Ngoja nikupe mfano mmoja labda utanielewa maana hatari Mimi nilikua mbishi kama wewe. Nimemiliki German car na nilikua na Pesa ya spare parts na service lakini ilikua inashinda zaidi garage kuliko nyumbani kwangi kwa miaka 2.
Rafiki yangu msauzi mjini Johannesburg alikua amemaliza mkataba wa corolla akawa anataka kuchukua SUV. Wenzetu Sauz hawanunui gari mpya kwa cash,ni contract ya miaka 5-7.
Akaniomba nimsindikize kwenye Hyundai/KIA dealership akaulizie akacheki SUV zao . Kufika pale tukakuta Benz,BMW kibao na Audi chache,ikabidi mi niulize jamani nyie no dealers wa hizi German brands pia? Kumbuka pale wanauza gari mpya tu na exclusive Kia/Hyundai.
Marketing officer hajaniambia hizo German brands wateja wamekuja kufanya trade in baada ya warranty kuisha na kuchuku eidha kia au Hyundai. Ipo hivi Merc,Benz, Audi wanampa mteja warranty ya km 60000 kwa miaka Kitano toka anaponunua gari.
Maana yake service zinafanywa na wao,repairs pia nk. Warranty ikiisha maana hata mkopo umemaliza so service ni juu yako. Bila warranty hizo gari ni kichomi maana rate ya breakdown baada ya 60000 km ni kubwa mno. Parts na service in ghali kweli.
Mteja anaamua kwenda kia/Hyundai au Toyota dealership kufanya trade in. Wao wanaithaminisha ile gari na kuichukua kama sehemu ya malipo ya gari Mpya watakayo mpa mteja. Unakuta thamani yake hatari sio kubwa sana ,kisha wao wataiuza kwa being ya kawaida cash bila warranty kwa mteja ambae yupo tayari kubeba huo msalaba.
Halafu hapa bongo mtu unaagiza Mercedes au BMW out of warranty yenye umri zaidi ya miaka 10,unatarajia nini kama sio kichomi na pressure?
Maajabu ni kwamba kampuni kama KIA, Hyundai, Toyota wanatoa unlimited km on motor na gearbox kwa miaka 7 kama mtu amechukua mpya.