Sikuwahi kumsikia mkuu!!!
Unajua mie sikuwa mtembeaji kabisa,nilikuwa ni mtu ambaye nilipenda kukaa nyumbani na kusaidia kazi za nyumbani na sikuwa mtu wa kutoka otherwise nimetumwa pale duka la jeshi Lugalo kununua mvinyo wa bei che basi narudi home,kama ni kutembea nilipenda kwenda kutembe pale maeneo ya daraja la Manzese nakaa kule juu ata masaa3 kisha narudi home,enzi hizo sii Manzese hii ya 'Walokole" naongelea Manzese ile ya vujo nyingi na biashara za nguo za mitumba,nauli ya daladala ilikuwa 50 kwa sisi madogo na 100 kwa mkubwa!!enzi hizo kuna kampuni1 tu ya simu inaitwa MOBITEL kabla ya kuwa sijui BUZZ,yale masimu makubwa yalikuwa yanauzwa laki3!
So sikuweza kuyafahamu makundi ya kihuni kabisa!