Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
INani wa kuwawajibishwa hao wanaivunja katiba sasa?
Watu wengi mnashindwa kulijibu hili swali ndio maana hamuoni umuhimu wa katiba mpya.
Do you see tunavyofail. Wewe unawezaje kumuwajibisha Ndugai?Sisi wananchi
I
Ndio tatizo, binafsi tunapaswa kujilaumu wananchi kwanza kabla yote. Hizi harakati za mitandao naona zina nguvu ndogo sana.Do you see tunavyofail. Wewe unawezaje kumuwajibisha Ndugai?
Mahakama ndio ilipaswa kuwa na uwezo wa kuwawajibisha hawa wote wanaovunja sheria moja kwa moja. Lakini kwa sababu iko mfukoni mwa serikali ndio maana inakuwa ngumu.
Kwa katiba ya sasa mihimili inaonekana imetenganishwa lakini je kiuhalisia ipo hivyo?
Mihimili imetenganishwaje ikiwa Raisi anapangua na kupanga safu ya majaji akiamua?
Raisi anachagua M/kiti wa tume ya uchaguzi ambao yenye mwenyewe ni mshiriki, Hivi kwa akili za kawaida eti leo simba sc wachague Refa ambayo atachezesha match kati yao na yanga halafu utegemee hiyo match itakuwa fair?
Katiba ni muhimu sana, kuliko wengi mnavyodhani.
Wenye maamuzi wanapaswa kuwa wananchi na sio kiongozi Kuna ule msemo wa kijinga kabisa na nadhani upo Tanzania tu kuwa"kauli ya rais ni sheria" katika taifa la watu wanao jitambua huwezi kuta ujinga wa namna hii na ndio maana kila kitu hata Kama kina maslahi makubwa kwa taifa lazima fulani aseme hapana hatuwezi fika kabisaNadhani pia, utaratibu wa upatika aji wa katiba ukifanikiwa, kuwekwe kipengele kingine kitakachoondoa sauti ya Raisi kwamba, Wananchi watakapoona Katiba yao inamapungufu na wanataka katiba iundwe upya tena, kusihitajike sauti ya Raisi kuamua iandikwe au la, Ni kuachwe kipengele cha kupiga kura kuanzishwa katiba nyingine, wananchi watapiga kura, na hizo kura zikifikia kiwango kitakachoruhusiwa kuandikwa katiba zikitimia, mtu yeyote asiseme eti achwe ajenge sjui nini ndio aone katiba kama itaandikwa
Watu wa mtwara na lindi wameshalipwa korosho zao? The answer is no,nani kawajibishwa ?hakuna .watu wamerudishwa kwenye umasikini kwasababu ya katiba mbuvuNani kasema anataka katiba mpya ili kuondoa umasikini? Watu wengine mpaka kero, alafu unakuta jitu lenyewe ni jitu zima lakini la hovyo sana.
Hivi mkuu, Solutions za matatizo yaliyopo ni ujio wa katiba pekee??Watu wa mtwara na lindi wameshalipwa korosho zao? The answer is no,nani kawajibishwa ?hakuna .watu wamerudishwa kwenye umasikini kwasababu ya katiba mbuvu
Na uhakika itapunguza zaidi ya 50%Hivi mkuu, Solutions za matatizo yaliyopo ni ujio wa katiba pekee??
Kiukweli mkuu, kaa ukijua wazi wazi kuwa, hiyo siyo kweli kabisa
kwa sababu gani, Vyama vyetu hivi tulivyonavyo, vinakatiba madhubuti lakini matatizo ni mengi kuliko tunavyotaka kujiamisha kwamba katiba mpya itamaliza matatizo yetu yote
Tunaweka matumaini makubwa mno kwenye katiba badala ya kuandaa viongozi ili wawe waadirifuKenya Uganda na Afrika kusini Zina katiba Bora kabisa lkn changamoto haziishi.Kinachosumbua hapa ni kuwa wapinzani wanataka kutumia hiki kuleta vurugu sambamba na kuamini katiba mpya itawafanya wao kuingia madarakani kirahisi Kisha wafanye yao