwa wake hiyo sumu au kamuwekea kwenye nguo, yeye mchawi hujua kiwango cha hiyo sumu aliyoweka itaanza kufanya kazi baad ya siku ngapi,

Sumu ikishaaanza kushambulia ubongo na kisha moyo basi mapigo ya moyo huanza kushuka na mwshoe hupotea kabisa na huwa wa baridi na kukauka ngozi kwa kifupi hakuna kifaa hata kimoja cha hospitali kitakachoweza kuonyesha kwamba moyo unadunda au kitasema kwamba mtu ni mzima ila itaonyesha amekufa... Hapa sasa ndo utajua kwanini chura yule jike hutumika maana sumu yake ndo inasababisha mtu kuonyesha dalili zote za kwamba mtu amekufa ila hapana hajafa..

Kiufupi mlengwa anakuwa hajafa ila ile sumu inakuwa imeleta pararaizi ambayo ni ya kiwango kikubwa mno kinachoathiri hadi moyo kwa kiwango kikubwa,

Hivyo baada ya mtu kuonekana amefariki...mchawi yeye hujua kiwango cha sumu aliyompa itaisha nguvu baada ya siku ngapi tangu mtu kuonekana kafariki, hapo inaweza kuwa ni sumu ya siku sita, saba au nane etc.

Sasa kwakuwa mchawi anajua sumu hiyo itaisha baada ya siku ngapi...na ikiisha kinachofuata ni mlengwa kuzinduka ila hatokuwa na akili timamu huwa anakuwa kama na mtu mwenye tatizo la usonji au anaweza kuwa kapoteza kumbukumbu nyingi au anakuwa hawezi kufikiri sawa sawa kwani ubongo unakuwa umeathiriwa vibaya sana na ile sumu.

Hivyo mkishazika mtu ambaye anaonekana kafa ilihali ni kazimia tu... Yeye Mchawi huenda kumfukua mlengwa wake zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya sumu aliyompa kuisha nguvu kwani anajua asipofanya hivyo mtu atazinduka na ataishiwa pumzi huko kaburini na atafariki.

Kwahyo mchawi humfukua mlengwa wake na anampatia baadhi ya mitishamba ili kuondoa baadhi ya sumu za ule mmea kwani asipofanya hivyo mtu huweza kuwa chizi kabisa na yeye mchawi lengo lake sio kukaa na chizi,

Akishampatia hiyo mitoshamba basi huanza kumtumia aidha kulima mashamba yake nyakati za usiku au kumuweka tu ndani na kumtesa kwa kumpa chakula kibovu na kumpiga na pia jambo la muhimu zaidi huwa anamkata msukule wake ulimi ili asiwe anaweza kuongea.

Na hivyo ndo jinsi msukule anavyochukuliwa, ila habari njema ni kwamba kama ukikutana na msukule usiogope huyo ni mtu kabisa kama wewe sema tu sumu aliyopewa imemharibu akili,

ila kama ukimuokoa msukule kutoka mateka ya mchawi anayemfungia... basi kuna baadhi ya waganga au hata hospitalini wanaweza kumtibia na mtu akapona kabisa na kuludi hali yake ya utimamu wa akili. Kwahiyo msukule sio mtu aliyekufa na wala hana nguvu zozote za kupotea, pia hana hata nguvu zozote za kiroho za kimiujiza,

Cha kuongezea pia japokuwa hii ni nje ya mada ni kwamba Mchawi yoyote anayekuroga ni lazima kuwepo na physical contact au ukaribu, kiufupi hakuna uchawi wa kutumwa kama mnavyohadithiana kwamba mtu yupo Mwanza anamlushia jini mtu aliyepo Dodoma. Hapana haipo hivyo

Hata nguvu za kupaa na ungo au kutoweka wachawi hawana nguvu hizo ila zilikuwepo hizo nguvu kwa miaka mamilioni nyuma ila mlango huo wa kichawi ulifungwa na mwenye dunia yake, kwahyo kwa sasa mtu asikudanganye hakuna mchawi anayeweza kupaa na ungo wala kutoweka au hata pia kumlushia jini mtu akiwa mbali ila mchawi ili akuroge ni lazima atengeneze dawa kwa kutumia mitishamba kisha aidha akupulizie au akuwekee kwenye chakula au atege ukanyage ndo hiyo sumu ikiingia ndani mwako ianze kukutesa. Na hapo ndo Demons zitaingia kupitia milango ya mateso yako yaliyosababishwa na sumu. Na demons hapo zitakuwa na kazi ya kunyonya energy ya roho yako kwa kukutia hofu akilini na Kukukatisha tamaa tu basi.

Kwa leo tuishie hapa ila eleweni wachawi hawana nguvu hizo za kimiujiza ila wana elimu ya juu mno ya mitishamba na kutengeneza sumu kwaajili ya kutesa miili ya watu na kuharibu saikolojia za watu.

MWISHO
Duh🤔
 
Yapo Sana ila huyu kila kitu ni mbishi.
Atakwambia mara Mungu hayupo,uchawi haupo na bla bla zingine kibao
watu wa hvo ndo wachawi hawatak watu waamin kama kuna uchaw wabak kizan ili wao wawafanye wanavotaka.
Mtu akijua kuna uchaw atajikinga kiroho kupitia iman yake kusari ama mizizi.
 
Mkuu unataka kusemaje mbna unanitishia amani
Mkuu hujasikia habari ya kijiji cha maajabu kupitia shuhuda za wananchi wake.

Kaishi na wachawi Mkuu ili kudumisha mila na desturi zetu za kiafrika.

Nafikiri kwa hali hiyo utakuwa na amani
 
Ndio anaweza moyo wake unakuwa unatumia energy ndogo mnoo kiufupi anakuwa nusu mfu hata damu huanza kuganda kwa mbalii
Energy ipi iyo ndogo anatumia maana kule chini bila oxygen mtu anatumia dakk 3-10 anakosa hewa kabisa na kufariki maan ata akipumua kidgo sana pia anatengeneza carbon, na ninavojua misiba nyingi ya kiafrika hamna msiba watu wanakaa siku moja ni zaid ya week.
 
Back
Top Bottom