Nashukuru Rais Kagame anaigopa Tanzania

Nashukuru Rais Kagame anaigopa Tanzania

Rwanda yenyewe ilikuwa sehemu ya tz, tunaweza tukaidai ili kukamilisha na kurejesha German East Africa, pia hawezi isema tz maana ndo waliompika so baba hasemwi. Malawi wanapata wapi jeuri ya kuita ziwa nyasa ni la kwao? Wanatuchukuliaje aisee?
 
Hivi ikitokea siku marais wa Tz, Rwanda na Burundi kukubaliana waungane , je wananchi wote wa hizi nchi watakubali? Ninahisi Tz na Burundi wanaweza kuafiki lakini Rwanda naona kama vile hawatakubali, wapo unique sana wale jamaa na wanaonekana sio watu wakuchangamana na jamii zingine
 
Watutsi wanajisikia sana. Hawawezi kukubali
 
Juzi Mhe Rais Paul Kagame akiwa ziarani huko Benin ametaja kuwa mgogoro wa DRC na M23 chanzo chake ni wakoloni kumega ardhi ya dola ya kale ya Rwanda na kuzipa nchi jirani.

Bw. Kagame ametaja nchi jirani zilizopewa ardhi Ardhi ya dola ya Rwanda ya kale ni DRC, Uganda na Burundi.

Kati ya nchi zote nne zinazopakana na Rwanda ni Tanzania tuambayo Bw Gen. Kagame hakujaribu kuitaja kua anadai ardhi hapa.

Ijapokua Historia inataja koo za Wanyiginya ambayo asili yao ni Rwanda ya kale zilikua zikimiliki tawala nyingi nchini Tanzania hasa mikoa ya Kanda ya ziwa na Kigoma. Kama ilivyo Burundi, DRC na Uganda.

Nadhani Kagame alielewa vyema somo alilopewa na Tanzania mwaka 2013 hatamani tena kupata somo la pili aina ya remidial.

Haha.
msilale mkijua yameisha , anaish kwa timing siku mkizubaa mtastuka kauli hii anaongelea akiwa dodoma
 
Mleta maada, fahamu kuwa kabla ya ujio wa wazungu hakukuwa na Tanzania au kitu chchote kinacho fanana na Tanzania. Lakini Rwanda ilikuwa ni dola kamili yenye ukubwa maradufu ya Rwanda ya Leo, Tanzania ya sasa i creation ya German East Africa.
 
Rwanda yenyewe ilikuwa sehemu ya tz, tunaweza tukaidai ili kukamilisha na kurejesha German East Africa, pia hawezi isema tz maana ndo waliompika so baba hasemwi. Malawi wanapata wapi jeuri ya kuita ziwa nyasa ni la kwao? Wanatuchukuliaje aisee?
Haijawahi kuwa sehem ya TZ my Friend, irikuwa sehemu ya German East African Company. Kuropoka eti ilikuwa sehemu ya TZ hata wanyarwanda wanaweza kusema Tanzania ilikuwa sehemu ya Rwanda, and by the way they have more ground than TZ, kwasababu kabla ya wazungu/wakoloni wa German hakukuwa na TZ au kitu chochote kinachofanana na Tanzania, Lakini kulikuwepo na dola ya Rwanda kubwa kabisa ikiwa na influence mpaka kwenye baadhi ya maeneo ya DRC, Uganda na TZ yenyewe, ukihitaji masomo kuhusu hilo nitafute, but you can do your own research. So dont put your self into that illusion. If that is the Case Rwanda has more right than TZ
 
Tanzania na Rwanda zimetenganishwa na Mto mkubwa tu.

Ardhi ya rwanda na tanganyika haikuwa imeungana tangu enzi za ukoloni

Ndio maana pale benaco ngara kuna daraja kubwa linalounganisha hizi mbili. Hazijaungana natural

Hivyo kagame yupo sahihi kutoiweka Tanzania
Hivi Ngara-Kibungo nayo inatenganishwa na mto?
 
Tanzania na Rwanda zimetenganishwa na Mto mkubwa tu.

Ardhi ya rwanda na tanganyika haikuwa imeungana tangu enzi za ukoloni

Ndio maana pale benaco ngara kuna daraja kubwa linalounganisha hizi mbili. Hazijaungana natural

Hivyo kagame yupo sahihi kutoiweka Tanzania
Wakati wa ukoloni wa Ujerumani, Rwanda na Urundi ilikuwa ni mikoa ya Tanganyika.
 
Juzi Mhe Rais Paul Kagame akiwa ziarani huko Benin ametaja kuwa mgogoro wa DRC na M23 chanzo chake ni wakoloni kumega ardhi ya dola ya kale ya Rwanda na kuzipa nchi jirani.

Bw. Kagame ametaja nchi jirani zilizopewa ardhi Ardhi ya dola ya Rwanda ya kale ni DRC, Uganda na Burundi.

Kati ya nchi zote nne zinazopakana na Rwanda ni Tanzania tuambayo Bw Gen. Kagame hakujaribu kuitaja kua anadai ardhi hapa.

Ijapokua Historia inataja koo za Wanyiginya ambayo asili yao ni Rwanda ya kale zilikua zikimiliki tawala nyingi nchini Tanzania hasa mikoa ya Kanda ya ziwa na Kigoma. Kama ilivyo Burundi, DRC na Uganda.

Nadhani Kagame alielewa vyema somo alilopewa na Tanzania mwaka 2013 hatamani tena kupata somo la pili aina ya remidial.

Haha.
Sasa Kagame Kwa kauli hizi anamaanisha kuwa M23 wanapigana na DRC kama njia ya kudai maeneo hayo? Basi kama ni hivyo Kagame anajinadi wazi kuwa ndie anahusika na machafuko hayo. Kiukweli hoja na kauli ya Kagame niyakichochezi sana. Tukifuata historia hakika Dunia haitakuwa Salama kabisa, maana ukianzia South Africa, uje Zimbabwe, TZ na nchi nyingine baadhi ya makabila kihistoria walikuwa wakiishi Kwa kuhamahama sana, hivyo je na wao wageuziwe kibao? La hasha hiyo ni historia tu kujua chimbuko la kila eneo na watu husika, na yalishapitwa na wakati. Mwisho "Hawezi itaja TZ Kwa sababu hiyo nafasi aliipata Kwa msaada wa baba lao TZ"
 
Haijawahi kuwa sehem ya TZ my Friend, irikuwa sehemu ya German East African Company. Kuropoka eti ilikuwa sehemu ya TZ hata wanyarwanda wanaweza kusema Tanzania ilikuwa sehemu ya Rwanda, and by the way they have more ground than TZ, kwasababu kabla ya wazungu/wakoloni wa German hakukuwa na TZ au kitu chochote kinachofanana na Tanzania, Lakini kulikuwepo na dola ya Rwanda kubwa kabisa ikiwa na influence mpaka kwenye baadhi ya maeneo ya DRC, Uganda na TZ yenyewe, ukihitaji masomo kuhusu hilo nitafute, but you can do your own research. So dont put your self into that illusion. If that is the Case Rwanda has more right than TZ
Hakukuwai kuwa na dola ya rwandaa acha umang'aaa ata Tanzania ya Leo kulikuwa na dola nyingi ndani yake kabla haijatawalwa na wa German
 
Kagame ameongea vizuri sana, Hata Nyerere amewahi kulizungumza hili vizuri sana jinsi Wabelgiji na Wajerumani walivyogawana utawala wa Ufalme wa kale wa Rwanda. Sehemu moja ikabaki Kongo, hiyo ndo inayokaliwa na Wanyamulenge, na sehemu nyingine ikabaki Rwanda. Nyerere akasema kuwa ni makosa makubwa kwa nchi za Kiafrika za leo zilizorithi ardhi husika kutaka hizo ardhi lakini watu waliokuwemo katika ardhi hizo haziwataki. Yaani haiwezekani nchi ya Kongo ya leo kuitaka ardhi ambayo wanyamulenge wanaishi lakini haiwataki wanyamulenge.
 
Mleta maada, fahamu kuwa kabla ya ujio wa wazungu hakukuwa na Tanzania au kitu chchote kinacho fanana na Tanzania. Lakini Rwanda ilikuwa ni dola kamili yenye ukubwa maradufu ya Rwanda ya Leo, Tanzania ya sasa i creation ya German East Africa.
Acha upuuzi ndo notisi zenu za history huko kwenu mnavyofundishwa? Laiti moto uliokuwa unaendelea 2015 kabla ya kubadilisha regime ungeendelea tusingekuwa na hawa wapuuzi.
 
Naona watu wanapotosha Historia ya dola za kiafrika kabla ya ukoloni.

Dola ya Rwanda ilikua mdogo kuliko nchi ya Rwanda ya sasa.

Inayoitwa Tanzania ya sasa ni jumuisho ya dola mdogo mdogo zaidi ya 100 ziliunganishwa na wakoloni na kua Taifa la Tanzania la sasa.

Hivyo hivyo Kwa DRC, Kenya na mataifa mengine barani Afrika.

Rwanda kuna kesi ya ukoo amaa uzao wa Banyiginya ambayo ndiyo waliokua waanzilishi wa wa utawala wa dola ya Rwanda Karne ya 16.

Ilipotoke mitafaruko ya kiutawala baadhi ya wazawa wa Kinyiginya walikimbia Rwanda na kuzamia makabila mengine ya jirani katika maeno ya maziwa makuu. Huko walianzishwa dola zingine Kwa model ya Rwanda. Mfano unatajwa hata ukoo wa Chief Rumanyika wa Kagera Tanzania alikua Mnyiginya. Hii inaaneda hata Kwa watawala wa Waha akina Mwami wengi walikua Wanyiginya.

Dola ya Rwanda ya kale ilikua kama nusu yu ya eneo la Rwanda la sasa. Hasa maeno ya Mashariki mwa Rwanda. Hata maeneo ya Magharibi mwa Rwanda haikua dola ya Rwanda ya kale sema zilikua dola huru zilizotawaliwa na Watusti Wanyiginya.

Na mara zote dola hizi zilikua na uhamsama wa dola ya Rwanda.
 
Juzi Mhe Rais Paul Kagame akiwa ziarani huko Benin ametaja kuwa mgogoro wa DRC na M23 chanzo chake ni wakoloni kumega ardhi ya dola ya kale ya Rwanda na kuzipa nchi jirani.

Bw. Kagame ametaja nchi jirani zilizopewa ardhi Ardhi ya dola ya Rwanda ya kale ni DRC, Uganda na Burundi.

Kati ya nchi zote nne zinazopakana na Rwanda ni Tanzania tuambayo Bw Gen. Kagame hakujaribu kuitaja kua anadai ardhi hapa.

Ijapokua Historia inataja koo za Wanyiginya ambayo asili yao ni Rwanda ya kale zilikua zikimiliki tawala nyingi nchini Tanzania hasa mikoa ya Kanda ya ziwa na Kigoma. Kama ilivyo Burundi, DRC na Uganda.

Nadhani Kagame alielewa vyema somo alilopewa na Tanzania mwaka 2013 hatamani tena kupata somo la pili aina ya remidial.

Haha.
Remidial class ni kitu cha kuogopa kweli ?
 
Back
Top Bottom