Nashindwa kumwacha hata kama hanitaki tena

Nashindwa kumwacha hata kama hanitaki tena

Tafuta pesa acha utoto kulialia, unamaliza chuo badala ya kutafuta kazi unasakama wanawake? Jibidiishe ushike pesa watakuja mpaka watakukifu, majina 'sweet, baby' yanauzwa kijana.
 
Hakuna kitu kizuri maishani kama kujipenda mwenyewe...ndio maana ninapokuwa kwenye mahusiano wanasema sijali najisikia hii yote sababu najipenda mwenyewe na kujiona bora nafanya ninachojisikia..acha kumuwazia mtu ambae hana mchango wowote mpaka wewe kufika ulipofika
 
Kibaya ni kwamba nshajaribu kutafuta mpenzi mwingine lakini sikuona kama anamsaada
 
Kibaya ni kwamba nshajaribu kutafuta mpenzi mwingine lakini sikuona kama anamsaada




Mkuu hebu waza mara mbili je na yeye anakuwaza kama unavyomuwaza tena usikute huko mwenzako anapigwa mambo wewe unakufa na kihoro..hebu jaribu kujipenda mwenyewe penda maisha yako..hebu fikiri wazazi wako wana matumaini gani kwako...mimi kwenye mahusiano nakuwa don't care sana hii yote napenda kutimiza malengo yangu kama wa kuoa nitakutana nae huko huko mbele kwa mbele
 
Ndo maana kumbe mtu anakosewa na still yeye ndo anaomba msamaha,mapenzi haya! Wengine hatuelewi tunaweka tu na kuchapa lapa.......
 
Usiwasiliane nae kabisa muda ni muhimu lakini ni ngumu pendelea kuwa na marafiki au kuwa busy usiwe mpweke ikakupa nafasi yakuaanza kumfikiria......kuliko kuwa alone ingia JF soma mada za watu na comments utajikuta unacheka na kufurahia hahahahah pole mkuu
 
Back
Top Bottom