Nasikia Cement imepanda hadi kuuzwa Sh 22,000 kwa mfuko. Mtaani kwenu mnanunua kwa bei gani?

Nasikia Cement imepanda hadi kuuzwa Sh 22,000 kwa mfuko. Mtaani kwenu mnanunua kwa bei gani?

Nimeona taarifa hii ya Azam TV ikieleza kuwa cement imepanda na kuwa baadhi ya maeneo inauzwa hadi Shilingi 22,000 hadi 23,500kwa mfuko wakati awali ilikuwa inaiuzwa kati ya Shilingi 15,000 hadi 17,000, sasa imekuwaje ghafla tu mzigo umepanda kwa kiwango hicho? Kuna nini nyuma ya pazia?

====================================

View attachment 3644265​
Shughuli za ujenzi nchini zinaweza kukumbwa na ongezeko la gharama baada ya bei ya saruji kupanda kutoka wastani wa shilingi 16,000 hadi 18,500, na kufikia shilingi 22,000 kwa mfuko mmoja katika baadhi ya maeneo.

Hali hiyo, inayohusishwa pia na upungufu wa upatikanaji wa bidhaa hiyo na kusababisha baadhi ya maduka kusitisha shughuli, imeibua wasiwasi miongoni mwa wananchi, wakandarasi na wafanyabiashara.

Serikali imesema inafahamu changamoto hiyo na tayari imeanza kuchukua hatua za kutafuta suluhisho, ikiwemo kufanya mazungumzo na wadau na wawekezaji katika sekta ya saruji ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa hiyo na kudhibiti athari za ongezeko la bei katika sekta ya ujenzi.
Hatari kweli ,enzi sie tunapanga tofali mfuko wa cement ulikuwa 9,500/= kama sasa ni 20,000/= kwa Dar basi noma ,kuna jamaa nimeona ndani ya mwezi amesimamisha ghorofa kwasasa anapua na kujenga fensi ,kwa speed ile naona jamaa anamaliza hadi finishing.
 
Watu wa Dar mnalalamika sana huku mwanza tunanunua sh 26000 kwa 25000 na hatupigi kelele ila huko kwenu daah mnakera muda mwingine
 
Viwanda vikubwa ikiwemo Dangote, Twiga na Tanga cement wapo kwenye shut down for maintenance, viwanda vichache vilivyobaki ndio vinazalisha na vyenyewe vimezidiwa na wateja , kwa mazingira hayo kwanini bei ya cement isipande
 
Asee noma mtaani kwangu mtimbira ndani ndani huko niliacha ni sh 21,000/= nimefika mwanza na musoma ni 24,000 kwa sh 25,000/ cha kushangaza nimefika tarime na rorya kuna boda boda wanakuletea mfuko wa cement kwa sh 16,000 au 17,000 mpaka mlangoni kwako. Usiniulize wanatoa wapi na wanapataje faida ila ujue ni boda boda hao sio wauza cement.
 
Back
Top Bottom