Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Mimi pia huwa nashangaa jinsi watu wanavyoweka mkazo kwenye katiba mpya zaidi ya ubora wa elimu yetu.
Tungekuwa na elimu ya viwango stahili suala la katiba lingekuwa agenda ya wananchi karibia wote na sio sasa ambapo wenye shida nayo ni wanasiasa, wanaharakati na wasomi tu.
Tungekuwa na elimu bora watanzania wasingeruhusu kuvunjwa kwa katiba, kuchezewa uchaguzi na mihimili mingine ya serikali kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.
Tunachohitaji haswa na elimu ya bora kwa ujumla na ya uraia ili tusije hata tukipata katiba mpya watu wakaendelea kuivunja maana watu ni walewale na uelewa ni ule ule na tabia zilizile.
 
Msingi mkuu wa ccm ni katiba tuliyo nayo kutaka kuibadili ni kucheza na maslahi yao hili ni jambo kubwa sana
Yatatokea mengi sana katika mchakato huu
Kiukweli hawana hoja yenye tija
Na chanzo cha shinikizo la haya yote ni uchaguzi uliopita


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wakati Kenya walipokuwa wanasubiri katiba yao mpya ilikuwa kila mtu ana mategemeo yamabadiliko ya kila kitu.Hata mtu akigombana na mwenzie anamwambia ngoja katiba mpya ije utaona ,mtu akienda dukani akikuta bidhaa bei ipo juu kidogo anajiapia kabisa kuwa hawa wanaopandisha bei vitu watakoma katiba mya ilkipatikana.Siku ilipozinduliwa Katiba iliyoitwa mpya walisherehekea na wa walipolala na kuamka asubuhi wakajikuta wako vilevile kama walivyokuwa juzi.😀😀😀
 
Nionyesheni ni wapi ambapo huyo mkuu wa mhimili huu wa Bunge alipohalalishiwa na katiba hii mbovu tuliyonayo kwamba naye hawezi kuwajibishwa,
Chanzo cha huyu spika kutowajibishwa ni Katiba yetu mbovu inayompa rais ufalme.

Kwa muktadha huo basi, kama kuwepo kwa Covid-19 bungeni kungekuwa kunamuudhi rais siku nyingi sana wangekuwa washaondolewa.

Lkn kwa kuwa ni Mungu mtu, na kwa kuwa kuwepo kwa Covid-19 bungeni Kuna mnufaisha yeye na chama chake ndiyo maana wapo hadi leo .

Usiulize ananufaikaje. Kuna ka kipengele ka kutoa misaada ya mrengo wa demokrasia kanataka bunge liwe na wabunge wa upinzani
 
Soma comment na 25
 

Loud and clear
 
Wakati wakenya washaandika katiba mpya na kusonga mbele kimaisha. Wabongo wataendelea na ujuaji wao hadi miaka 50 baadae bila ya kupiga hatua yoyote.
 
Mkuu,Ujue sipika halindwi na katiba pindi anapovunja katiba

lakini kwa nini sasa hakuna anayemshughilikia?

Ni nani wa kumshughulikia
 
Katiba ya nchi inalindwa na dola Rais, bunge na mahakama. Vyombo hivi vikiwa huru katiba italindwa lakini kama vilivyo hivi sasa ni mali ya Rais na ndiyo sababu anavitumia na kuviamrisha atakavyo!
 
Ndicho kilichonifanya nilete uzi huu hapa mkuu, Ni kina Nani hawa ambao watajiyokeza kwa ujasiri kudai haki yao pindi katiba inapovunjwa?

Ni hawahawa vijana wanapotangaziwa mandamano ya ukuta, kunatangazwa tu kesho usafi utafanywa na usalama, wanalala mpaka muda wa kukutana unapita na mandamano yanahamia mitandaoni?

Ni nani atakuwa mtetezi wa katiba ambayo tunadhani itakuwa mwarobaini wa viongozi wavunja katiba?
 

..nadhani Watz wapewe katiba mpya.

..inaweza isitusaidie sisi tuliopo sasa hivi lakini ikavisaidia vizazi vijavyo.

..katiba mpya na bora equals to 50% of the work, kinachobakia ni kuiheshimu na kuilinda.

..kwangu mimi that is better than katiba mbovu isiyolindwa wala kuheshimiwa.
 
Wanao taka Katiba mpya wote wanataka Katiba itakayo wapa urais kwenye ushindan na sio sababu ya wananch ndiomana ukiangalia chadema ccm nccr Act na wengine wengi kila siku wanaivunja Katiba yetu wazi waz
NCCR wameivunja vipi hiyo katiba ?
 
Shida sio kuandikwa katiba ingine,, shida ni implementation za hyo mpya,, kama ya zaman inawashindwa mtaweza mpya[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] #allpoliticiansarefilthyliers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…