Nashindwa kulielewa hili gari

Nashindwa kulielewa hili gari

Mimi nna SVR autobiography. Chawa wewe
Kila kitu kinawezekana.. kuwa wa SVR wewe sio wa kwanza na sio kuwa wa mwisho. Sinaga ukaribu wapumbav.u kama wewe na mwenye mantality ya kimaskini namna hiyo
 
Bado nipo ndani ya gari nimekaa sijala na siskii njaa haya magari yanazingua asikwambie mtu nimepongezwa sana ofisini sijui naingiaje kesho nilimtetemesha mpaka HR ila lazima nitengeneze no way
Mkuu ni kweli umetetemesha,Sawa utatengeneza omba mungu itulie,je ikizingua kitu kingine tena? Ndo utakuwa mwanzo wa kufilisika Mzee.

Ebu cheki mwenendo wake,kama mzuri komaa nayo kama sio uza,usije ukataka kuonekana mshua huku unateketea huku unajiona.
 
Huwezi kukataa sometimes jamaa nimetumia sana Allion yake so siwezi kugoma kuazimisha ikowa mimi huazima
Hata mie kumnyima gari mtu wangu wa karibu siwezi, ikiwa na mie huwa nachukua magari za watu. Ila ikitokea hitilafu huwa narekebisha mwenyew.
 
Magari ya ulaya either ni soft sana au hatujui kuyatunza.

Jamaa yangu anafanya kazi za kuvuta magari mabovu sana sana kutoka mikoani. Anakwambia gari anazovuta mara kwa mara ni Audi Q7, VW Touareg, Discovery 3 na 4. Kwa ufupi ni vimeo, hakuna siku utasikia Prado imefia mkoani inaitaji kuvutwa 😂😂😂
Ukiacha utunzaji lakini pia upatikanaji wa spare pia ni tatizo. Hizo Prado na nyingine sio kwamba haziharibiki lakini pia ukipata breakdown kupata fundi na spare popote kwenye kamji ni rahisi..
 
Gharama si zilezile tu kama wana hela je wasinunue? Ishu iko pale pale spea bei ghali iwe dar au lubumbashi. Kote kuna wenye hela na walalahoi.
Nakupa homework moja, siku angalia magari ya IT yanayoelekea nchi za wenzetu alafu fananisha na yetu.. Ni mentality tu sio ishu za hela wala nini. Wakenya tu hapo jirani wametupiga gap la kutosha tu
 
Pole sana mkuu mm nazani hapo ni pump tu pump yake bei n8 ghari kidogo..
 
Sio atafute, bali akutafute umsaidie..

Mzee gari hizo mafundi ni wawili ninawajua, yupo huyu mwamba jitu, kuna mwamba mwingine anaitwa ivan yupo mwenge pale yeye ana deal na gari za Ulaya tu.

Mafundi wapo mkuu.

Mimi sipo mjini. Nimetoka kidogo. Nipo kijijini huku. Kuna muda hata namba yangu haipatikani.
 
German cars are known for being unreliable worldwide, wabishi can Google that for themselves. Kununua BMW bongo afu ya zamani ni tatizo la kujitakia. Huo ni mwanzo tu utaliuguza Hadi uchoke
Show me luxury car ambayo ni reliable hata kama ni toyota.
 
Nakupa homework moja, siku angalia magari ya IT yanayoelekea nchi za wenzetu alafu fananisha na yetu.. Ni mentality tu sio ishu za hela wala nini. Wakenya tu hapo jirani wametupiga gap la kutosha tu
Haya magari yote yalikuwepo nchi ilipofunguka miaka ya zamani peugeot, land Rover, benz, Volvo, Renault ila toyota alikuja ku take over bongo kwa sababu ya urahisi wa spea kwa wananchi wa kawaida hayo mengine bado wananunua watu wenye ukwasi wa kujiamini
 
Nakupa homework moja, siku angalia magari ya IT yanayoelekea nchi za wenzetu alafu fananisha na yetu.. Ni mentality tu sio ishu za hela wala nini. Wakenya tu hapo jirani wametupiga gap la kutosha tu
Hilo la magari ya IT, nakuunga mkono kuna gari kali zinapita pale mbezi hatari sana, wabongo tuna mentality mbaya sana.
Mtu hajawahi kumiliki au kuendesha gari ila anatoa ushuhuda mpaka kero
 
Sasa hilo mbona liko wazi tena wabongo au wewe riziwani uko ulaya out of touch na reality? Of course watu wanataka usafiri ila wanataka spea rahisi kwani huo ni muujiza kwa nchi maskini kama Tanzania? Au nyie mna hela mnashangaa mtanzania kuona gari za Europe zinagharama kwenye spea? Huo ndiyo ukweli.
Hakuna Luxury car yenye spea za bei rahisi. Kama ipo itaje.
 
Hizo warranty ni limited kulingana na nchi sasa bongo kama hawapo utagharamia usafiri wa kulipeka ulaya lifanyiwe service na kulirudisha bongo?
Kwamba hapa Bongo wenye Mercedes,Audi,Bimmer etc likizingua under warranty hua wanayarudisha ulaya kufanyiwa service sio? 😄😄😄😄😄
 
Mentality za kifukara hizo mkuu, nakushauri achana nazo. Hakuna service ya million 20 labda gari iwe imeanguka. Nilikaa na yule muhasibu nikaongea nae sana, service na check up za kawaida bill kubwa aliyoniambia ni Million 6, tena hapo ni gari ina worth more than 200m. Sasa kweli mtu anaafford kununua gari zaidi ya millini 200 ashindwe service ya 6M tena hapo unakuta anapeta miaka kadhaa bila service ya gharama hivo tena?

Subiri nikupe hii, kuna rafiki yangu alikuwa anatoka mkoa kują Dar, njiani gari ilimsumbua kama mara mbili na kote alikuwa akisimama anaita mafundi wanatengeneza anaendelea na safari. Alivyofika Dar baada tu ya siku lile tatizo likaanza upya, nikampeleka hapo kwa hao jamaa, ilibidi tuombe warekebishe kwa express maana alikuwa na safari ya kurudi mkoa tena. Gharama aliyotumia pale haikuzidi elfu 35 na walitibu tatizo kabisa. Lakini huko njiani alikotengeneza alinunulishwa mpaka pump mpya wakati tatizo hata halikuwa pump.
Service ya kitu gani hio inafika 6m mkuu?
 
Back
Top Bottom