Nashindwa kumsamehe Magufuli kwa hili

Nashindwa kumsamehe Magufuli kwa hili

Wewe kweli ni mataga wa PhD, tukio ambalo hakuna hata ripoti moja iliyo rasmi unaona ugumu kuamini conspiracy na unataka uthibitisho ila tukio ambalo limetolewa ripoti nyingi zilizo rasmi unang'ang'ania kuamini conspiracy! Kalaghabao.
Kwa mihemko hii hutaweza kunielewa hata upigiwe tarumbeta!😂
 
Tangu lini serikali inagharamia matibabu ya wabunge?
Ulimsikia waziri wa afya wakati huo Ummy Mwalimu? Alikua waziri wa nini, si waziri wa serikali?

Job Ndugai ametibiwa India, alikua anatibiwa na nani?
 
Kuwa na utata au kutokowa na utata sio kiini cha mjadala. Hata ripoti rasmi ya tukio la Lissu ingetolewa au ikitolewa lazima kuna watu au upande ambao kwao itabaki utata lakini jambo la muhimu lazima watu waonyeshe wamewajibika angalau kufanya kazi yao ya msingi.
Rudi kasome komenti zangu za awali nimejibu maswali yako mengine tatizo uelewa.
 
Hv ungekuwa rais ungeweza kujigawa ufanye ubaya na kuamulu kila ubaya kila mkoa ? Kuna tunaonesha unyani wa hali ya juu , yaan makosa ya mgambo unaenda kusema alitumwa na RPC , akili fupi sana , ktk maelezo yako yote sijaona neno rais ila mwisho kweny lawama unamshishia rais kana kwamba aliwatuma
Vyombo hivi vinavyofanya utesaji na upotezaji wa wakosoaji na wapinzani wa serikali hasa za ki Africa. Hufuata hulka, maelekezo na amri wahusika wa ukosoaji huo.

Geita anakotoka mh sana hakukutakiwa upinzani na hasa mpinzani mwenye nguvu .

Kama alivyokuwa akikemea ufisadi na uzembe kazini. Alitakiwa pia akemee uhalifu wa reja reja, hasa dhidi ya wapinzani wake. Lakini kimya kile kilibariki viroboto wengi , na upande wa pili hakuna rangi hawakuwahi kuishuhudia .
 
kwa tukio hili Magu hakutakiwa kufa alitakiwa kupewa adhabu hapa hapa tushuhudie. Hata kilema kizito au ukichaa tu
 
Kuzuia matibabu na kumnyima haki zake za kibunge, hilo nalo vipi? Wabunge wa CCM na wana CCM wengine kuzuiwa kwenda kumuona Nairobi nako ni sehemu ya upelelezi? Hujui hadi leo wabunge wengi wa CCM na wana CCM wengine wanaumia sana kushindwa kwenda kumuona Nairobi?

Muacheni abebe mzigo wa dhambi mwenyewe, msimsaidie kwa jambo msilolijua.

Dhambi kubwa ni kumficha dereva,shuhuda namba moja.
 
I declare interest Mimi sio mwanachadema kabisa kabisa lakini nikiwa kama mtanzania mwenye akili timamu nikifikiria tukio la Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi pale Dodoma ile 2017 naumia mno.

Kushambuliwa kwa binadamu kama mnyama mchana kweupe kwenye majengo ya serikali inaumiza saana, lakini kinachouma zaidi ni kwamba hakuna hata mtu mmoja alieshikiliwa wala kuhojiwa shameful, tutawaambia nini watoto wetu huko baadae.

Kitendo cha Magufuli Rais wa nchi Amiri jeshi mkuu mfariji mkuu kukaa kimya bila kujitokeza hadharani na kukemea lile tukio liliniumiza mno kwa nature ya Magu aliwezaje kukaa kimya what was behind the scenes

Je angeshambuliwa Polepole kama Lissu je mzee angekaa kimya? Lissu alipigwa risasi na nani, nani aliwatuma, kwa maslahi ya nani ili iweje nikikumbuka hili tukio hata unitajie mema mia ya John siwezi kuyaona

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Ha ha ha!
Vivyo hivyo kama zilivyo zile 10 Commandments; Hata ungefanya mema/mazuri yapi, ukikosea japo moja tu, kamwe huwezi kuona Ufalme wa Mbinguni!
 
Soma tena hiyo post yako ndio utajua kwanini nimejua una cheti feki wakati sikujui.
Ninyi mlikula keki sasa ni zamu yetu, Mama kaachia uwanja kila mtu na nguvu zake.
dance.gif
 
Ulimsikia waziri wa afya wakati huo Ummy Mwalimu? Alikua waziri wa nini, si waziri wa serikali?

Job Ndugai ametibiwa India, alikua anatibiwa na nani?
Unasikitisha sana. Unashusha hadhi ya JF unajua. Uwe unafanya utafiti mdogo kabla ya kuongelea mambo makubwa ila usiyokuwa na ufahamu nayo.

Matibabu ya wabunge yanaratibiwa na Bunge. Na ndio maana hata Lissu mwenyewe hajawahi kuilalamikia serikali juu ya matibabu yake mahali popote pale. Hilo ni jukumu la Bunge, and so unapaswa umlalamikie Spika.

Lissu anailalamikia serikali linapokuja suala na uchunguzi, na yupo sahihi. Hata hivyo siku zote amekuwa akikwamisha uchunguzi kwa sababu anazozijua mwenyewe.

Siku nyingine usiongelee mambo usiyoyajua. Unajiaibisha wewe binafsi, familia yako na zaidi ya yote unashusha hadhi ya JF kama home of great thinkers.
 
Kitendo cha Magufuli Rais wa nchi Amiri jeshi mkuu mfariji mkuu kukaa kimya bila kujitokeza hadharani na kukemea lile tukio liliniumiza mno kwa nature ya Magu aliwezaje kukaa kimya what was behind the scenes

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Mkuu kiroka, yaani Magufuli aagize mwenyewe kuwa Tundu Lissu auawe na azikwe kwao Singida mara moja, halafu ulitaka yeye mwenyewe tena alaani?
 
Unasikitisha sana. Unashusha hadhi ya JF unajua. Uwe unafanya utafiti mdogo kabla ya kuongelea mambo makubwa ila usiyokuwa na ufahamu nayo.

Matibabu ya wabunge yanaratibiwa na Bunge. Na ndio maana hata Lissu mwenyewe hajawahi kuilalamikia serikali juu ya matibabu yake mahali popote pale. Hilo ni jukumu la Bunge, and so unapaswa umlalamikie Spika.

Lissu anailalamikia serikali linapokuja suala na uchunguzi, na yupo sahihi. Hata hivyo siku zote amekuwa akikwamisha uchunguzi kwa sababu anazozijua mwenyewe.

Siku nyingine usiongelee mambo usiyoyajua. Unajiaibisha wewe binafsi, familia yako na zaidi ya yote unashusha hadhi ya JF kama home of great thinkers.
Polisi huwa inafanyaje uchunguzi na kukamata watuhumiwa kwenye kesi za watu wanaouwawa ?
 
Msamehe,usiposamehe wewe pia hutasamehewa,lakini pia hakuna ushahidi kuwa magu ndio alimpiga risasi lisu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Ushahidi upo wa magu kumtuma Makonda na kikundi cha wasiojlikana, wala usiwe na wasiwasi. Ni suala la muda. Hata kama ametanguia iko siku tutakunya kwenye kaburi lake pale Chato
 
Msamehe,usiposamehe wewe pia hutasamehewa,lakini pia hakuna ushahidi kuwa magu ndio alimpiga risasi lisu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Acha kujaribu kumsafisha shetani.

Alikataza watu kumchangia damu na fedha.

Alikataza viongozi wenzake wa chama na serikali kwenda kumjulia hali Nairobi.

Alimnyima stahiki zake zote za kibunge na akaishia kumvua ubunge.

Shetani wahed!
 
Hakuzuiwa labda haukuwa unafuatilia , Lissu alikataa kuhudumiwa bongo na kibaya zaid akaona kenya sio sehemu sahihi pia akaenda ubelgiji na kumbuka dhamana ya serikali ni lazima uhudumiwe ndani ya nchi na kisha ikihitajika ndo unapewa kibali na serikali kwenda nje so ukiwa nje haki zako za kibunge zinatimizwa maana umetoka nje kwa taarifa rasmi , ila kwa kipindi chote anahudumiwa nje hakukuwai kupelekwa taarifa yake bungeni kuwa ana matatizo na ukumbuke serikali yyt duniani haijiendesha kwa vyombo vya habari au facebook au jf , hiyo ni pie hata Lissu angekuwa rais utaratibu ungekuwa huo huo so Lissu alikosea na anajuwa kisheria alikosea ila kisiasa alitaka kulitumia lile ttzo lke km mtaji wa uchaguz 2025 ila alikuwa kakosea kusoma upepo maana wenzie walimuwai kumpokonya jimbo ambalo ndo ilikuwa silaha kubwa kwake
Hivi unajua watu kama kina Polepole na wengine leo hii wanauona ubovu wa uendeshaji serikali ?!. Kuna siku karibu utatamani uliyoyaandika uyameze, lakini kumbukumbu hazifutiki.

Ulitaka Lissu atoe taarifa gani ?, huku uwanjani alikuwa amesindikizwa miongoni mwao akiwemo spika !! Ambaye ni kiongozi muhimili aliokuwa anautumikia Lissu. Haya mambo ya kujifanya mzalendo zaidi, leo kina Polepole wanaishuhudia rangi halisi ya unafiki. Miongoni waliojibu upumbavu ni pamoja na yeye juu ya Lissu
 
Back
Top Bottom