Nasikia Cement imepanda hadi kuuzwa Sh 22,000 kwa mfuko. Mtaani kwenu mnanunua kwa bei gani?

Hatari kweli ,enzi sie tunapanga tofali mfuko wa cement ulikuwa 9,500/= kama sasa ni 20,000/= kwa Dar basi noma ,kuna jamaa nimeona ndani ya mwezi amesimamisha ghorofa kwasasa anapua na kujenga fensi ,kwa speed ile naona jamaa anamaliza hadi finishing.
 
Watu wa Dar mnalalamika sana huku mwanza tunanunua sh 26000 kwa 25000 na hatupigi kelele ila huko kwenu daah mnakera muda mwingine
 
Viwanda vikubwa ikiwemo Dangote, Twiga na Tanga cement wapo kwenye shut down for maintenance, viwanda vichache vilivyobaki ndio vinazalisha na vyenyewe vimezidiwa na wateja , kwa mazingira hayo kwanini bei ya cement isipande
 
Watu wa Dar mnalalamika sana huku mwanza tunanunua sh 26000 kwa 25000 na hatupigi kelele ila huko kwenu daah mnakera muda mwingine
Tena wakati wao walikuwa wananunua kwa 16,000 sisi mwanza tulikuwa tunanunua kwa 21,500- 22,500.
Tulishazoea
 
Asee noma mtaani kwangu mtimbira ndani ndani huko niliacha ni sh 21,000/= nimefika mwanza na musoma ni 24,000 kwa sh 25,000/ cha kushangaza nimefika tarime na rorya kuna boda boda wanakuletea mfuko wa cement kwa sh 16,000 au 17,000 mpaka mlangoni kwako. Usiniulize wanatoa wapi na wanapataje faida ila ujue ni boda boda hao sio wauza cement.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…