Nashindwa kulielewa hili gari

Modern cars kuanzia 2002 zina computer. Huko ndio kunawekwa maelezo yote yanayolihusu gari hilo. Likitokea tatizo kubwa kwanza engine management light inawaka na unatakiwa usome kutoka kwenye computer kujua chanzo. Ukianza kubadili vitu bila kusoma humo utamaliza hela na usijue shida iko wapi.
 
Mimi nilikaa na BMW 318 miaka mitatu bila shida yoyote mpaka nikaiuza...Fata tu maelekezo ya service tu.
Mkuu wabongo washazoea service ni kumwaga oil tu, tena hapo bajeti unakuta kaweka top top elfu 50. Oil ya 30k, filter 10k na fundi 10k. Mbongo kupeleka gari garage ikakaguliwe yote hafanyi hiyo kazi hata akiwa na safari ya kwenda mbali atamwaga oil tu tena hapo kama imemaliza au imekaribia kilomita. Tyre wananunua hizi za kichina na hapo kubadilisha ni mpaka iwe kipara. Tyre za kichina sio reliable kabisa, tena hasa kwa safari ndefu ila kwakuwa tunapenda vya bei rahisi tunaona poa tu.

Gari ya kizungu lazΔ±ma ukubali kila baada ya miezi sita at least uipeleke check up, tena sio zile chini ya mti ni ile unakabidhi gari na email yako wewe unaendelea na mambo yako. Check up ikiwa tayari unakutana na Invoice kwenye email unalipa unaenda na slip yak unachukua mali yako na guarantee juu.

Nilijisikia fahari sana nimepeleka gari service siku naenda kuchukua nikakaa na Muhasibu wao kuongea akaniambia ile garage Mzee Jakaya ndio garage ya magari yake. Na wala bill haikuwa kubwa, walikagua gari na wakatoa spare ambayo waliona inaelekea mwisho wakaweka nyingine basi, ningepeleka chini ya mwembe vingebadilishwa mpaka vizima ili kazi iwe kubwa na wao apate pesa nyingi.
 
Uko sawa mkuu.,Hapa kwetu watu wanamiliki magari kwa ushabiki na sio kujua gari lipate SERVICE aina gani...
 
Umenielewa vizuri au umekurupuka kunijibu bila kuelewa. Punguza wenge, soma tena nilichosema halafu urudi tena....
 

Tazameni hii video halafu mshushe comments zenu,hii in service ya 2001 BMW 3 series. Kabla hazijawa complicated zaidi.
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ Jamaa unashangaza kinoma noma yani.. ila acha maisha yaendeleee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…